Ushauri: Rafiki yangu amekataliwa kwa mama mkwe

Habari wana JF,

Rafiki yangu amekataliwa kwa mama mkwe alivyopelekwa kutambulishwa eti kisa ana kithembe, mbaya zaidi ni kwamba huyo mwanaume alikuwa nae katika mahusiano kwa miaka minne sasa

Kwakweli anahitaji ushauri na maombi yenu, maana hayuko sawa kabisa.

Ushauri wenu ni kitu cha muhimu kwa sasa.
Mwaka 2009 niliwahi kukataliwa na mama mkwe, probably kwa kuwa kipindi kile sikuwa vizuri sana kiafya na kimuonekano nilikuwa nimekondeana... Since then binti yake hajawahi kuolewa mpaka leo hii yupo ana randa randa na anakaribia miaka 30!
 
Mwaka 2009 niliwahi kukataliwa na mama mkwe, probably kwa kuwa kipindi kile sikuwa vizuri sana kiafya na kimuonekano nilikuwa nimekondeana... Since then binti yake hajawahi kuolewa mpaka leo hii yupo ana randa randa na anakaribia miaka 30!

Dah polee sana au walifikiria unaumwa?
 
Mmh huyo mama ana lake jambo, sidhan kama hyo ni sababu kabisa ya kumkataa mtu...kwa mwendo huu wenye vithembe kazi tunayo
 
May be kuna sababu nyingne yenye mashiko zaid ya hyo aliyoambiwa nadhan hyo imetumika kumask vitu vngne nyuma ya pazia namshauri huyo dada ajaribu kukaa na huyo mchumba wke wazungumze kwa kirefu atayajua mengne zaid ya hilo
 
Hivi kwani mpaka sasa hivi kuna watu wanachaguliwa myu wa kuoa na wazazi wao?

Ina maana huyo mzazi atakulisha wewe na mkeo hadi akuchagulie mke.
Nawashukuru sana wazazi wangu.
Walichofanya kutupa sisi ni Elimu tu basi. Mengine mtu utayajua mwenyewe ukubwani
 
Story yako imenikumbusha 2014nilipelekwa kutambulishwa mama mkwe akanikataa kisa namichiriz ya mikono na kijana wake akashikilia mama alichosema tukaachana.

nililia nilijilaumu nilipaka madawa ya kutoa michiriz lakin mwisho wa yote nilikumbuka furaha yangu ipo kwa Mungu kwa wakati wake atanipa Mume aliye mwema ambaye hataona kasorozangu na kutumia kama siraha ya kunipigia.

namshukuru Mungu mwaka huu unaisha niko kwenye ndoa na mume wangu karidhika na kila nilicho nacho.
Mwambie asife moyo tegemeo lake aweke kwa Bwana.maana mtume paul anasema furaha ya bwana ni udhaifu wangu,ili apate kujitukuza
 
Ni simpo sana kujua kweli, wafuatilie tu hao watu ndani ya siku moja utajua ukweli. hawa ni watu wenye kuuma na kupuliza kaa mbali. kama nawe ni mmoja wapo anza kujichunguza hususan stori na maneno unayowalisha watu wako wa karibu.
wenye kithembe ni watu wa kutoa siri za ndani pia.
Hizo ni dhana ambazo hazina mantiki kabisa. Huo ni ulemavu wa aina fulani na unatibika kwa kutumia voice therapy utotoni.
 
shukuru umempata asie kisiran kuna wamama ni ishu kwa watoto wao kuoa nna rafiki angu ana 40 hajaoa kisa maza sasa hapo ni baraka gan unata au unapata?mwingine mpk alioa kisiri mama anamkuta mkwe home akapiga kimya.et hatak mwanae aoe kisa hatamsaidia kweli hapo utasubiri baraka?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom