Ushauri Tafadhali

What is the other option? Unataka akubali bila kujua kwa hakika kama ni wake au sio. Binti kamaliza darasa la 7, akimchukua na kuanza kumtunza atatumia gharama kiasi gani mpaka aanze kujitegemea au kuolewa?

Halafu hakutakuwa na mahusiano mazuri kama mzee ana shaka na uzazi wa huyo mtoto. Ana sababu za kuwa na mashaka, DNA is the best option. Hata kama ni 5mil, jipige uende.

hapo sawa nimekusoma mkuu
 
Unataka kunichekesha mie, yaani kipimo kionyeshe mtoto ni wako halafu ushindwe kuukubali ukweli, utafurahi siku ukikuta huyo binti anajiuza barabarani coz maisha yamekuwa magumu kwake

Nashukuru kwa ushauri wako. Lakini vipi kuhusu muda uliopita mpaka sasa. Hata kama DNA ikionesha kweli ni wangu, nahisi itaniwia vigumu sana kuupokea huo ukweli.
 
Waungwana naomba mnisaidie mawazo kwenye hili.

Nina mke na watoto watatu, na tunamshukuru Mungu maisha yanakwenda vizuri.

Kuna binti niliwahi kuwa naye siku za nyuma wakati niko sekondari. Tulikuwa tukionana wakati narudi likizo huko kijijini kwetu. Baadae ule uhusiano haukuendelea baada ya yeye na wazazi wake kuhamia mkoa mwingine ambako nasikia baadae aliolewa. Hii ni kama miaka 17 iliyopita. Pale kijijini walibaki dada zake na ndugu wachache.

Mimi niliendelea na maisha yangu wakati huo sekondari na kisha chuo na sasa nina shughuli zangu binafsi.

Hivi karibuni nimepata simu kutoka kijijini kwetu kwamba kuna binti mdogo mtoto wa wa yule msichana wa zamani amekuja kwa ndugu zake pale kijijini na kudai kwamba ameambiwa na mama yake kwamba mimi ndiyo baba yake mzazi. Huyo binti amemaliza darasa la saba huko kwa mama yake.

Habari hii imenishangaza sana hasa ukizingatia kwamba wakati uhusiano wetu unakwisha miaka hiyo ya 1995 hakuwahi kuniambia kwamba alikuwa mjamzito. Na hata kipindi chote hicho hajawi kuwasiliana na mimi kwa chochote wala ndugu zake waliobaki kijini hawakuwahi kuniambia chochote mimi au ndugu zangu licha ya kuwa huwa narudi kijijini mara nyingi.

Napata wakati mgumu sana juu ya hili hasa ukizingatia kwamba sasa hivi nina familia yangu. Ningependa hili swal liishe kabla halijaleta mchafuko wowote kwenye ndoa yangu.

Naomba ushauri wenu please.

Wewe msomi mbona unapata tabu. Fanya taratibu wasiliana na mama yake nendeni mahakamani kupata kibali (not case) ili muwahi kwa mkemia mkuu wa serikali. Una uwezo lipia DNA yako subiri majibu ni mwisho wa kila kitu. But wakati unafanya hayo weka wazi kwa mke wako black and white. Hili tatizo dogo sana kwa mke understanding maana mtoto kama atakuwa wa kwako atakuwa alipatikana wakati ambao hamjaoana na hukuwa na taarifa naye ndiyo maana hukumwambia wakati wa uchumba. Full stop.
 
Asante sana. Nitafanyia kazi ushauri wako.
 
Unataka kunichekesha mie, yaani kipimo kionyeshe mtoto ni wako halafu ushindwe kuukubali ukweli, utafurahi siku ukikuta huyo binti anajiuza barabarani coz maisha yamekuwa magumu kwake

Asante kwa ushauri. Lakini unazungumziaje kuhusu ukimya wa mama mtu kwa kipindi chote hicho cha takribani miaka 17?
 
huyo mtoto atakuwa wako, huyo mdada alifanya siri hakutaka watu wajue kwamba ulimpa mimba, ila mtoto amekuwa na kuanza kukumsumbua anataka baba yake hakuwa na jinsi imebidi amuonyeshe baba yake. Angekuwa ni muongo angekuongopea mapema ili apate matumizi ya mtoto, lakini kalea mimba, kalea mtoto mpaka amekua
 
Back
Top Bottom