Ushauri: Ununuaji wa magari

Maelezo mazuri sana na msaada kwa wengine wengi. Nimeyapenda na yamenifungua akili. Asante. Gu senks gwako gwingine nakugongea pale pembeni.

MwanaHaki
 
Hi JF,

Nataka ninunue gari, kama wana JFnisaidieni mawazo yenu ni gari ipi ni nzuri

- Inayotumia mafuta kidogo sana kama pikipiki

- Spare zinapatikana kwa urahisi kabisa

Sina uwezo sana sitaki gari inayokula wese
 
Kuna jama yangu Japan kaniambia eti Startlet mwisho kutengenezwa ni mwaka 1999 hivyo hakuna ya 2000.

Wakuu hii ni kweli au ni porojo zake tu huyu jamaa kwa anajishughulisha na uletaji wa magari used kutoka Japan na yeye hana hiyo gari kwenye stock yake wakati kuna jamaa wengine kwenye yard yao wana Starlet ya mwaka 2002
 
Ukweli ni kwamba starlet walishaacha kuzitengeneza platform yake wanatengenezea Vitz. Kama unataka gari imara la mizunguko ya mjini kamata gari aina ya Toyota ushauri wangu chukua Vitz au kama khali inaruhusu nunua Toyota IST ni kama Vitz ila body ndo tofauti ingawa iko juu kwenye bei.
 
Nashukuru kwa mawazo yenu ila VVTI maana yake nini?? Nitafute Starlet
Pia hapa mjini kweli unaweza kupima mileage yaani 1litre per how many km? na hizi foleni?

Toyota IST ziko juu sana
 
Mkuu ni kweli Starlet hazizalishwi tena na mbadala wake ni Vitz ambayo nadhani ni bora kwako kutokana na vigezo vyako.na hata ukiipata nyingi ni zile zaidi ya miaka 10 ambapo kodi yake ni 100%. Zipo pia duet na swift ni sawa na Vitz sema tatizo lao ni vipuri vinasumbua upatikanaji wake
 
Achana na Starlet maana ni za kuanzia 90 to 1997 so dumping fee yake ni bora ununue Toyota IST ya 2002 kuendelea, ili ukwepe dumping fee.
 
Achana na mafuta si tofauti sana mimi natumia Nissan Hard body lt moja km 10-12 inategemea na foleni! so chukua kitu roho inapenda
 
Usinunue gari, panda daladala. Very economy. Mwenzio napanda daladala na ninaonjoi kama wenye ma-vogue yao.
 
Back
Top Bottom