Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

That is to say if you are a man you must be either of the two, and you cant be both

Drink or F*
Naah!
ukiwa cha-pombe utaishia kupiga mshindo mmoja na kulala!..utaishia kuzaa watoto wa kike.....!

wasiokunywa wanasifiwa sana na lediiz
 
Makanyagio,

Ndugu yangu, Dawa ni moja tu nayo ni YESU

Aokoke kwa kumchagua Yesu kuwa Mungu na Bwana na Mwokozi wa Maisha yake.

Yesu ameponya walevi wengi.

Kwa Yesu yote yanawezekana.
 
  • Thanks
Reactions: THT
Pombe ni kitu ambacho hakikubaliki kabisa kwa baadhi ya madhehebu ya dini, na wanaotumia huwa wanajifichaficha, pombe ni bidhaa ambayo ikikukolea kuacha ni tabu kweli kweli.

Sikiliza hii. Bibie mmoja alikuwa akikasirishwa na tabia ya mumewe kulewa tena kila siku, kila anapomsihi aache pombe ilikuwa ni ugomvi mkubwa, siku moja alimuomba atakaporudi arudi na kitoweo cha nyama kwani tangu Christmas ya mwaka uliopita hawajawahi kula nyama tena hapo nyumbani, jamaa aliafiki kwani yeye huwa akila akiwa baa.
Kabla ya kurudi jamaa alipitia butcher na kununua nyama lakini alionelea apitie baa japo apate moja mbili. Waliendelea kunywa na rafiki zake huku akimuomba mchoma mishikaki akate japo kidogo ile nyama ya kupeleka nyumbani, waliendelea kidogo kidogo mpaka yote ikaisha.

Saa za kurudi jamaa alirudi akiwa chakali, na mkewe alimfungulia na kwa bahati mbaya jamaa alitapika sebuleni, na vipande vya nyama vilionekana dhahiri. Mkewe hakutaka shari akamkokota mpaka chumbani akamlaza vizuri na kumfunika. Jamaa akachapa usingizi. Mkewe akarudi kupiga deki matapishi na kuokota vipande vyote vya nyama na kuvihifadhi kwenye bakuli.

Asubuhi mkewe aliamka mapema na kusonga ugali nakuandaa meza likiwemo bakuli la nyama aliyoitapika jamaa usiku akafunika vizuri kwa KAWA. Jamaa alipoamka na kuoga alikaribishwa mezani, hamadi! alipofunua bakuli alikumbana na nyama yenye harufu ya matapishi ya kilevi akapandisha hasira na kufoka '' umepata wapi nyama hii?'' Mkewe kwa kujiamini na sauti ya upendo akajibu ''Ulituletea jana mume wangu, mimi na watoto tulishakula ya kwetu usiku''
Jamaa alifedheheka sana, na akaamua toka siku hiyo pombe basi na kila akipata pesa mboga nzuri ikiwemo nyama ililiwa nyumbani kwake sio mpaka siku ya Christmas. Wana JF leteni mikasa iliyosababisha watu fulani kuacha kabisa pombe. Ijumaa njema na wikiendi njema.
 
Jamaa mmoja alikuwa ni mshindaa baa mpaka asubuhi ! Sasa ikatokea kaenda kwa wakwe kijijini siyo mbali sana na mjini anapoishi! Basi baada ya kuwajulia hali na vijizawadi vya hapa na pale akaaga kurudi mjini kwa mkewe na watoto! Wakwe kwa ukarimu wakampatia jogoo ili watoto wakinjoi minofu yake! Kwakuwa ilikuwa ni wikiendi, jamaa alipofika mjini kama kawa wakawasiliana na washikaji zake na kupanga pa kukutana ili kutuanga masanga kisawasawa! Basi wakakutana kwenye baa waliyoizoea wakaanza kutwanga pombe na yule jogoo wakamuweka chini ya meza! Mjamaa ikapiga pombe na kusahau kama kuna jogoo anatakiwa kufikishwa nyumbani ... saa 2 usiku 3,4,5...8,9...10 alfajiri.....mara jogoo likawika chini ya meza kokolikooooooooooooo....! Jamaa walizinduka na kutimuka mbio wakizani ni wanga wameingia! Kufika home huku akihema kagonga hodi kwa nguvu na kufunguliwa ...mkewe kwa upole kamuuliza vp mbona umechelewa sana na yule jogoo wazazi waliyekupa umlete yuko wapi... Jamaa ndiyo akili ikamrudi kuwa aliyewika ni wake na si Mwanga ....ila sijui kama aliacha pombe
 
Pombe huwa inaachwa kwa sababuza kiafya (mpaka daktari aseme) au uchafu utakaokutana nao kwenye pombe.............

kuna jamaa alikuwa anagombana na mkewe kila kukicha kwa sababu y apombe za kienyezi maarufu kama mataputapu. Bi mkubwa alichofanya ni kuongea na mama muuza amletee pombe nyumbani. Bi mkubwa kaitunza ile pombe mpaka siku ya pili jamaa alikuwa nyumbani akapewa ile pombe. Jamaa akawa anakunywa tar-tiiiibu. Ile kufika mwisho si akakutana na vitoto vitogo viwili vya panya........ Jamaa kwa kichefuchefu alichokuwa nacho alitapika sana na mwisho akaamua kuacha pombe maana kila akisogeza pombe mdomoni, ile picha ya vitoto vya panya visivyo na manyoya inamjia na hapo hapo anaanza kutapi.
 
Pombe huwa inaachwa kwa sababuza kiafya (mpaka daktari aseme) au uchafu utakaokutana nao kwenye pombe.............

kuna jamaa alikuwa anagombana na mkewe kila kukicha kwa sababu y apombe za kienyezi maarufu kama mataputapu. Bi mkubwa alichofanya ni kuongea na mama muuza amletee pombe nyumbani. Bi mkubwa kaitunza ile pombe mpaka siku ya pili jamaa alikuwa nyumbani akapewa ile pombe. Jamaa akawa anakunywa tar-tiiiibu. Ile kufika mwisho si akakutana na vitoto vitogo viwili vya panya........ Jamaa kwa kichefuchefu alichokuwa nacho alitapika sana na mwisho akaamua kuacha pombe maana kila akisogeza pombe mdomoni, ile picha ya vitoto vya panya visivyo na manyoya inamjia na hapo hapo anaanza kutapi.

Mmmmmh! Hii hata mimi ningeacha pombe!
 
Hata kama ni wewe ile kufikiri tu unakula vipanya ukisogelea tu kichefuchefu, lazima uache...
 
Basi wakakutana kwenye baa waliyoizoea wakaanza kutwanga pombe na yule jogoo wakamuweka chini ya meza! Mjamaa ikapiga pombe na kusahau kama kuna jogoo anatakiwa kufikishwa nyumbani ... saa 2 usiku 3,4,5...8,9...10 alfajiri.....mara jogoo likawika chini ya meza kokolikooooooooooooo....! sijui kama aliacha pombe?

Aliacha huyo.
 
Kwa kawaida simba hali binadamu mpaka aonje japo mara moja hapo ataendelea, Jamaa mmoja alipokuwa anarudi kilabuni akakutana na mnyama huku akifikiri ni mbwa, kwa sauti ya kilevi akamfokea ''we, kijimbwa koko nta-ntafuta ni-niniii saa izi'' kumbe alikuwa simba, aligundua kesho yake asubuhi alipokuta dume lake kubwa la ngombe halipo zizini na michirizi ya damu kuelekea porini na baada ya msako walimkurupusha simba akila ng'ombe wake si mbali sana na nyumbani, akawaungurumia wakakimbia naye akapotelea porini, kwa kunusurika huko jamaa hajanywa pombe tena mpaka leo.
 
Bibi yangu mzaa mama alikuwa mlevi sana wa pombe, yaani ni lazima anywe kila siku tena zile pombe za watu wa songea plus ulanzi.

Watoto wake walikaa na kupanga jinsi ya kumfanya mama yao aache pombe, kwani kila siku anapokunywa anatukana hovyo na kuleta tabia mbaya mbaya mbele ya wajukuu na wao pia. wakamvisia siku moja akiwa amelewa sanaaaa, (kijijini) wakachukua kinye** cha mtoto mdogo na kumuwekea kwenye nguo zake ili aonekane yeye ndio amejiny*a kisha wakambeba na kumlaza nje.

Asubuhi alipoamka aliona aibu sana kwamba analewa hadi anajisaidia na kulala nje. Toka siku hiyo akaacha pombe yeye mwenyewe bila kuambiwa, na sasa hivi pamoja na ukongwe wake alionao walau ana afya kuliko angeendelea kunywa sijui kama mimi ningelimuona hadi leo.
 
Sasa hicho kitendo mbele za Mungu si dhambi kubwa,yaani kumfanya bibi yenu adhani amejinyea kumbe sio,hata hivyo ilikuwa dawa poa sana.
 
Hii yangu ni ya kweli kabisa.

Kaka mmoja alikuwa mlevi kupindukia. Alibahatika kuchumbia mwanamke ambaye wanatoka kijiji kimoja huko moshi marangu ila yeye anakaa mjini. Mwezi mmoja kabla ya harusi yake akiwa huko marangu kama kawaida yake akatoka kwenda kunywa. Akalewa sana na bahati mbaya mvua kubwa ikaanza kunyesha so ikabidi ajikongoje kwenda nyumbani. Hakufika mbali akaanguka kwenye matope chini ya mgomba akawa anajikongoja kuamka ila anashidwa maana amelewa sana. Bahati mbaya wakwe zake watarajiwa wakapita wakamuona wakamuokota na kumkokota mpaka nyumbani kwao (kwa wakwe), kesho yake asubuhi anaamka nyumba tofauti amechafuka matope wakwe wanamtolea macho... Je hivi ndivyo utaenda kututesea mtoto wetu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom