Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA

Status
Not open for further replies.
Haya, Waislam wako 98.6953% of the total population iliyobaki ni hizo dini nyingine. Waislam wenzangu nadhani tumemaliza. Tuangalie mambo mengine bajeti vp mnaionaje waislam wenzangu
 
Nimepata tabu kwa muda ili kujaribu kufikiri na kupata sababu na jibu la maana la waislamu kususia hesabu ya watu nchini yaani sensa. Bado sijaelewa idadi ya watu, ama hesabu ya watu inahusiana vipi na imani za kidini wakati wanaohesabiwa ni watanzania wenye dini mbali mbali walionea na kusambaa nchini kwetu.

Je! Serikali ikichakachua idadi kamili ya watu wa dini fulani na kutoa idadi tofati kutakuwa na faida gani? Je! idadi ndogo ya waumini inasababisha kupungua imani ya watu kwa dini yao? Ukiwa na imani unaweza kuwa na dini yako peke yako, au ya watu sita tu na bado ikawa dini bila ya halaiki ya watu.

Au lengo letu ni kushindana idadi na watu wa imani nyingine? Hiyo itakuwa na faida gani kwetu.

Ikiwa ni hivyo, ushauri wangu ni huu.

Tuiache sensa ya serikali ifanye kazi yake, tukubali kuhesabiwa. Baada ya hapo tufanye sensa yetu ya waislamu tu. Nina hakika kila mtaa haukosi kuwa na shekhe ambaye anaweza kupita na kujua idadi ya waislamu walio katika mtaa wake, ndani ya kipindi kifupi tunaweza kupata majibu kwa kupitia sensa yetu ya uhakika. Maustadhi na mashekhe wetu mbona mengi mnayapigania na kufanikiwa? Je, sensa maalumu kwa ajili ya waislamu tu, itawashinda?

Hakuna sababu ya kutaka kujua idadi yetu kwa kubebwa na sensa ya serikali wakati uwezo tunao watu wakihamasishwa. Huo ndio ushauri wangu, isije ikawa tunafanya mambo kinyume na demokrasia na matakwa ya jamii inayotuzunguuka.

Huu ushauri wako wa bure bora ukaenao utakusaidia mbeleni.
 
Sawa! lakini itambulike officially na Serikali.
Na kama serikali inaweza kugharimia ufanyaji wa sensa , vilevile hawa Masheikh watakaofanya hii kazi wagharimiwe na Serikali.

Tambua kua idadi ya watu katika dini yoyote haina manufaa kwa serikali ya Tanzania, hivyo haiwezi kugharimia sensa yoyote ya kidini hata siku moja. Kitu kidogo tu kama mnataka jua mko wangapi kila MSIKITI ulete idadi ya waumini wake na mjumlishe. Sisi hatutaki hata kujua mko wangapi coz haina mantiki kimaendeleo ya Tanzania yetu.
 
Sawa! lakini itambulike officially na Serikali.
Na kama serikali inaweza kugharimia ufanyaji wa sensa , vilevile hawa Masheikh watakaofanya hii kazi wagharimiwe na Serikali.
Makubwa! Kumbe kelele zoooooote, mnataka posho tu! Idadi yenu itambulike vp na Serikali wakati Serikali haizihitaji takwimu hizo? Jihesabuni wenyewe kwa afya zenu na kwa gharama zenu. Wenzenu Wakristo wa Roma wako so organised, kuanzia ngazi ya Jumuiya ndogo ndogo(mitaa) - Kigango - Parokia - Jimbo - Taifa. Kila mwaka huhesabiana bila gharama yoyote, ni kiasi cha tamko tu kuwa leteni idadi ya waumini inapelekwa within one week imeshafika kwa Mwadhama Kardinali Pengo na kujulikana wako wangapi bila gharama yoyote, ambaye naye huwasilisha Vatican kwa ajili ya takwimu ya Waroma wote duniani. Acheni kuendekeza ugonjwa wa wanasiasa wa posho, na kutaka "msaada kwenye tuta" baada ya kudandia madodoso yasiyo yenu, ambayo hata hivyo hamchelewi kudai yamechakachuliwa. Jihesabuni wenyewe kule masjidi kwa swadaka zenu bana.
 
Juma Salaam,
Kwanza sina shaka juu ya uislamun wako kama wengine humu JF, wanaojifanya waislamu kumbe ni makafiri wazuri.
Kimsingi hata mimi binafsi siathiriki na sensa na matokeo yake.
lakini unapaswa kuangalia mbali zaidi ya hoja zako hapo juu. Wakristo wanataka Waislamu wafikiri kama wewe ulivyofanya, kwa hiyo itawahakikishia dhulma bila bughdha
  1. Madai ya msingi ya Waislamu ni kuwa Wakristo kwa kuwa ndio wengi serikalini na kwenye ufanyaji maamuzi wanatumia mwanya wa kutokuwa na takwimu sahihi kuhalalisha wao kuwa wengi kila mahali.
  2. kama idadi ya watu wa dini fulani sio issue, kwa nini izungumzwe ile ya makadirio?
  3. Kama kuna haja ya kuwa na makadirio (estimates) kwanini kusiwe na real data?
  4. Pia kuna confusion inayotokana na records za nyuma, mwanzo waislamu walikuwa majority TZ, leo kwa nini wawe 35%?
Mwisho KWA NINI TUNAOGOPA KUPIMWA? wakati tunasisitiza watu wakapimwe ukimwi! Hapa tunaogopa ukweli?
Mtaandika sana, mtapayuka sana...mwisho wa siku matahesabiwa kama watanzania wengine bila kuwepo kigezo cha dini kwenye sensa..Iweke hii post kama kumbukumbu tutairejea baada ya zoezi la sensa...
 
Kuhusu kuwepo wakristu wengi serikalini ni kwamba ile iahitaji Elimu Dunia, ambayo wengi wetu waislamu hatukuitilia maanani na kubaki kuimba na kukariri elimu Ahera. Hapo tu ndo tulichezea shilingi chooni.
 
Taabu ya hawa wenzetu hata ukiwapa uongozi wa nchi,yaani Rais,makamu,waziri mkuu na mawaziri wote,makatibu wote,wakurugenzi wa idara wote,wakuu wa mikoa,wilaya wote,wakurugenzi wa mashirika ya umma wote na kadha wa kadha bado hawa jamaa zetu wataendelea kulalamika na kudai mfumo kristo unatawala,frankly is very hard to deal with these characters,they are funny and useless!

Punguza chuki uongeze siku za kuishi mkuu.
 
Waislam wana haki kama Watanzania na wanalipa kodi ni haki yao kuhesabiwa na serikali hakuna tatizo.

HAYA ni mawazo ya kipimbi na mafupi kama maisha ya funza. Jichangisheni tu kama mnataka kujua mko wangapi sio serikali itumike kwa mabo yasiyo na msingi katika maendeleo. Una haki ya kujihesabu pia sio upewe hela ya kujihesabu.....
 
Sawa! lakini itambulike officially na Serikali.
Na kama serikali inaweza kugharimia ufanyaji wa sensa , vilevile hawa Masheikh watakaofanya hii kazi wagharimiwe na Serikali.

Mkuu, sasa ndo nimeelewa kwanini mnataka kwenye sensa hii serikali iweke kipengere cha dini, kumbe issue hapa mnataka kujua mko wangapi kwa gharama za serikali? Nyie wenyewe hamna kabisa mbinu mbadala za kujuana, mbona wakristo wanaweza? Niliwahi kumsikia askofu 1 wa kanisa la walokole la EAGT mahali fulani akitaja idadi ya waumini wa kanisa analo liongoza nchini Tanzania, Burundi, Zambia na Rwanda, hivi naye alisaidiwa na serikali kujua hayo? Uvivu mwingine bana, siku nyingine mtakuja kudai serikali iwawekee akili kichwani kama Wakristo, mnadai hata visivyo daiwa!
 
Mtaandika sana, mtapayuka sana...mwisho wa siku matahesabiwa kama watanzania wengine bila kuwepo kigezo cha dini kwenye sensa..Iweke hii post kama kumbukumbu tutairejea baada ya zoezi la sensa...

Naona Chadema wote wamerudi nyumbani CCM halafu useme mtaitoa CCM madarakani thubutu! Saizi nyie Chadema mnafuata amri ya Wassira kuhusu sensa na nyie ndio mnapambana kweli, chezea CCM wewe.
 
Juma Salaam,
Kwanza sina shaka juu ya uislamun wako kama wengine humu JF, wanaojifanya waislamu kumbe ni makafiri wazuri.
Kimsingi hata mimi binafsi siathiriki na sensa na matokeo yake.
lakini unapaswa kuangalia mbali zaidi ya hoja zako hapo juu. Wakristo wanataka Waislamu wafikiri kama wewe ulivyofanya, kwa hiyo itawahakikishia dhulma bila bughdha
  1. Madai ya msingi ya Waislamu ni kuwa Wakristo kwa kuwa ndio wengi serikalini na kwenye ufanyaji maamuzi wanatumia mwanya wa kutokuwa na takwimu sahihi kuhalalisha wao kuwa wengi kila mahali.
  2. kama idadi ya watu wa dini fulani sio issue, kwa nini izungumzwe ile ya makadirio?
  3. Kama kuna haja ya kuwa na makadirio (estimates) kwanini kusiwe na real data?
  4. Pia kuna confusion inayotokana na records za nyuma, mwanzo waislamu walikuwa majority TZ, leo kwa nini wawe 35%?
Mwisho KWA NINI TUNAOGOPA KUPIMWA? wakati tunasisitiza watu wakapimwe ukimwi! Hapa tunaogopa ukweli?

Ndugu yangu, sensa, wala idadi ya watu si suluhu ya matatizo ya waislamu. Wala sensa si mkombozi wa waislamu. Hata kama tungekuwa wengi ambao tunawazidi wakristo mara sita au kumi. Kama hatuna elimu na wasomi wa kutosha katika dini yetu bado tutalalamika.

Cha msingi ni kuamka sasa na kuanza kutafuta tatizo lilianzia wapi, chanzo kilikuwa nini mpaka tumeathirika kwa kiasi kikubwa na kutokuwa na elimu dunia.

Nadhani historia iko wazi tangu zamani watoto wa kislamu hawakushiriki kwa karibu sana elimu dunia. Yatupasa tubadilike sasa, elimu ya ahera kwa dunia ya sasa haimsaidii sana mtu. Tuangalie namna ya kubadili mfumo wa elimu yetu waislamu. Hiyo itatusaidia kwenda sambamba na dunia ya sasa bila kulalamika,
 
tatizo ni elimu baba kwa wengi wa viongozi wa hii dini... leo watasusi sensa...kesho watatusia mchakato wa katiba..kesho kutwa watasusia uchaguzi mkuu mwisho wa siku wataanza kususiana wao kwa wao na kutafuta nani mchawi wa mabo yao "KIPOFU HAWEZI KUMUONGOZA KIPOFU MWENZI..WOTE WATATUMBUKIA SHIMONI"~ maneno ya YESU haya bwana
 
Juma umetoa ushauri mzuri ningekuwa na huwezo we ungekuwa sheikh mkuu tanzania.
 
Sawa! lakini itambulike officially na Serikali.
Na kama serikali inaweza kugharimia ufanyaji wa sensa , vilevile hawa Masheikh watakaofanya hii kazi wagharimiwe na Serikali.
Kuna dini zingine fahari yake ulalamishi na masononeko, mbona wapagani kila siku wakitukanwa na hizi dini zenu za kuletwa na wakoloni (waalabu na wazungu) lakini hawajawahi kunyanyua midomo yao kulalamika wala hawana wasiwasi na uwingi wala uchache wao! lakini kila siku utasikia wakristo wakisema hawa wapagani wanaamini mashetani na waislamu nao wakiwaita makhafir Achaneni na dini za kasumba za kikoloni ndiyo maana hamjiamini, ni infiliority complex hiyo. wapagani watakubali kgharamia sensa ya waumini wenu wakati mwawatukana kila siku?
 
Naona Chadema wote wamerudi nyumbani CCM halafu useme mtaitoa CCM madarakani thubutu! Saizi nyie Chadema mnafuata amri ya Wassira kuhusu sensa na nyie ndio mnapambana kweli, chezea CCM wewe.

Mkuu umeona enhe! hapa Wassira ni bonge la kiongozi mbele ya Wahafidhina wa CDM! ama kweli ni vigumu kutofautisha kati ya CDM, kanisa na CCM ! (pole Ritz).

Kikwebo.
 
Sawa! lakini itambulike officially na Serikali.
Na kama serikali inaweza kugharimia ufanyaji wa sensa , vilevile hawa Masheikh watakaofanya hii kazi wagharimiwe na Serikali.

Then ikitambulika na serikali ili iwaje? Zijengwe barabara, hospitali, shule kwa ajili ya waislam tu? Zitungwe sharia za waislamu tu? Ianzishwe mikoa ya waislam tu? Hapa hii ni sensa ya serikali kwa watu wake (na nyie mkiwepo).
Tatizo mnafikiria kwa kutumia masaburi na kutafuta sababu za kupigana! Mkitaka hayo nendeni somalia mkachapane!
 
Ficha ujinga wako kuliko kujifanya muislamu kumbe kaf...r mkubwa weye.Kawa danganye wajinga wenzio lazima kipengele cha dini kiwepo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom