Ushauri: Nimebeba ujauzito wakati mshono wa mimba ya kwanza haujapona vizuri

Pole sana. kamuone daktari. Kamuone daktari haraka iwezekanavyo. Ila usijaribu kutoa maana ni laana na ni mauaji kwa mtoto asiye na hatia. Daktari anaweza kukushauri kupata muda wa kutosha kupumzika na kukufanyia upasuaji mtoto akishakomaa tumboni. Ila baada ya hapo ongeza uangalifu lisijirudie tena. Pole na Hongera sana.
asante mamafive
 
asante kwa ushauri, sijawai kujichubua, sema mimi ni mnene
Ooh ndio mana sema inamafuta,miaka mitatu wala sio tatizo utabeba salama tu,utajifungua salama ,mtoto ananafasi yakutosha kukua,pungiza kulakula vitu vya mafuta,jitahidi kujishugulisha ili mwili uwe na nguvu kidogo,fata utaratibu wa daktari,pole mpenzi
 
We, kamuone daktari haraka saana tu. Hakuna daktari mwenye akili timamu atukanaye wagonjwa. Hizo ni hisia potofu. Tena usiende kwa mwingine, daktari wako anaujua udhaifu wako hivyo atajua la kufanya. Waweza kuamriwa hata kukaa karibu na hospitali kwa maangalizi zaidi ili upone
 
asante
 
Ooh ndio mana sema inamafuta,miaka mitatu wala sio tatizo utabeba salama tu,utajifungua salama ,mtoto ananafasi yakutosha kukua,pungiza kulakula vitu vya mafuta,jitahidi kujishugulisha ili mwili uwe na nguvu kidogo,fata utaratibu wa daktari,pole mpenzi
asante kwa ushauri, ubarikiwe
 
Kama utaenda BMC unaweza muona Dr Rumanyika, Dr Bumodoka, Dr Mahendeka au Dr Ng'walida

Kama una noti nyingi muone Dr Kilonzo pale Mwanza Hospital mtaa wa Uhuru

Wapo wengi sana wanaoweza kukusaidia

Ujauzito ni baraka usihofu utapata ushauri na maelekezo. Nadhani tunaokushauri huu sio muda wa kukushambulia, itakuwa ni kukuongezea athari. Wengine wanafikiria kuplant wawe na watoto!
wilaya nyamagana, mkoa mwanza
 
Mkuu mbona hayo majina uliyotaja kama ni ya kufikirika.
Any way hongera kwa hicho kitambi naona kila siku glass haitoki mkononi.
 
Kama utaenda BMC unaweza muona Dr Rumanyika, Dr Bumodoka, Dr Mahendeka au Dr Ng'walida

Kama una noti nyingi muone Dr Kilonzo pale Mwanza Hospital mtaa wa Uhuru

Wapo wengi sana wanaoweza kukusaidia

Ujauzito ni baraka usihofu utapata ushauri na maelekezo. Nadhani tunaokushauri huu sio muda wa kukushambulia, itakuwa ni kukuongezea athari. Wengine wanafikiria kuplant wawe na watoto!
asante ndugu
 
asante ubarikiwe. ukiwa hujapatwa na tatizo mtu unaweza kukomenti chochote maana hufeel chochote, lakini kumbuka muda mwingine tunakumbana na vitu ambavyo hatuvitaki na kuvipenda kwa wakati huo, lakini vinatupata bila ridhaa yetu! asante lakn
Kwahiyo mimba imeingia bila ridhaa yako Dunia? Kitendo cha kuamua na kukubali kufanya mapenzi pasipo na njia za kujikinga na ujauzito wakati uliahaonywa hiyo ni ridhaa tosha. Labda useme ulifanya mapenzi pasipo ridhaa yako, hapo sawa.
Hapo abortion haiepukiki dada Dunia.
 
Rudi kwa daktari japo asilimia 90 utaambiwa utoe maana kwa ajili ya afya yako hakuna sheria itakayoweza kukushtaki.
Pole sana, siku nyingine uwe makini, uwe unatumia vidonge vya uzazi wa mpango au ufunge uzazi mpaka hiyo miaka ifike.
Au siku nyingine ukifanya sex na ukaona haukuwa safe na hauna kinga yoyote uliyoitumia ili usipate mimba basi tafuta vidonge viitwavyo 'The Morning after pills' jina lingine ni plan B.

KUMBUKA KUZUIA USIPATE MIMBA NI HERI KULIKO KUTOA.
 
Daktari anaanzaje kukutukana kwa mfano bi shostito eeh!!?...nenda ukamuone kama ni professional yake hawezi kukutukana,.kutukanwa na uhai wako heri ni nini!??
Sipendi nikupoteze atii.....
 
Mwachie Mungu kama ni mimba ya haki atakupigania, usije ukajaribu kuitoa au ukapokea ushauri wa namna hiyo...zaidi nakuombea

Kitabibu ni tatizo kubwa sana.. maana lazima igharimu maisha ya mama au mtoto sasa tusimpe mawazo ya kufariji wakati uhalisia wake ni hatari.
 
Daktari anaanzaje kukutukana kwa mfano bi shostito eeh!!?...nenda ukamuone kama ni professional yake hawezi kukutukana,.kutukanwa na uhai wako heri ni nini!??
Sipendi nikupoteze atii.....
asante shost
 
Back
Top Bottom