Ushauri unahitajika haraka sana

Jana rafiki yangu kanipigia simu kuniomba ushauri kuhusu kutokuelewana na mkewe wa ndoa kuhusu simu ya mkononi,jamaa ni mfanyakazi mwajiriwa na mama nimfanya biashara na biashara yenyewe ni jamaa mwenyewe katoa mtaji,sasa anasema usiku wa jumamosi kuamkia jana jumapili mkewe aliingia bafuni yeye akawa yupo kitandani, akachukua simu ya mkewe na kuanza kusoma sms,mama alipo toka bafuni akakuta mzee anasoma sms,mkewe akamuuliza mbona unapenda sana kupekua simu yangu?jamaa naye akamuuliza kwani niipekua kuna shida gani?asema mkewe alikuja juu na kumuonya siku akikuta ameshika simu yake tena na anaipekua ataivunja hiyo simu,sasa jamaa ndo kaja kwangu kuniomba ushauri yeye anasema kweli mke wake ni mwaminifu tena kama mwanzo?hakuna lililojificha ndani hapo?hivyo kabla sijampa ushauri nikaona ni vema na mimi niwashirikishe,hiki kisa ni cha kweli kabisa hivyo ushauri uwe wa kweli ni watu wapo ndani ya ndoa kwa miaka kumi sasa,asanteni

mmh huyo rafiki yako naye?kwa nini apekue wakati mkewe akiwa mbali?hapo mwanamke huenda kapata hasira kwa sababu jamaa kaonyesha kutomuamini or huenda hawana utaratibu wakupekuliana simu. Ila kwa upande mwingine kama mwanamke kahamaki sanaa huenda kuna kitu hapoooo..hizi simu jamani zina mambo, tusipokuwa makini nazo hata hizo ndoa zitavunjika nyingi.
 
Vigezo na masharti kuzingatiwa.....huu msemo una maana kubwa sana
 
asanteni sana kwa ushauri na hata wale waliotukana nashukuru ni wakilisha ushauri kama ulivyo
 
Ukweli jamani uaminifu ni kitu cha thamani sana ktk ndoa na uhusiano wowote ule. Haiwezekana huyu mama aone simu yake kuangaliwa na mumewe ni kupekuliwa kama haina wadudu, na je huyo mama hashiki simu ya mume wake? Au ndo maisha yao? Yawezekana huyo baba kafanya kinyume na makubaliano yao. Nimewahi kusikia familia moja ya watu wazima kabisa wote wamestaafu lakini hakuna mtu anaeshika simu ya mwingine.
 
Back
Top Bottom