Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA

Status
Not open for further replies.
kama ndivyo basi makanisa na misikiti ndio wahesabu watu/waumini wao kama dhamira ni kwa matumizi ya imani

sensa ni kwa ajili ya kujua idadi ya watu na itikadi zao za dini.sio jambo jipya Tanzania wala duniani kwa ujumla.ukijaribu kutaka kujua idadi ya watu nchi yoyote na itikadi za dini zao unapata.swali kwaninï iwe ajabu sasa na hapa Tanzania?kuna jambo nyuma ya pazia.
 
nasubiri nione kama kikwete,bilal,zungu,zitto,makamba,kigoda km nao watakataa kuhesabiwa hakiamungu ngoja nione halafu muwateme...!
 
Power power power! Hata siku moja power will never go to the unprepared! Mifano ipo watu wasio na uwezo wakapewa power huwa wanafanya nini.
 
Nimepata tabu kwa muda ili kujaribu kufikiri na kupata sababu na jibu la maana la waislamu kususia hesabu ya watu nchini yaani sensa. Bado sijaelewa idadi ya watu, ama hesabu ya watu inahusiana vipi na imani za kidini wakati wanaohesabiwa ni watanzania wenye dini mbali mbali walionea na kusambaa nchini kwetu.

Je! Serikali ikichakachua idadi kamili ya watu wa dini fulani na kutoa idadi tofati kutakuwa na faida gani? Je! idadi ndogo ya waumini inasababisha kupungua imani ya watu kwa dini yao? Ukiwa na imani unaweza kuwa na dini yako peke yako, au ya watu sita tu na bado ikawa dini bila ya halaiki ya watu.

Au lengo letu ni kushindana idadi na watu wa imani nyingine? Hiyo itakuwa na faida gani kwetu.

Ikiwa ni hivyo, ushauri wangu ni huu.

Tuiache sensa ya serikali ifanye kazi yake, tukubali kuhesabiwa. Baada ya hapo tufanye sensa yetu ya waislamu tu. Nina hakika kila mtaa haukosi kuwa na shekhe ambaye anaweza kupita na kujua idadi ya waislamu walio katika mtaa wake, ndani ya kipindi kifupi tunaweza kupata majibu kwa kupitia sensa yetu ya uhakika. Maustadhi na mashekhe wetu mbona mengi mnayapigania na kufanikiwa? Je, sensa maalumu kwa ajili ya waislamu tu, itawashinda?

Hakuna sababu ya kutaka kujua idadi yetu kwa kubebwa na sensa ya serikali wakati uwezo tunao watu wakihamasishwa. Huo ndio ushauri wangu, isije ikawa tunafanya mambo kinyume na demokrasia na matakwa ya jamii inayotuzunguuka.
tanzania haina dini... sasa kuna shida gani ya kuondoa kipengele cha dini kwenye sensa??
 
Waislam Hawaishi Kulalamika..LEO Rais wa Muungano ni MWISLAM..Makamu wa Rais ni MWISLAM..Kule Zanzibar Rais ni MWISLAM,Makamu wa Rais Nzanzibar ni MWISLAM..Halafu Mnalalamika eti Mfumo Kristo,hamupewi Nafasi..Hivi hizi nilizozitaja Si Ndiyo Nafasi TOP kuliko zote?..Mbona Wakristo Hawajalalamika kuwa Viongozi wa nchi ni waislam?..Halafu assume sensa ikachukuliwa pamoja na kipengele cha dini..Matokeo yakitoka Tofauti na Matarajio ya waislam(kwa mfano wakristo wakawa wako wengi kitakwimu),Kesho yake tu Waislam watakuwa barabarani Kupinga Matokeo na Kuandamana..JAMANI HEBU FANYENI SENSA YENU WENYEWE HAKUNA ANAYEWAKATAZA..Full Stop
hao ilio wataja labda ndugu zetu wanaelewa wameisha badili dini na kuwa watu wa mlengo wa kushoto.
kuhusu nia ya kujua idadi, ili kama wakiwa wachache wapeane majukumu ya kuzaa watoto sita sita ili wawe wengi, sasa hivi bila hizo data wanashindwa kupanga hiyo mipango.
mwisho ni tegemeo langu Raisi ataongea na mufti kuu ili ampe somo kuhusu umuhimu wa sensa , na hakuna haja ya kususia.au Prof Shivji itabidi awape somo kidogo ndugu zetu
 
sensa ni kwa ajili ya kujua idadi ya watu na itikadi zao za dini.sio jambo jipya Tanzania wala duniani kwa ujumla.ukijaribu kutaka kujua idadi ya watu nchi yoyote na itikadi za dini zao unapata.swali kwaninï iwe ajabu sasa na hapa Tanzania?kuna jambo nyuma ya pazia.

Ni kweli kabisa physics, nimesoma hoja za wachangiaji wote naona wote wanaopinga hili jambo kama vile kuna maslahi flani wanayatetea. Vinginevyo sioni ugumu wa suala hili hata kidogo, na kwa ujumla hoja zao hazina uzito wala mantiki. Nitazieleza hoja chache tu kama ifuatavyo:

1. Waislamu watafute idadi yao wenyewe: hoja hapa si kwamba waislamu wanataka idadi yao, bali wanataka idadi rasmi ya watanzania kwa dini zao. Wakijihesabu wao bado haitasaidia kujua makundi ya dini nyingine officially. Wengine wanadai kuwa dini si waislamu na wakristo tu kuna dini za asili na wapagani, tuambieni wapagani ni wangapi? dini asilia ni wangapi? Na hii ni takwimu ya kawaida tu kwa nchi na nchi nyingi duniani zina data hizi na zinapatikana kwenye sensa zao. (angalia country profiles za nchi katika websites za cia, undp, worldbank, n.k.). Hoja ni kuwa kipengele cha dini kikiwekwa itakuwa ndiyo official data ya Tanzania as of 2012. Sioni tatizo na nadhani wanaopinga na kujiona eti wamekwenda shule dunia itawacheka kwa kupinga jambo la kawaida mno.

1. Waislamu wakijua wako wangapi so what? Kwani wamarekani, waingereza, wajerumani, wa Indonesia n.k. tunajua idadi ya dini zao mbali mbali so what? kusema hivyo si maanishi kwamba haina maana ina maana na partly maana hiyo ndiyo inayowafanya wanaopinga waendelee kupinga. Maana yake ni kubwa mno baadhi yake ni kutuwezesha kufanya country and regional comparisons of religious groups na preveiling social relations which affect their lives and the way they relate with others. Mf. unasema Northern Ireland majority ni Catholics, while England majority ni Anglican. Vile vile unasema nchi yenye waislamu wengi duniani ni Indonesia n.k. Kwa nchi takwimu za dini zina maana sana hata kwa serikali kwa mfan; katika mipango miji ni serikali inayotayarisha maeneo ya matumizi mbali mbali kama makazi, biashara, taasisi, viwanda, na maeneo ya ibada (misikiti, makanisa). Maeneo ya ibada hutengwa kwa kuangalia idadi ya waumini wa dini husika. Usipojua idadi yao unaweza ukaweka eneo kubwa na kuyanyima matumizi mengine yanayohitaji ardhi zaidi, au ukaweka eneo dogo ambalo halitoshelezi mahitaji ya waumini na hivyo kuleta msongamno ambao baadae huleta mizozo isiyokuwa ya lazima.

3. Wakatoliki wanajua idadi yao: Kwani wakristu wote ni wakatoliki? mbona hamjasema Anglican, Lutheran, SDA, Assemblies of God nao wanajua idadi yao. Na hata hao wakatoliki mbona sijaona hata mmoja wenu amesema precisely wako milioni ngapi Tanzania, huko ndo kujua idadi yao. Na zaidi ya hayo wasio na dini nao wanaipataje idadi yao maana wao hawana kanisa la kuwafanya wahesabiane kwa matumizi yao ya kidini.

4. Serikali kuwafanyia waislamu sensa: Kilichopo ni kwamba serikali inataka kufanya sensa ambao ni utaratibu wa kawaida wa nchi kujua idadi ya watu wake kila baada ya miaka kumi. Wanachoomba waislamu ni kuingizwa kipengele cha kujua dini ya mtu katika sensa ambayo inataka kufanyika. Jambo hili haliongezi wala kupunguza gharama ya serikali kufanya sensa. Ingekuwa serikali imekwisha fanya sensa, halafu waislamu wanaomba ifanyike tena hapo kidogo ungeweza kusema wanataka kufanyiwa, lakini si hivyo.

5. Waislamu kutokusoma: Sioni mantiki ya kuingiza suala la kusoma katika hoja hii. Nadhani inataka kutumika kama kisingizio kukwepa au kupindisha hoja ya msingi. Siku zijazo nitaanzisha thread tujadili mnaposema waislamu hawakusoma maana yake hasa ni ipi, na hivi kweli sentesi hiyo ina nguvu leo kama ilivyokuwa mwaka 1961?

6. Totofautishe usomi na kufundishwa: Kuna tofauti kati ya msomi (intellectual) na aliyefundishwa (trainee/trained person). Trained person hufanya na kuamua mambo kwa kufuata vile alivyo fundishwa, wakati intellectual hufanya na kuamua mambo kwa kufuata real and genuine facts hata kama zitapingana na dini, kabila, kundi, mkoa au kanda anayotoka, n.k. Nikitazama michango katika hoja hii naona wachangiaji wengi wanafanana zaidi na trained person kuliko intelectuals, ingawa wanawalaumu waislamu kuwa hawakusoma. Nadhani kusoma kwenye manufaa ni kuwa intellectuals na sio trainees.

Mtanzania Makini
 
Sawa! lakini itambulike officially na Serikali.
Na kama serikali inaweza kugharimia ufanyaji wa sensa , vilevile hawa Masheikh watakaofanya hii kazi wagharimiwe na Serikali.

yaleyale ya mahakama ya kadhi.
 
Hii yote inasababishwa na tabia ya attention-seeking kama ya binti-kigori aliyevunja ungo. Yaani kaa watoto wa kiume mmekaa barazani atajipitishapitisha hapo weeee, ataenda na kurejea na kubadili nguo mara 4 ndani ya muda wa nusu saa ilimradi tu mumpigie miluzi na kumuimbisha!

Serikali kupitia NBS ilishasema idadi ya mgawanyiko wa imani haina matumizi nayo, sasa hawa sijui ni wa wapi wanaolazimisha hiyo data ikusanywe. Kwa wale mlofuta ujinga mnaeza mkaelewa mfano wa mtu anayefanya risechi kuhusu kadhia au tabia fulani, una kuwa na maswali yako ya dodosa, halafu jidubwana jingine linakulazimu uweke maswali yasiohusu risechi yako..wewe utalichukulia hili rijamaa kaa rina akiri timamu? huo ni mfano tu.
 
Sasa ndio umeandika nini? anyway kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake! UTAFITI/ukusanyaji wa takwimu zozote si halali isipokuwa uwe umepewa kibali na serikali kupitia mamlaka husika. kama ulikua hujui.

Sawa, achilia mbali kibali. Hata iwe kwa leseni, mbona tunaomba vibali vya maandano? iweje vingine viwe na ugumu?
 
Nimepata tabu kwa muda ili kujaribu kufikiri na kupata sababu na jibu la maana la waislamu kususia hesabu ya watu nchini yaani sensa. Bado sijaelewa idadi ya watu, ama hesabu ya watu inahusiana vipi na imani za kidini wakati wanaohesabiwa ni watanzania wenye dini mbali mbali walionea na kusambaa nchini kwetu.

Je! Serikali ikichakachua idadi kamili ya watu wa dini fulani na kutoa idadi tofati kutakuwa na faida gani? Je! idadi ndogo ya waumini inasababisha kupungua imani ya watu kwa dini yao? Ukiwa na imani unaweza kuwa na dini yako peke yako, au ya watu sita tu na bado ikawa dini bila ya halaiki ya watu.

Au lengo letu ni kushindana idadi na watu wa imani nyingine? Hiyo itakuwa na faida gani kwetu.

Ikiwa ni hivyo, ushauri wangu ni huu.

Tuiache sensa ya serikali ifanye kazi yake, tukubali kuhesabiwa. Baada ya hapo tufanye sensa yetu ya waislamu tu. Nina hakika kila mtaa haukosi kuwa na shekhe ambaye anaweza kupita na kujua idadi ya waislamu walio katika mtaa wake, ndani ya kipindi kifupi tunaweza kupata majibu kwa kupitia sensa yetu ya uhakika. Maustadhi na mashekhe wetu mbona mengi mnayapigania na kufanikiwa? Je, sensa maalumu kwa ajili ya waislamu tu, itawashinda?

Hakuna sababu ya kutaka kujua idadi yetu kwa kubebwa na sensa ya serikali wakati uwezo tunao watu wakihamasishwa. Huo ndio ushauri wangu, isije ikawa tunafanya mambo kinyume na demokrasia na matakwa ya jamii inayotuzunguuka.

Unajua maana ya zoezi la sensa, au unasoma tu kwenye madudu ya mtandaoni? Kwa taarifa yako, huwezi kufanya "sensa" kwa kujihesabu kundi fulani moja tu bila ya kuwahusisha Watu wa makundi tofauti. Kwa maana hii, Waislamu hawawezi kujihesabu wao wenyewe tu misikitini bila kuwahusisha watanzania wenye imani tofauti, na hesabu zao kuchukuliwa kama ni halali kitakwimu. Kama ingekuwa ni rahisi namna hiyo, nadhani hata BAKWATA miaka mingi wangefanya "sensa" yao na kuja na takwimu zao za idadi ya Waislamu Tanzania, achilia Waumini wa dini na madhehebu tofauti, ambao nao wangefanya "sensa" zao kivyao, na kuja na takwimu zao za Waumini.
 
mimi ninavyo jua waislamu ni watiifu saana kwa viongozi wao, hivyo iwe bakwata au misikiti ikisema leo hii, inataka waumini wao wakajiandikishe majini, mahali wanayo ishii, mke , mume, miaka basi watajitokeza na kupata idadi yao, baada ya hapo ikishafanyika sensa kuu (taifa) basi unafanya hesabu ya kutoa unapata hizo dini nyingine ni wangapi? au utajua % ya waislamu kulinganisha na idadi ya wa tanzania.
Dini zingine hilo la idadi haliwati hofu, mkisema makafiri ni 25% sawa, 35% sawa, waumini wa kweli-waislamu ni 75% sawa.
 
Unajua maana ya zoezi la sensa, au unasoma tu kwenye madudu ya mtandaoni? Kwa taarifa yako, huwezi kufanya "sensa" kwa kujihesabu kundi fulani moja tu bila ya kuwahusisha Watu wa makundi tofauti. Kwa maana hii, Waislamu hawawezi kujihesabu wao wenyewe tu misikitini bila kuwahusisha watanzania wenye imani tofauti, na hesabu zao kuchukuliwa kama ni halali kitakwimu. Kama ingekuwa ni rahisi namna hiyo, nadhani hata BAKWATA miaka mingi wangefanya "sensa" yao na kuja na takwimu zao za idadi ya Waislamu Tanzania, achilia Waumini wa dini na madhehebu tofauti, ambao nao wangefanya "sensa" zao kivyao, na kuja na takwimu zao za Waumini.

Inaonekana mzigo wa midevu umekuzidi kiasi unashindwa kuona na kusoma kwa makini. Rudi tena pale usome uelewe. Nimesema tukubali sensa, tuhesabiwe. Baada ya hapo, tufanye sensa ya waislamu sasa ili kujua idadi yetu. Sawa! Au bado?
 
Wee unaijua mantiki au unaisikia msikitini au labda kwenye madrassah enzi za vidudu? Sensa ya Waislamu wao kwa wao haikubaliki kimantiki kulingana na taratibu za kitakwimu za kisasa. Sasa usije kutuletea maana ya "sensa" kulingana na Kuran, maana kama ni hivyo, kwa nini mtegemee "sensa" inayohusisha Watanzania wote? Jee, mmeshafanya "sensa" zenu na kuweka wazi takwimu zake kutokana na vigezo vya Kurani? Allah anasema nini kuhusu vigezo vya "sensa" halali? Iweje mng'ang'anie vigezo vya sensa vilivyowekwa na "makafiri" na hata kugoma kushiriki kwenye "sensa" kwa vile muonekano wenu hauendani na misingi ya "sensa" zinazokubalika kisasa, na ilhali nyie hamjatoa matokeo ya "sensa" halali kulingana na imani yenu?
 
Sawa! lakini itambulike officially na Serikali.
Na kama serikali inaweza kugharimia ufanyaji wa sensa , vilevile hawa Masheikh watakaofanya hii kazi wagharimiwe na Serikali.
Hakika hii ni mpya ya mwaka. Hivi kweli serikali igharamie posho ya masheikh? Aibu!!
 
ukichagua kazi ya dini ni sharti umuombe MUNGU akujaalie hekima,busara na unyenyekevu ili uwaongoze waumini wako vizuri.siyo vizuri kwa kiongozi wa dini kuwalazimisha waumini wake kupingana na serikali kwa mambo ambayo hayana msingi wowote.viongozi wa dini wawe mstari wa mbele kuwahimiza watu wao wamjue MUNGU wao kwa dhati na wawaunganishe katika kujiletea maendeleo. hivi ukijua kuwa waislamu wako mil 20 ndio hosptali itajijenga au ndio mwanzo wa kutaka kuilazimisha serikali iwajengee hosptali kwa kigezo kwamba ni wengi?
 
Hakika hii ni mpya ya mwaka. Hivi kweli serikali igharamie posho ya masheikh? Aibu!!
Lilikuwa jibu la swali ambalo ni mpya ya mwaka!
JumaKidogo
tuiache sensa ya serikali ifanye kazi yake, tukubali kuhesabiwa. Baada ya hapo tufanye sensa yetu Waislamu tu. Nina hakika kila mtaa haukosi kuwa na shekhe ambaye anaweza kupita na kujua idadi ya Waislamu walio katika mtaa wake, ndani ya kipindi kifupi tunaweza kupata majibu kwa kupitia sensa yetu ya uhakika.
Sideeq
Sawa! lakini itambulike officially na Serikali.
Na kama serikali inaweza kugharimia ufanyaji wa sensa , vilevile hawa Masheikh watakaofanya hii kazi wagharimiwe na Serikali.
- Atleast hao Ma-sheikh watakuwa wanalipwa kwa kazi walioifanya na muda wao waliopoteza kuliko Wakatoliki ambao wamejikalia tu na kupewa pesa ya bure na Serikali kupitia MOU, pesa ambayo inakusanywa katika kodi inayolipwa na Muislamu pia! aibu!
 
Kama waumini wote wangekuwa wanakwenda kuswali msikitini na wakristo wote kwenda makanisani sensa ingekuwa nyepesi ..... naona kazi ya kwanza ya dini ni kuwarejesha waislamu na wakristo wote kwenda nyumba za ibada ili wapate sensa yao. wamrudie Mungu hesabu itakuwa rahisi wala hakutakuwa na haja ya kuisumbua serikali ambayo idadi ya waumini wa dini haina umuhimu katika kupanga maendeleo ya watu kama vile barabara, umeme, maji.
bado sensa itakuwa nyepesi. Muumini ni yule anayetimiza au anayejaribu kufuata misingi ya dini yake. Kama Joseph haendi kanisani hata siku muhumu, kanisa alimtambui Joseph kama Mkristu. Vilevile kwa Waislam, kama Abubakar haendi msikitini hata zile siku muhimu, Msikiti haumtambui Abubakar kama Mu-Islam. Hapa watu wanashindwa kutofautisha Muumini na mtu mwenye jina tu linalotumika na dini fulani.
 
Lilikuwa jibu la swali ambalo ni mpya ya mwaka!
JumaKidogo
tuiache sensa ya serikali ifanye kazi yake, tukubali kuhesabiwa. Baada ya hapo tufanye sensa yetu Waislamu tu. Nina hakika kila mtaa haukosi kuwa na shekhe ambaye anaweza kupita na kujua idadi ya Waislamu walio katika mtaa wake, ndani ya kipindi kifupi tunaweza kupata majibu kwa kupitia sensa yetu ya uhakika.
Sideeq
Sawa! lakini itambulike officially na Serikali.
Na kama serikali inaweza kugharimia ufanyaji wa sensa , vilevile hawa Masheikh watakaofanya hii kazi wagharimiwe na Serikali.
- Atleast hao Ma-sheikh watakuwa wanalipwa kwa kazi walioifanya na muda wao waliopoteza kuliko Wakatoliki ambao wamejikalia tu na kupewa pesa ya bure na Serikali kupitia MOU, pesa ambayo inakusanywa katika kodi inayolipwa na Muislamu pia! aibu!
Ambayo muislam anaitumia kwenye shughuli za afya/elimu ya juu na shughuli nyingine za jamii bila kubaguliwa...aibu kubwa
 
bado sensa itakuwa nyepesi. Muumini ni yule anayetimiza au anayejaribu kufuata misingi ya dini yake. Kama Joseph haendi kanisani hata siku muhumu, kanisa alimtambui Joseph kama Mkristu. Vilevile kwa Waislam, kama Abubakar haendi msikitini hata zile siku muhimu, Msikiti haumtambui Abubakar kama Mu-Islam. Hapa watu wanashindwa kutofautisha Muumini na mtu mwenye jina tu linalotumika na dini fulani.
Kwenye ajira na elimu ambapo Waislamu wanadai kubaguliwa pia hawataki kujua aidha Muislamu huyu ni msafi au si msafi!......una jina la Kiislamu basi inatosha kubaguliwa!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom