Ushauri unahitajika haraka

Zneba

Senior Member
May 12, 2010
192
7
Habari zenu wana jf,kuna rafiki yangu wa karibu sana amepata tatizo hili hapa na anaomba mumsaidie ushauri.naomba ambae hayuko serious asichangie kabisa.

Rafiki yangu ana boyfriend ambae wanapendana sana tu, tatizo hawa watu kwanza wana dini tofauti mwanaume ni mkristo na msichana ni muslim shida imekuja mwanaume amewambia ndugu zake kuwa anataka kumuoa huyo binti kwa ndoa ya bomani ndugu wamekataa kabisa wanataka amuoe msichana wake wa mwanzo ambae ni mkristo km yy, ila jamaa anasema huyo msichana hakuwa anampenda tangu mwanzo ila ndo ndugu wanamtaka huyo.

Na tatizo lingine alilogundua huyu rafiki yangu jamaa amepunguza mawasiliano nae wala hamtembeli tena akidai emechanganyikiwa hajui nini cha kufanya. Sasa bint anauliza, VIPI AAMUE YY KUMUACHA JAMAA TU MANA ANAMUONA KAMA HANA MSIMAMO COZ HATA KAMA KUNA HILO TATIZO KWA NINI ABADILIKE?

MSHAURINI AU ASUBIRI TU MANA JAMAA AMEMUAMBIA ANAENDA KUONGEA NA NDUGU ZAKE KAMA WATARIDHIKA JUU YA HILO.
 
ni rafiki yangu kweli coz ningejitaja hakuna shida coz hakuna anayenijua.
 
Kama matatizo yameanza wakiwa bado hawajaingia kwenye ndoa na wakijaingia itakua je? Kilichopo asifikirie kwa sasa tu wafikirie na baadae itakua je wakiwa kwenye ndoa afu achukue uamuzi thabiti ambao hataujutia baadae
 
ila ndugu ndo huwa issue au nifafanulie hapo ulimakafu
 
Kama matatizo yameanza wakiwa bado hawajaingia kwenye ndoa na wakijaingia itakua je? Kilichopo asifikirie kwa sasa tu wafikirie na baadae itakua je wakiwa kwenye ndoa afu achukue uamuzi thabiti ambao hataujutia baadae

anayetakiwa kufikiria zaidi hapa ni nani mwanmke au mwanaume sijakupata vizur
 
Rafiki yangu ana boyfriend ambae wanapendana sana tu,tatizo hawa watu kwanza wana dini tofauti mwanaume ni mkristo na msichana ni muslim shida imekuja mwanaume amewambia ndugu zake kuwa anataka kumuoa huyo binti kwa ndoa ya bomani ndugu wamekataa kabisa wanataka amuoe msichana wake wa mwanzo ambae ni mkristo km yy ila jamaa anasema huyo msichana hakuwa anampenda tangu mwanzo ila ndo ndugu wanamtaka huyo.na tatizo lingine alilogundua huyu rafiki yangu jamaa amepunguza mawasiliano nae wala hamtembeli tena akidai emechanganyikiwa hajui nini cha kufanya.sasa bint anauliza.VIPI AAMUE YY KUMUACHA JAMAA TU MANA ANAMUONA KAMA HANA MSIMAMO COZ HATA KAMA KUNA HILO TATIZO KWANINI ABADILIKE?MSHAURINI AU ASUBIRI TU MANA JAMAA AMEMUAMBIA ANAENDA KUONGEA NA NDUGU ZAKE KAMA WATARIDHIKA JUU YA HILO.

Mabadiliko yanasababishwa na mengi ... inawezekana yeye rafikiyo anaona mabadiliko ya mwenzake kuliko ya kwake ...kwanza katika kipindi hiki ambapo kuna mgogoro huyo rafikiyo anatakiwa awe na mwenzi wake karibu sana na anatakiwa amshauri au washauriane nini kinatakiwa na kwa wakati gani, pia ni vyema wakawekana wazi kikwazi kiko kwa nani hasa sidhani kama ndugu wote ni kikwazo .

Je upande wa rafiki yako wanaridhia juu ya huyo bwana maana nimeona iko upande mmoja tu. na kwa nini afikiria kumwacha jamaa ilihali ndo safari inataka kuanza ??? je wao wamekubaliana kusimama kwa dini gani baaada ya ndoa??? watoto watafuata dini ya nani???
 
kwa upande wangu mm ninaona hata iwe vipi tatzo litabaki pale pale mana hata ndugu ya jamaa wakikubali bado ndoa yao itaendelea kuwa na tatzo kwny upande wa dini hvyo basi nivizur mmoja wapo akakubali kuingia kwny din nyngne kuliko ndoa kuwa vuguvugu na kama itashndikana nivizur kila mmoja achukuwe taimu yake mana wakiwa kwny ndoa matatzo yatakuwa makubwa mara nne ya sasa na hvyo jamaa anaongozwa na ndugu na kuwasikiriza ajiadhar sana huyo rafiki yako
 
mabadiliko yanasababishwa na mengi ... inawezekana yeye rafikiyo anaona mabadiliko ya mwenzake kuliko ya kwake ...kwanza katika kipindi hiki ambapo kuna mgogoro huyo rafikiyo anatakiwa awe na mwenzi wake karibu sana na anatakiwa amshauri au washauriane nini kinatakiwa na kwa wakati gani, pia ni vyema wakawekana wazi kikwazi kiko kwa nani hasa sidhani kama ndugu wote ni kikwazo . je upande wa rafiki yako wanaridhia juu ya huyo bwana maana nimeona iko upande mmoja tu. na kwa nini afikiria kumwacha jamaa ilihali ndo safari inataka kuanza ??? je wao wamekubaliana kusimama kwa dini gani baaada ya ndoa??? watoto watafuata dini ya nani???

aliyebadilika siyo rafiki yangu ni mwanaume ndo amebadilika baada yakuwaeleza ndugu zake,na mwanamke hana tatizo yko tayari kumpa sapoti yoyote kwa kipindi hiki na upo sahihi kabisa ila anashangaa jamaa amebadilika kwenye hiki kipindi cha matatizo,kuhusu upande wa mwanamke bado hawajaeleza wazazi wake akasikia wanasemaje ila baadhi ya ngugu zake aliwaeleza na hawana tatizo na hiyo imani na kuhusu watoto wataifata imani ya baba hilo lilikuwa lipo wazi na pia halikuwa na shida kihivyo.anafikiria kumuacha coz anahisi jamaa km ana fikiria hivyo kwanini sasa abadilike
 
kwa upande wangu mm ninaona hata iwe vipi tatzo litabaki pale pale mana hata ndugu ya jamaa wakikubali bado ndoa yao itaendelea kuwa na tatzo kwny upande wa dini hvyo basi nivizur mmoja wapo akakubali kuingia kwny din nyngne kuliko ndoa kuwa vuguvugu na kama itashndikana nivizur kila mmoja achukuwe taimu yake mana wakiwa kwny ndoa matatzo yatakuwa makubwa mara nne ya sasa na hvyo jamaa anaongozwa na ndugu na kuwasikiriza ajiadhar sana huyo rafiki yako

Hilo nalo neno na yy alichogundua ni jamaa anawasikiliza sana ndugu zake ndo mana amepata hofu juu ya muendelo wa uhusiano huu
 
aliyebadilika siyo rafiki yangu ni mwanaume ndo amebadilika baada yakuwaeleza ndugu zake,na mwanamke hana tatizo yko tayari kumpa sapoti yoyote kwa kipindi hiki na upo sahihi kabisa ila anashangaa jamaa amebadilika kwenye hiki kipindi cha matatizo,kuhusu upande wa mwanamke bado hawajaeleza wazazi wake akasikia wanasemaje ila baadhi ya ngugu zake aliwaeleza na hawana tatizo na hiyo imani na kuhusu watoto wataifata imani ya baba hilo lilikuwa lipo wazi na pia halikuwa na shida kihivyo.anafikiria kumuacha coz anahisi jamaa km ana fikiria hivyo kwanini sasa abadilike

tatizo rafikiyo alipoambiwa kwamba ndugu wa mwanaume hawataki ni lazima ilimshtua na ameshajenga uoga ... unasema kabadilika mwanaume kwa vile umesikiliza upande mmoja .. kaa na rafiki yako umwambia awe karibu na jama asisubiri hadi jamaa amtembelee
 
…tatizo hawa watu kwanza wana dini tofauti mwanaume ni mkristo na msichana ni muslim.

Mapenzi ya kweli hayana dini, kabila, rangi, sura, mali wala umri… Dini siyo issue!

mwanaume amewambia ndugu zake kuwa anataka kumuoa huyo binti kwa ndoa ya bomani ndugu wamekataa kabisa wanataka amuoe msichana wake wa mwanzo ambae ni mkristo km yy, ila jamaa anasema huyo msichana hakuwa anampenda tangu mwanzo ila ndo ndugu wanamtaka huyo. .

Huwezi kuomba kibali cha kumwoa yule unayempenda ila unaweza kutoa taarifa kwa ndugu; jamaa; marafiki. Kumbuka hakuna demokrasia kwenye maisha ya watu wanaopendana. Maisha ni ya wawili. Mwanaume ameonyesha kutojiamini na ni dalili mbaya za maisha ya baadaye. Nyumba inaweza kutawaliwa na ukoo mzima..

Na tatizo lingine alilogundua huyu rafiki yangu jamaa amepunguza mawasiliano nae wala hamtembeli tena akidai emechanganyikiwa hajui nini cha kufanya..

Kwa nini achanganyikiwe badala ya kumshukuru Mungu kwa kumkwepesha na bomu? Huyo jamaa yake wanafaa kwa kufanya mazoezi ya mapenzi tu lakini HAFAI kwa jukumu la kumpa moyo na maisha yake.

..Sasa bint anauliza, VIPI AAMUE YY KUMUACHA JAMAA TU MANA ANAMUONA KAMA HANA MSIMAMO COZ HATA KAMA KUNA HILO TATIZO KWA NINI ABADILIKE?

Kumbe jibu zuri la suluhu analo..Kama alikuwa anataka support hapa JF..mwambie yuko sahihi kupiga chini huyo jamaa.. Hamna kitu hapo!
 
yani tulizo asante kwa ushauri wako ameupata hata mi kwa mtazamo wangu nimeona jamaa atamsumbua huko mbele familia nzima itatoa maamuzi kama hapo tu ameshindwa kutoa maamuzi na kubadilika juu ni wazi kabisa mbleni ni hatari kubwa,thanx
 
Habari zenu wana jf,kuna rafiki yangu wa karibu sana amepata tatizo hili hapa na anaomba mumsaidie ushauri.naomba ambae hayuko serious asichangie kabisa.

Rafiki yangu ana boyfriend ambae wanapendana sana tu, tatizo hawa watu kwanza wana dini tofauti mwanaume ni mkristo na msichana ni muslim shida imekuja mwanaume amewambia ndugu zake kuwa anataka kumuoa huyo binti kwa ndoa ya bomani ndugu wamekataa kabisa wanataka amuoe msichana wake wa mwanzo ambae ni mkristo km yy, ila jamaa anasema huyo msichana hakuwa anampenda tangu mwanzo ila ndo ndugu wanamtaka huyo.

Na tatizo lingine alilogundua huyu rafiki yangu jamaa amepunguza mawasiliano nae wala hamtembeli tena akidai emechanganyikiwa hajui nini cha kufanya. Sasa bint anauliza, VIPI AAMUE YY KUMUACHA JAMAA TU MANA ANAMUONA KAMA HANA MSIMAMO COZ HATA KAMA KUNA HILO TATIZO KWA NINI ABADILIKE?

MSHAURINI AU ASUBIRI TU MANA JAMAA AMEMUAMBIA ANAENDA KUONGEA NA NDUGU ZAKE KAMA WATARIDHIKA JUU YA HILO.

Asilimia zaidi ya 50% ya ahadi wanazopeana wapenzi ni za uongo. Nadiriki kusema kuwa huyu rafiki yako kadanganywa...

Kinachoonekana hapa huyu jamaa alikuwa na huyu dada ki-mapenzi zaidi lakini linapokuja suala la kuoa, inabidi awe siriaz, na ndicha anachofanya. Kusema kuwa ndugu wanamkataa, hata mimi ndicho ningesema kama nataka kumuacha mtu ambaye sina sababu ya kueleweka kwake. Indication kubwa ya uongo huo ni huyo jamaa kupunguza mawasiliano kwa kisingizio eti 'amechanganyikiwa'.... Naamini huyo dada atakuwa na umri mdogo au uzoefu mdogo sana katika mapenz, otherwise angeshamshtukia jamaa.

Kwa hiyo huyo dada ajue tu kuwa kama ataendelea kuwa na huyo jamaa, kikomo chao ni jamaa atapooa mtu wa dini yake, ama kwa sababu ya dini au kwa sababu anampenda huyo mwingine zaidi, maana pia inawezekana hampendi tena huyo rafiki yako, anatafuta kisingizio. Zipo threads kadhaa humu za namna ambavyo watu wana-act pale wapenzi wao wa dini tofauti wanapokataliwa na ndugu. Zipitie, utaona kuwa anavyofanya shem wako, sivyo ianvyokuwaga real, hapa natafuta kisingizio tu...
 
Habari zenu wana jf,kuna rafiki yangu wa karibu sana amepata tatizo hili hapa na anaomba mumsaidie ushauri.naomba ambae hayuko serious asichangie kabisa.

Rafiki yangu ana boyfriend ambae wanapendana sana tu, tatizo hawa watu kwanza wana dini tofauti mwanaume ni mkristo na msichana ni muslim shida imekuja mwanaume amewambia ndugu zake kuwa anataka kumuoa huyo binti kwa ndoa ya bomani ndugu wamekataa kabisa wanataka amuoe msichana wake wa mwanzo ambae ni mkristo km yy, ila jamaa anasema huyo msichana hakuwa anampenda tangu mwanzo ila ndo ndugu wanamtaka huyo.

Na tatizo lingine alilogundua huyu rafiki yangu jamaa amepunguza mawasiliano nae wala hamtembeli tena akidai emechanganyikiwa hajui nini cha kufanya. Sasa bint anauliza, VIPI AAMUE YY KUMUACHA JAMAA TU MANA ANAMUONA KAMA HANA MSIMAMO COZ HATA KAMA KUNA HILO TATIZO KWA NINI ABADILIKE?

MSHAURINI AU ASUBIRI TU MANA JAMAA AMEMUAMBIA ANAENDA KUONGEA NA NDUGU ZAKE KAMA WATARIDHIKA JUU YA HILO.

Mwambie aingie huku tumshauri yeye moja kwa moja...!
 
kama huyo jamaa yako hayo serious we mteme tu bhana, atakuja kuwa kikwazo bureee, inaonekana hawezi maisha, ie He cant afford challenges in life.
 
Temana tu, maana hata mkioana familia yenu hasa watoto watayumba sana, mtaishi kwa kuogopana badala ya kuheshimiana. Fikirieni mbali zaidi na nyayo zenu. Usiwasikilize wanaokudanganya kwamba dini haina nafasi ktk ndoa, Maadili Mazuri ya dini ktk Familia ndiyo yanayoongoza nyumba.
 
Wazee wa ukoo walikuwa wasiwasi na ndugu yetu kuoa dini ingine, lakini jamaa aliendelea na msimamo wake,ajabu ile umekuwandoa ya mfano kwa kila familia, wanaishi kwa amani na upendo karibu kuliko wote wanandoa wa lika lao kwenye ukoo, kwa hiyo kama huyo jamaa atakubali hili limshike wala hakufai achana nae tu kabla hujaumia moyo
 
Back
Top Bottom