Ushauri:uhakiki wa vyeti vya watumishi wote

Mpigaji

JF-Expert Member
Feb 6, 2011
384
42
Kuna watu wengi ambao ni waajiriwa katika sekta binafsi na taasisi za umma ambao hawana sifa stahiki katika ajira walizonazo kwa kuwa walitengeneza vyeti feki ili kujipatia ajira hizo.Ushauri wangu waajiri wote wakusanye vyeti vya watumishi wao na kuvipeleka Baraza la Mitihani na katika vyuo husika ili vihakikiwe uhalali wake!
Naomba kuwasilisha!
 
Haiwezekani hili zoezi...HAIWEZEKANI
tatizo hili ni kubwa sana haswa serikalini
kwenye majeshi yetu yote, halmashauri
zote,mashirika ya uma na binafsi, waalimu, ma-dr, na hata wahadhiri...
mbaya zaidi hata Mawaziri & wabunge
tunapenda kuwaita vigogo...wengi wameingia
kazini kwa vyeti vya ndugu zao au vya kughushi
(Rejea kitabu cha Msemakweli-Mafisadi wa Elimu).
Sheria imewapa mamlaka baraza la mitihani
kufanya uhakiki wa vyeti popote wanapohisi kuna walakini
Lakini walipojaribu kufanya hivyo walitishwa wakakaripiwa
waache mara moja kwani zoezi hilo lingeigharimu sana
serikali ambayo imefilisika...Hata hivyo labda zoezi la vitambulisho
vya utaifa litaibua upya mambo hayo kwani watumishi hutakiwa kusajili
cheti cha form iv hivyo kompyuta itagundua cheti kimoja kinatumiwa
na zaidi ya mtu mmoja...
Ila kihalisia HAIWEZEKANI HADI PALE WANASIASA WATAKAPOKUWA WAAMINIFU...
 
Kumbe inawezekana pale kila mmoja atakapokuwa muaminifu!
 
Hili nizoezi gumu kupitishwa kuliko lile la kubadili chama tawala
 
Kumbe inawezekana pale kila mmoja atakapokuwa muaminifu!

Narudia tena MKUU mpiganaji, HAIWEZEKANI kila mtu akawa mwaminifu
Vinginevyo neno uaminifu litakosa maana yake halisi....
Ni watu wachache humu wanatumia majina yao halisi kama mimi na Kigwangala
Kama kila mmoja angekuwa mwaminifu isingekuwepo haja ya kuficha majina humu
Ili neno Uaminifu libaki na maana yake haiwezekani kila mmoja akawa mwaminifu
Ndiyo maana nasema zoezi hilo haliwezekani, hivi sasa natafuta cheti nami niwe
daktari maana inavyolekea watapata mshahara mkubwa sana hivi karibuni...baada ya
kugomea hali ya kutokuwepo na uaminifu kwa wanasiasa...nami pia nakosa uaminifu...
Ndiyo maana narudia kusema HAIWEZEKANI kupata kila mtu mwaminifu
zoezi la kuhakiki vyeti haliwekani kwa vile "the beautiful ones are not yet born"
 
Utawagusa wengi hasa walimu na mapolisi ndo noma wanafoji vyeti balaa with evidence....................i humbly submit
 
Hivi mnazungumzia serikali gani ndugu zangu?? hahahhahahahaaa kama umefuatilia ajira za walimu hivi karibu utagundua kuwa bado hatuna system inayoeleweka. Kama wizara moja inaweza kutoa ajira mara mbili kwa mtu mmoja what do u expect?? Hapa namaanisha kuwa mtu ni mwalimu ameajiriwa na alipwa mshahara kama mwl. wa Sekondari halafu kaenda shule baada ya kumaliza degree ameomba kazi upya for the sake ya kulamba zile hela za kujikimu, the same wizara inamuajiri huyu mtu na anapangiwa kufundisha sekondari nyingine tofauti na ile ya kwanza. Mtu anaenda anaripoti anavuta mkwanja halafu anarudi shule yake ya zamani anaripoti kuwa amemaliza shule anaendelea na kazi Bongo ni nchi ya hovyo more than u think
 
inamaana wanapoajiriwa hawahakikiwi?

Vyeti havihakikiwi na mamlaka husika!Kinachotakiwa kufanyika mara baada ya kupata admission au ajira vyeti husika kwa mfano vya sekondari vipelekwe NECTA vihakikiwe majina pamoja grades zilizopo!Mfano mzuri NECTA huhakiki taarifa za watahiniwa wa Diploma za ualimu,na hubaini Vilaza wengi ambao huondolewa katika watahiniwa tarajali!Ni jambo linalowezekana kabisa kama itaamuliwa hivyo!Halmashauri ya Jiji la Tanga ilifanya uhakiki wa watumishi wake mwaka jana ambapo kila mtumishi aliyeajiriwa alipeleka particulars zake!Wale ambao hawakujitokeza wakafuta katika PAY ROLLS!Sasa itolewe ORDER kuwa watumishi wote wapeleke vyeti vyao ili vihakikiwe!Kuna watu watakimbia vituo vyao vya kazi!
 
Kuna watu wengi ambao ni waajiriwa katika sekta binafsi na taasisi za umma ambao hawana sifa stahiki katika ajira walizonazo kwa kuwa walitengeneza vyeti feki ili kujipatia ajira hizo.Ushauri wangu waajiri wote wakusanye vyeti vya watumishi wao na kuvipeleka Baraza la Mitihani na katika vyuo husika ili vihakikiwe uhalali wake!
Naomba kuwasilisha!
kijana unatafuta kurogwa?endelea na hizi kelele zako utakuja kunikumbuka...!
 
Back
Top Bottom