Ushauri: Nimechoka na hii hali ya kuachwa na wanaume

Ushauri wangu mimi husiogope kuanzisha uhusiano mpya heti kwa sababu uliumizwa uko mwanzo, ila angalizo langu na hapa ndipo unapokosea, husitoe kipochi manyoya mpaka ndoa, mwanaume mwenyenia na wewe hatojali sharti ilo, kama ukisema utulie bila uhusiano, hakuna siku itatokea ukaonyeshwa huyu hapa, ni lazima uwe na uhusiano ndipo upate mume, husiogope maana uoga ni adui mkubwa, ila husitoe kipochi, yangu ni hayo.
 
pole sana mkuu, kuna kitabu kimoja cha mchungaji kenneth onyeme kitakusaidia, ni pm nikutumie baadhi ya maombi, ukisali kwa imani utafanikiwa maisha ni kusaidiana ni pm nikusaidie
Kipi THT au cha Vitu 35 ambavyo kila mwanamke lazima afanye ili aweze kumtunza mumewe amkinge na wanawake wengine cha 2005?
 
Mtindi lapa, k bandari ya salama. Ndo vitu vikuu viwili vinavyowaachisha wanawake. Wanaume tunavutiwa na umbo la nje sana, mtoto mtindi boost kijungu mashalla ukikivalia tight camel toe kwa mbali. But after a deep into it. Gosh! Unatambua gear shift ratio sio ile uliyodhania, unaacha.
ndivyo mawazo yako yanayo waza?
 
Namshukuru Mungu nimeifuatilia thread hii tangia mwanzo, naona tatizo. Tatizo ni binti yangu mwenyewe. Mimi ni Social Worker, nadhani anahitaji ushauri nasaha. Unaona ukim provoke analipuka. Fuatilia thread unaiona. Anahitaji ushauri wa kitaalamu, bila hivyo itakuwa shida kufikia adhima yake. Afuatilie washauri kama hawa wapo, watamsaidia.
 
Kuna dada mmoja aliwahi kusema kuwa ni kosa kubwa kwa mwanamke kutikisa kiberiti kwani hatari yake ni kuwa njiti zaweza kumwagika. Kosa la kwanza nililoliona hapo ni kuwa ulimdanganya yule bwana aliyekuwa nje kimasomo kuwa una mimba yake kumbe si kweli, na inawezekana alikulikuwa anajua hakukuwa na mazingira ya wewe kupata ujauzito; na reaction yake kuwa kubwa, na pengine hata yeye hajakuambia mpaka leo kwa nini ali-react vile; kwa mtazamo wangu alijua ule ujauzito sio wake au na yeye alikuwa anaku-test (hivyo hii ndio kutikisa kiberiti mpaka unamwaga njiti).

Kingine usijaribu kusema tena uongo hata siku moja; sasa kama unamtegemea Mungu halafu unavunja amri yake ya nane; je hapo imekaaje? Kitu kingine naona kama una majibu ya mkato kwani Nyani Ngabu amekujaribu hapo na wewe umempa jibu la mkato na kama hasira juu yake (hicho kilikuwa ni kipimo cha uvumilivu, na inaonekana ni mtu wa kulipiza).

Halafu watu hawafungi ndoa kwa sababu wengine wanafunga ndoa. Kitu kingine achana na majaribio, na usiwe na mahusiano nje ya uchumba - na muda wa uchumba uwe kati ya miezi sita na miaka miwili.

Mwisho tafuta test za psychology kwa wataalamu wa psychologia ili uweze kufahamu vizuri personality yako; na haya mambo hayana formula ingawaje ni vizuri kusikiliza experience za wengine.

Rai yangu: ukitaka kununua gari lililotumika ukaona linavuja oil lazima utatia shaka, lakini ukiona halivuji oil utanunua ila baadae likianza kuvuja oil hautalikimbia bali utalifanyia ukarabati.
 
Habari zenu,

Naombeni ushauri wenu ili niepuke na hii hali,

Kama mtu atashindwa kunishauri naomba aache maana sipendi kutukanwa.

Mimi ni binti ni mkazi wa Dar ila kikabila nimetokea mkoa uliopo karibu na Kanda za Ziwa, na mshukuru Mungu kaniumba msichana wa kawaida sina uzuri kama malaika wala sina ubaya ni wakawaida tu, nimepitia maisha ya mahusiano yenye kuniumiza sana, mara ya kwanza nilikuwa na mvulana ambaye ni msukuma wa Shinyanga kipindi nimeanza mahusiano yeye alikuwa chuo nikamvumilia sana mpaka akamaliza chuo.

Mungu akamsaidia akapata kazi katika ofisi moja kubwa tu hapa Dar alikuwa ni mwanasheria, nilijitahidi niwe mwaminifu nikijua atakuwa mume wangu lakini alikuwa ni mtu muongo na kunidanganya sana, nikaja kugundua kumbe aliacha mchumba wake kwao na alikuwa na watoto wawili niliumia sana nikapiga moyo konde nikaanza maisha mapya.

Badae nilipata mtu mwingine alikuwa ni mfanyakazi wa kampuni moja ya simu kubwa tu hapa Tz huyo kijani alikuwa ni mchagga na mshukuru Mungu katika swala la kunijali alinijali sana yeye alikuwa anasali haya makanisa ya kilokole mimi ninasali Lutheran, kweli tulipendana sana ikafika muda wa kunipeleka kwao ila mama yake mzazi alitokea kunichukia ghafla, hivyo sikuona sababu ya kuendelea nae huku mama yake hanipendi na nikamwambia bora tuachane kuliko kukosa baraka kwa wazazi wako kisa mimi, japo niliumia sana nikamuomba Mungu anipe ujasiri, siku zikaenda nikasahau nikajipa moyo ipo siku.

Baadae nikampata mwanaume mwingine ambaye nilidumu naye zaidi ya miaka minne, kwakweli namshukuru Mungu amenipa moyo wa uvumilivu na sina tabia ya uhuni au tamaa za muda mfupi huyu alikuwa ni msukuma tena wa Mwanza na kiukweli alikuwa kijana mwenye hofu na Mungu sikutegemea kama angenibadilikia baadae, alikuwa anafanya kazi kwenye mgodi mkubwa wa Tz na ndugu zake wengi walikuwa Mwanza hivyo Dar alikuwa anaishi na kaka yake tu hivyo hakuwa mwenyeji sana huku na kama ikitokea kaja Dar likizo basi alikuwa anakuja kwajili yangu, katika kipindi cha mahusiano alipata nafasi ofisini ya kwenda kusoma nje na mawasiliano yetu yalikuwa ni mazuri ilikuwa kila siku lazima anitafute alijitahidi kuniweka karibu nae na kila siku ilikuwa neno lake nitulie akirudi atanioa kwakweli katika hali ya kibinadamu ilihitaji moyo sana lakini nilimshirikisha Mungu kwa kila hatua ili nisiingiwe na tamaa, japo ndugu zangu wengi waliniambia nikipata mtu mwenye nia ya kunioa nisikatae maana hawana uhakika nae lakini nilijitahidi kutowasikiliza.

Badae mawasiliano yalianza kupungua nina weza kumtafuta akawa yupo online anapata SMS lakini hajibu anaweza kujibu SMS badaa ya mwezi ukimuuliza anasema masomo magumu mama, mara naachaga data wazi, nilikuwa naumia sana ila nika note kitu, akapata likizo akarudi wakati namfuata airport nilipomuona nilihisi kabadilika sana, nikajipa moyo labda kutokana na mazingira aliyokutana nayo, likizo ilipoisha aliondoka nikasema ngoja nipime imani yake nikamtumia text kuwa nina mimba sikutegemea, alikuwa mkali chui akani please nitoe mimba sababu siwezi kulea ikiwa baba yake yupo mbali akaniambia usipotoa nakuacha.

Kwakweli niliumia sana nikawaza je ingekuwa ni kweli nina mimba ningekuwa na hali gani, nilichomjibu nikamwambia sawa nitafanya abortion ila usinitafute, badaa ya kama miezi kadhaa alirudi akanitafuta na kuni please turudiane nilikataa nikaamua kuacha nitulize akili na mpaka leo kwenye akili yake anajua nilikuwa na mimba kumbe haikuwa hivyo, katika hali ya kibinadamu nilikaa single karibu mwaka nikapata mvulana huyu amenipita miaka 4 na yeye ni msukuma wa Shinyanga na ni mfanyakazi wa serikalini nilijiona ni mwenye bahati na kikubwa niliona familia yao ni watu wenye hofu na Mungu.

Tulipendana sana na alinijali sana, lakini mwaka huu mwezi wa 4 ndo ilikuwa mwisho wa mahusiano yetu baada ya kunipeleka kwao kunitambulisha ili mwezi wa saba tufunge ndoa, baada ya utambulisho mimi nilirudi Dar sababu mwenzangu kwao ni Dodoma, nilipoondoka kumbe huku nyuma kulikuwa na mtafaruku kati yake na wazazi na kanisa, ni kwamba walikuwa hawataki kijana wao aoe mwanamke anayetoka nje ya kanisa la kilokole, hivyo alianza kubadilika mwenzangu akawa ananiambia ndoa tuhairishe hadi nimalize kujenga nyumba, bla bla zilikuwa nyingi ila nilijua kuna sababu kubwa hataki kuniambia, mwisho wa siku ilibidi aniweke wazi niliumia sana na sikuwaza hata siku moja kama wakristo tuna weza kubaguana kiasi hiki.

Tangu hapo nimekuwa mtu mwenye mawazo mengi, maumivu makali kuna wakati huwa naweza jifungia ndani nalia sana, na pia nimekuwa mtu mwenye hasira kila wakati japo najitahidi ku control hasira, kingine nimekuwa sitamanani mwanaume yoyote yule yani naweza nikaanza mawasiliano na mtu baada ya wiki nampotezea, kubwa nimekuwa na hofu na hawa watu na kikubwa roho ya kupendwa na waume za watu inaniandama na mimi sitaki kabisa kuja kufanya chukizo kwa Mungu ku date na mume wa mtu, wamekuwa wananisumbua sana yani mtu yupo radhi anipe kila ninachokitaka ili mradi anipate, dunia sahivi ina maradhi mengi na mimi sipo tayari nizikwe kwa tamaa, pia nimekuwa muoga na kabila la wasukuma maana ndo nina bahati nao mbaya.

Je nifanye nini ili hii hali isiwepo tena kwenye maisha yangu maana nimechoka kucheza harusi za wenzangu, na mimi natamani siku moja waje wacheze yangu, japo huko kwetu bibi zangu wanasemaga kuna mizimu ya babu zetu inatuandama ndo maana wajukuu tunakuwa hatufanikiwi kwenye malengo tunatakiwa tukafanyiwe matambiko, japo mimi binafsi siamini katika hilo maana namtegemea Mungu.

Naombeni ushauri wenu katika hili, nisameheni kama nitawachosha kwa thread ndefu.

Note: Matusi sitaki.
Nenda kwa bibi
 
Angalia hii list pengine itakusaidia, kuna tabia nyingine ambazo ukiwa nazo Kwa kweli utakuwa unaachika tu:

- kuonyesha utegemezi sana Kwa mwanaume.
- lawama na kulalamika.
- kuharakisha steps, like kutaka ndoa mapema
- ku react Vitu vidogo
- background
- kujirahisisha
 
Tofauti inaonekana katika imani if possible na ww kuwa mlokole tu sawa na mumeo kama unaamini katika ukristo pia utawafanya wazazi waone mko pamoja na isilete taabu
 
Back
Top Bottom