Ushauri toka kwa ceo wa foundation of civil society

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
12,013
10,170
Nikiwa naangalia kipindi cha uchumi kupitia ITV kuna kauli ilitolewa na CEO wa Foundation of civil Society kiukweli ilinifurahisha aliposema uchumi unapokuwa kama nchi hakuna utawala bora maana yake wananchi wataendelea kubaki katika umaskini kwa kuwa kunakuwa hakuna uwazi kuhusu matumizi ya serikali kwani mahali popote palipo na uwazi hakuna uchafu au maovu hivyo kama kiongozi akifanya kosa ama ataondolewa au ataondoka mwenyewe. Kiukweli nimeitafakari kauli hii nikaona ina mantinki maana kwa mwananchi wa kawaida mara nyingi amekuwa akilalamika kuhusu hali ngumu japokuwa wanasiasa wanatuambia uchumi umekuwa kumbe fedha zote hizo ndi zile ambazo wananunulia mashangingi na matumizi mengine yasiyo ya lazima kama kutaka kuajiri wasaidizi wanne kwa kila mbunge pamoja na kujenga ofisi kila jimbo (nadhani hapa inaweza kuwa ni mfano wa kile jamaa alichokuwa anachangia)
 
Back
Top Bottom