Ushauri: Ununuaji wa magari

JMF,
Maelezo Mazuri saana hivi cleaening and forward agent hapa anasaidia nini? Je ni kama humudu porukushani ya bandari au? Ufafanuzi tafadhali
 
Tumia beforward mimi nimepata langu juzi 7/6/2016 , niliagiza mwezi wa April. Kabla hujalipa unaenda bank Exacutive banking ambapo unaweza uliza na wakachek kama hiyo bank unayotaka kulipia ipo na kama akaunti hiyo ni ya beforward.

Baada ya kuhakiishiwa unalipa na kutuma TT copy(telegraphic transfer copy) na baada ya hapo jamaa wanakutupia page yako (inakua kama website kwa ajili yako tu) wanakupa link katika email kisha utakuta kuna list ya steps zote zitazofanyika kabla gari halijakufikia na kitu cha kwanza utakuta sehemu ya malipo imejazwa 'completed" na kila watachofanya wanaandika na kukutumia email na inabidi uwe uanafungua email yako ili kupata taarifa kwa wakati maana kuna mamba otatakiwa kuwa unatoa ufafanuzi ili wajaze documents ila hata usipotoa wanaweza kukamilisha hata mimi kuna baadhi sikueleza ila wanauzoefu walijaza tu .

Mimi natoa ushuhuda humu maana nilipata woga baada ya mtu mmoja kunihofisha humu ila wengi walinipa moyo. Angalia sana kuna makampuni hawana ofisi TZ ila wanaweza kukuletea tu lakini incase kuna tatizo? Kama una ndugu au rafiki Dar Muombe aende ofisini kwao aombe akaunti namba na ulinganishe na uliyotumiwa na pia uloiona katika website yao, aombe na namba zao za mobile hawa jamaa wako vema na wana clear na kudeliver mpaka ulipo ukipenda.

Walinikatia bima ila wakasahau kama nataka ya Commercial na niliwapigia walifungua ofisi wikiendi kwa ajili yangu na kunikamilishia kwa haraka. Ndipo nikagundua kuwa siri ya mafanikio ya kampuni hii ni pamoja na ukarimu na huduma kwa wakati tena shirikishi. I recommend this.
 
Hao be forward hawawezi kufanya hizo kazi wao wenyewe wewe ukasubiri gari lako tu?
 
Kiongozi me naomba unisaidie kuhusu kuagiza gari Japan aina ya Toyota rav 4 old model ya mwaka 1998-1999. Mfano nimeangalia befoward ina range $2700 - 3000 mpaka nije niikamate itacost sh ngap ntashukuru sana.
 
JMF,
Maelezo yako mkuu yamenisaidia Sanaa! Kuna Harrier naishughulikia mwanzo nilikubali kulipa bei yao iliyopo kwenye website yao be forward na wakanitumia pro forma invoice kabisa ila niliposoma huu uzi nikarudi kubargain bei upya nikatoana nao CIF 2,932USD mpaka CIF 2,650USD na jumatatu nailipia, ni ya mwaka 1998 na ina 122,000km.

Tatizo sasa wadau wanasema odometer huchezewa napata mchecheto mpya tena wa kutaka kuuliza details za hii gari hasa kujua prior owner (s) na kuuliza wanithibitishie hili kama gari hii kama zake hizi ni sahihi!

Nahisi naelekea kuwa msumbufu kwao (my first time to buy a car japan/online) kwani kwenye bargaining ilifikia kipindi tukawa tunashindana bei tunaagana lakini wao wenyewe wakawa wananipigia simu tena ndo tukafikia makubaliano! Ila nilichopenda hao jamaa ni waungwana sana ukibargain nao kwa simu kuliko kupitia emails!

1. Lakini kwa uzoefu wenu wana JF be forward ukikamilisha maswala ya malipo gari hutumia wastani wa siku ngapi kufika Dar Es Salaam?

2. Pia ninaweza subiri gari ikifika ndo nianze kuprocess maswala ya kulipia kodi zote na ushuru au the soonest tu wakishanitumia the needed documents hata kama gari hawajaliship huku?

3. Pia muda gani ambao ni grace period kwa gari kukaa bandarini kama mnunuzi hajalilipia kodi mpaka pale serikali inapoamua kulipiga mnada?

Thanks, kweli JF ni kisima cha maarifa na upashanaji habari!

Nasubiri majibu yenu!
 
  • Thanks
Reactions: JMF
muuza ubuyu,
1. Gari huchukua wastani wa wiki 4 - 6

2. Ukishapokea documents toka Beforward, tafuta agent kwa ajili ya kuanza mchakato wa kulitoa gari. Wao huwa wana taarifa rasmi kuwa meli itafika lini, Ingawa nawe unaweza kui trace kupitia baadhi ya websites kujua meli ilipo. Agent atakuambia ni lini mchakato uanze, pia Beforward wanafanya hiyo kazi ukipenda kuwatumia for clearance.

3. Siku 7 za mwanzo huwa bure, baada ya hapo unaanza kulipia storage charge, kwa sasa sijui ni sh ngapi kwa siku. Wakati fulani ilikuwa elfu 20 kwa siku.
 
1. Gari huchukua wastani wa wiki 4-6

2. Ukishapokea documents toka Beforward, tafuta agent kwa ajili ya kuanza mchakato wa kulitoa gari. Wao huwa wana taarifa rasmi kuwa meli itafika lini, Ingawa nawe unaweza kui trace kupitia baadhi ya websites kujua meli ilipo. Agent atakuambia ni lini mchakato uanze, pia Beforward wanafanya hiyo kazi ukipenda kuwatumia for clearance.

3. Siku 7 za mwanzo huwa bure, baada ya hapo unaanza kulipia storage charge, kwa sasa sijui ni sh ngapi kwa siku. Wakati fulani ilikuwa elfu 20 kwa siku.
Asante sana kwa majibu mjarabu kiongozi, maelezo yako yatanisaidia kuepuka gharama zisizo za lazima, thanks! Niliwasiliana na be forward Dar Es salaam office wakaniambia clearance na vingine wanafanya na cost yao ni 295,000 Tsh. Hope nitawatumia wao wenyewe masuala yangu yote, thanks again!
 
muuza ubuyu,
Hongera mkuu. Usiwe na hofu kuagiza gari mwenyewe. Ni bei rahisi sana kuliko kununua toka kwenye yard. Kuhusu malipo, account ya BEFORWARD inafahamika dunia nzima. Nimekuwekea kama screenshot kwenye attachment.

Kuhusu status ya hiyo ODO METER angalia hapo hapo kwenye website yao ukisha click gari huonesha kama odometer has been changed. Ila kwa gari hiyo kama ingekuwa imeshabadilishwa isingekuwa imeshasoma hadi laki na zaidi. Hatua inayofuata ni wewe kwenda bank kufanya malipo kwa ku print hiyo Proforma Invoice na sales agreements.

Ukishalipia uta scan hiyo TT application form uwatumie kama bank hawatakupa TT hapo kwa hapo. Wakishapata hiyo, wao watasubiria uwatumie TT ukishaichukua bank na baada ya hapo watabadilisha status ya hilo gari kwakuandika Under offer. Malipo yakishawafikia itasomeka has been sold na watakutumia Export Certificate kwa njia ya email.

Hiyo itakuhakikishia kama odometer imeshabadilishwa au laa na pia kama gari ilishakuwa na owners wangapi maana itaonesha umbali ambao kila mmiliki alioanzia kutembelea na mwaka. Ipo kwa kijapani lakini inaeleweka upande wa chini kushoto.

Wakati huo utakuwa na Car Progress (CAP) page ambayo ni link watakayokuwa wamekutumia kwa email na uki click itafungua hiyo cap page yako ambayo ndo itakuwa sehemu salama ya kukupa maendelea ya kila hatua. Wakati huohuo utakuwa umeshatafuta clearing agent ambaye utamkabidhi hiyo Final Invoice na ata play part yake hadi gari ifanyiwe inspection.

Gari ikipita kwenye inspection watatuma report na watahitaji uhakiki contacts zako (physical address) ambayo baadae gari ikishapakiwa kwenye meli wataitumia kukutumia Bill of Landing, Original Export Certificate, Insurance coverage letter na zawadi yako). Kupitia cap page yako utajua gari inaletwa na meli gani na inatarajia kuondoka tarehe ngapi na kufika tarehe ngapi.

Muda wa kufika meli unatofautiana kulingana na kampuni. Mfano kampuni ya Hoegh Brasilia brake ya kwanza ikifika Africa ni Durban, Maputo, Dar es salaam kisha Mombasa na kwa wastani huchukua siku 29 kufika Dar. Ambazo zinakuja Dar mojakwa moja huwahi kufika. Unawezaku track meli kwakutumia marine vessel ttaffic na utajua ilipo na hii itakusaidia kujipanga. Kama kuna lolote uliza mkuu.

13d6effc69fc9cb53a4f03fad8ba0c42.jpg
 
[QUOTE="JMF, enyewe unasave sana kwani nanunua gari kwa mil 13.5 (gharama zote mpaka naliweka mkononi, CIF & gharama za hapa Tanzania) ambapo ningelikuta yadi nahisi ningepigwa hata mil 20!

Thanks JF! Asante pia JMF
 
1.Gari huchukua takribani miezi miwili na katika webpage unayopewa inaonesha siku gari itaondoka na siku ya kufika na haizidi siku mbili kwa tarehe walokueleza na inaweza kuwa pungufu.

2. Nakushauri uwe na pesa yako kwa malipo ya kodi na pia uwe na kama milioni moja kwa extra charges za bandali bima nk. Kuna kamchezo wanacheza hao ma agent ka kuchelewesha mchakato ili gari ichelewe bandarini na kama si mzoefu unajikuta unaingia katika kulipia storage fee maana watakucheleweshea mpaka grace period itapita, hii ni bongo mambo ya 10% si ajabu.

3. Gari unaweza kuamua kulipia ikaguliwe na utapata cheti kwa mtandao kikionesha uzima wa gari na kama inakubalika kwa viwango vya Tanzania. Jitahidi usiwape nafasi ya kukaa na gari yako ikishafika. Niliamua kutumia agent wa beforward ili ikitokea fyoko nijue nani nakomaa nae si unajua mambo ya "sisi tumepokea hivi mara vile" so nakushauri ukomae na hao hao maana kuna mchezo wa kuchomoa vitu kama redio nk. Ubora wa kutumia agent tofauti ni katika kupata unafuu wa bei na kuepuka kucheleweshwa kwa makusudi ili watu wale %
 
Justine Marack, Thank you kaka! Hata mie mpango wangu ni kutumia be forward wenyewe ofisi ya Dar ili waweze kushughulikia mapema issue hii! Wameshaniambia fee yao pia ambayo niliona ni reasonable!
 
Nataja kununua Suzuki Escudo ya 2001 nimewasiliana na SBT Japan wameniambia 16ml.vp wadau hawa jamaa wako safi? Pia nishaurini ni gari ya kazi kwa road zetu bongo?
Hawa jamaa wapo vizuri sana me nilichukua gari kwao halina hata miezi 2 but usiwatumie wale wa pale NHC watakupunguzia dollar 100 watumie SBT wa Japan utapata kwa bei nzuri sana
 
Wadau naomba ushauri wenu, nahitaji kununua kati ya IST toleo la 2005 au WISH ya 2007 ni ipi inafaa zaidi kwa TZ?

Pia nataka ninunue kupitia tradecarview japo nipo Japan kwa miezi minne zaidi lkn sina uhakika na yard zao pia lugha ni tatizo wengi hawajui kiingreza. Naomba uzoefu wenu.
 
Wadau naomba ushauri wenu, nahitaji kununua kati ya IST toleo la 2005 au WISH ya 2007 ni ipi inafaa zaidi kwa Tanzania?

Pia nataka ninunue kupitia tradecarview japo nipo Japan kwa miezi minne zaidi lkn sina uhakika na yard zao pia lugha ni tatizo wengi hawajui kiingreza. Naomba uzoefu wenu.
Chukua WISH kwa kuwa haitachajiwa uchakavu sana maana ni ndani ya miaka 10 pia tafuta kampuni ya beforward ni nzuri ukiweza tumia BFS 178357 utapata punguzo zaida na utafurahia hiyo gari kwa bei ya discount
 
Back
Top Bottom