Biashara ya Stationery: Ushauri, Vifaa, Gharama na Mbinu za Uendeshaji

Smarter

JF-Expert Member
Nov 10, 2008
527
110
stationery-03.jpg


Awali ya yote Napenda Kushukuru na Kupongeza Jukwaa kwa Mawazo Elekezi.

Naomba nielimishwe/nijulishwe juu ya Biashara ya Stationaries kwa ujumla, (Uuzaji wa Tonner, Karatasi, madaftari, peni, Office equipments, Photocopies) nakadhalika.

Natamani kusikia kwa mtu anaefanya hii biashara, Mzigo unatoka wapi?, secrets behind business, na Mtaji wa kiasi gani unaweza kuanza nao kwa kufungua Stationary,

inawezakana niko too general stilll bt in anutshell I hope mtanisaidia Wandugu.

WADAU WENGINE WANAOHITAJI KUJIFUNZA KUHUSU BIASHARA HII
Vitu gani vinatakiwa kuzingatiwa unavyofungua ofisi ya stationery?

Naomba ufafanuzi wa faida, hasara na changamoto zake kwa ujumla.
Naomba ushauri ndugu zangu ya kufungua biashara ya stationary mkoa wa songea je inalipa jaman tafadhali sana niambie kabla sijapoteza haka kapesa kangu kamkopo.
Habari za siku mingi wanaJf ni muda sasa sikuwa naposti wala kukoment ila mara mojamoja nilikuwa napita kama msomaji hii ni kutokana na majukumu.

Nilibahatika kupata ajila taasisi moja hivi ila pia ni mjasiriamali ambaye nimewekeza kwenye stationery mbili kubwa tu ila imefika muda napenda kuongeza ubunifu.

Nimevutiwa na biashara ya kuprint covers za simu (smartphones) ambapo nimekua nikiona baadhi ya watu wameprint picha zao kwenye covers za simu zao lakini nikiwauliza wengi husema waliprint Nairobi sasa nahitaji kujua ni mashine ipi na ina bei gani pia material zake na upatikanaji wake pia.

Naamini humu hawakosi wataalamu wa idara hiyo please tupeane mautundu si unajua tena mwanamke kujishughulisha.!
Habari wanajamii, naomba kufahamishwa in deep nataka kuanza biashara ya stationery kwa mtaji wa Tsh. miloni 1 kwa Dar es Salaam.

Je, mtaji unatosha kuanza?

Sent using Jamii Forums mobile app
Salam, naomba ushauri wana JF. Nina biashara ya stationery ila nataka nijiongeze kwa kuuza rim paper e.g mond kutoka south afrika kwa jumla na rejareja.

Msaada 1. Ni wapi zinajumliwa hapo dares salaam au mpaka niagize nje.

2. Nikitaka niuze kwa jumla, nikienda kwa wafanya biashara wakubwa wataniuzia kuanzia idadi gani na kwa shilingi ngapi. Kwa sababu za kuuza rejareja huwa nauziwa tsh 7200/- kwa moja.

Nipo Lushoto, Tanga. Samahani kama kiswahili changu kitakuwa siyo kizuri ila namaanisha karatasi za kuandikia A4.
Habarini wadau,

Naomba kwa mwenye ufahamu juu ya vifaa mbalimbali vya stationery na bei zake tafadhali anisaidie. Nina eneo tayari na mtaji wa milioni mbili kwa kuanzia.

Asanteni


MAJIBU KUTOKA KWA WADAU KUHUSU BIASHARA HII
NI BIASHARA NZURI, ZINGATIA ENEO

Biashara hii ni nzuri sana ila inabidi kuangalia location kama chuo, kanisa au shule ili mambo yaende vizuri.
Kwenye upande wa huduma utapata wateja wa photocopy, printing, passport size na scanning. Pia inabidi uwe mbunifu mfano nyaraka ambazo kupata inamchukua mtu muda mrefu unakua nazo ofisini kwako. Unaweza kuwa na copy ya fomu ya NIDA, fomu ya maombi ya TIN (TRA) na huduma ya kuprint onlipe copy ya kitambulisho cha NIDA zote hizi zitaongeza kipato.

Kwa upande wa bidhaa weka bidhaa kama daftari, kalamu, notebook, riboni za kupambia, vifaa vingine vya mapambo, gundi, na vifaa vya shule vingi. Ukiwa na connection, uchangamfu na uchapakazi utauza sana.

Ongeza huduma kama Mpesa, Airtel, luku na malipo mengine. Hakikisha mtu unayemweka ana ujuzi na biashara hii vinginevyo utapoteza wateja (nmewahi kuifanya biashara hii).

Kama mtaji wako ni mdogo, fanya yale mambo ambayo unaweza kumudu vizuri usipende kubeba mambo mengi kuliko mtaji.

Hakikisha una computer, printer 3 in 1, photocopier (nashauri Canon) kama unaweza chukua na Camera kwa passport.
FANYA UTAFITI WA ENEO
Photocopy nzuri ni Canon Image Runner 2525 bei 1.5mil, zinapatika Kariakoo. Angalizo: kabla ya kufungua biashara ya stationery fanya utafiti wa eneo la biashara kwanza vinginevyo utaifunga au kugeuza banda la Miamala na Vocha tu.
KUWA NA MTAALAMU PINDI UNUNUAPO MASHINE ZA PHOTOCOPY
Hongera kwa wazo zuri kwanza tuanze maandalIzI tahadhari kipindi hiki shule, mavyuo na taasisi zingine za elimu zimefunga na ndio wateja wazuri wa hii biashara.

1: Tafuta eneo zuri ambalo lipo karibu na chuo na hostel za wanachuo.

Mgawanyiko wa pesa: Chukua mashine used ya photocopy haitazidi laki 4 na elfu 50 (ushauri usinunue bila kwenda nacho mtu wako mwenye ujuzi kidogo na mashine za photocopy maana zinashida nyingi sana)

Kuna umuhimu wa kununua Desktop kwa 350000 haitazidi laki 4.

pia printer mashine nzuri kuna member hapo juu amesema ir 2025 kwa haitazidi laki 3 mara ya mwisho ilikuwa 260000

Katika issue ya pango I reccommend ungechonga banda lako la chuma la kueleweka au kununua used (nimeona wengi Dodoma wanatumia hili) hii itaepusha cost kubwa ya kulipia pango, all the best mkuu pia uwe na bei ya kirafiki na uwezo wa kuderiver kazi hata baada ya masaa 3 utakubalika zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
ANGALIA MTAJI WAKO
Safi sn mkuu. Kwa ushauri wng mimi, milioni mbili ni ndogo sn, na inategemea ni aina gani ya stationery unataka kuanzisha.

Nasema hivyo kwa sababu, photocopier nzuri ya kisasa, ambayo ni used, ni zaidi ya hiyo milioni 2. Hapo bdo hujanunua computer na printer za rangi. Printer black & white unaweza ukatumia hyo hyo photocopier.

Hzo ni components tu ambazo ni vitendea kazi vya haraka haraka, bado hujanunua mzigo. Ni ngumu kuweka bei za mzigo kwani zinatofautiana gharama za upatikanaji wke, na inategemea upo wapi.

Kwa mikoani kuna gharama za usafirishaji kumbuka. Ungekuwa na kama mil 8 hv, ungekuwa pazuri sn.

Sent from my iPad using JamiiForums app
TAFUTA MBINU BORA YA USHINDANI. KUWA MBUNIFU
Nimetaja competition sababu as you know wewe ndio unajua ubavu wako, je una nguvu kiasi gani ? na je unaouwezo wa kutoa good quality at a low price kulinganisha na wenzako? kwahiyo cha kufanya ni kwa haraka kuangalia bei za wenzako na kuona kama you can do better than them au kama wenyewe na bado ukatoa bei kama yao au chini ya kwao. Kuhusu Tshirts je itakuwa screen printing au Heat transfer, au vyote. Kuhusu ID hapa mara nyingi utategemea Tenders kwahiyo hata kama unayo ofisi lakini inabidi uingie mitaani au wilayani kutafuta tender, pens, teacups and plates hapa unaweza ukapata maharusi kuweka picha zao kwenye sahani etc au ukaongea na kampuni zikakupa matangazo yao ili uyaweke kwenye hizo pen

I hope kwa niliyosema hapo juu umegundua kwamba biashara yako haitegemei sana window shopping kwamba mtu hajui anachotaka katika pitapita zake alafu anaona kitu na kusema haa nakitaka hicho, which means utahitaji kufanya marketing and promotion na wateja wengine unaweza ukawa unawapata kwa kuwafuata maofisini kwao na kuwaonyesha sample (mfano printing kwenye pens) au ukipeleka sample ya printed sahani kwenye mikutano ya harusi, au tshirt printing ukiwatengenezea watu vizuri kwenye misiba au sherehe zao. IDs kazi ikiwa nzuri watu watakujua through word of mouth, na pia unaweza ukapeleka sample zako kwenye secretarial services ambapo utawapa comission kama wakikupatia mauzo.

Conclusively Choice between Dar and Mwanza depends na umahili wako and how big you want to be (can you fight with the big boys?, although you dont have to be big unaweza ukawa Dar lakini bado ukawa unatoa hizi huduma utapata tu, customer base) au Mwanza ambapo competition sio kali kama Dar kwahiyo ukiweza kuoffer better quality at a lower price then its fine..., lakini the best scenario unaweza ukawa Dar alafu Mwanza ukawa una agents (watu wenye secretarial services) ukiongea nao ili wawe wanachukua orders na wewe unafanya kazi dar unawatumia alafu unawapa commission.

Kuhusu kupata mtu anayefanya hii biashara akuambia watu ni wachoyo kukwambia, the only way to find out ni wewe kujifanya mteja ili uende from different suppliers na uulizie bei zao na uangalie quality ya kazi zao alafu ufanye comparison na kazi yako. Kumbuka kama nilivyosema usiogope kuanza, start small utajifunza kwa makosa, na hata kama hauna mashine zote still unaweza ukachukua kazi ukafanya kwa watu wenye mashine, Nimeona umesema unazo heavy duty machines, how heavy is heavy, sababu kama una desktop printer ya kawaida inabidi ujue if it can handle mitikisiko ya kazi isije ikawa ni printer moja alafu katikati ya kazi inaalibika. Kuhusu Glass and Plates hivi ni rahisi sana kuviuza sababu maharusi watapenda wawe na ukumbusho and its something unique, kuhusu pens kama quality ni nzuri every company is potential customer unaweza ukaweka majina ya kampuni kwenye hizo pens, kampuni nyingi zitakupa tender.....
NI BIASHARA NZURI, ENEO RAFIKI NI MUHIMU
Biashara ya stationery ni nzuri japo inategemea location (yaani mahali ilipo). Ukifanikiwa kuweka stationery karibu na taasisi ya elimu yaani shule/chuo uwezekano wa kulipa kwa haraka ni mzuri. Hata hivyo kama zilivyo biashara zingine itategemea unapata mzigo kwa bei gani na wewe utauza/kutoa huduma kwa bei gani kwani stioneries ni nyingi na bei za bidhaa zinatofautiana toka duka moja kwenda lingine.

Binafsi nina stationery Arusha lakini ilinichukua muda kuanza kupata faida. Mtaji wangu ilikuwa karibia mil 10 ila ni kwa sababu mimi niliweka internet cafe, photocopy machine, printing, lamination, scanning, na uuzaji wa stationeries zenyewe. vifaa na stationeries nilichukulia/nachukulia Arusha, japo naanza kuangalia uwezekano wa kuona kama naweza kuwa nachukulia Dar kutegemea gharama za usafiri.

Ukipata location nzuri na bei zako zikawa reasonable uwezekano wa kufanikiwa kwenye biashara hii ni mkubwa.
ZIELEWE PRINTERS VIZURI HAPA
Nadhani hapa unaongelea printers inkjet na sio laser printers (kwa kufanyia printing za rangi n.k.) laser printer ni cheap kama unaprint black and white na kama unazo ir series basi unaweza ukaconnect copier yako ikawa printer (hivyo basi ukawa unafanya printing kwa bei ya photo copy)

Kama ni printing za rangi inkjet printers ni cheaper zaidi (running costs) issue ni kwamba catridges zake huwa ni bei mbaya sana hivyo inabidi ufanye refilling (na hapa issue sio kwamba printer ipi ni bora bali ni catridges zipi zinapatikana kwa urahisi hapo ulipo).., Printers inkjet ni bei ndogo sana kwa sasa kwahiyo hata ukichukua ya bei rahisi ikiharibika mara nyingi you dont need spares pesa yake inakuwa isharudi wewe unatupa na kuchukua mpya...

Watengeneza printers mara nyingi wanatengeneza na kuuza kwa bei ndogo ila faida yake wanapata kwenye mauzo ya catridges (just imagine kipindi fulani kulikuwa na inkjet printer ndogo kwa bei elfu 55 na ukinunua catridges mbili ya rangi na black ni elfu 55, hivyo basi ilikuwa bora kila wino ukiisha ununue printer mpya), kwahiyo utakuta ili hizi kampuni zisife inabidi ziendelee kuuza wino ndio maana hizi kampuni huwa zinatisha watu kwamba refilling inaua printers (lakini hizi ni propaganda tu)

Tukirudi kwenye swali lako hapa una option mbili, kununua printer kulinganisha na upatikani wa catridges zake hapo ulipo kwa bei nzuri na wino ukiisha unakuwa unajaza (refill kwa kutumia sindano)

Option ya pili printers either canon au Epson zina kitu third parties wanaunganisha wanakiita CISS (Continuous Ink Supply System) yaani kwenye hizi printer za epson na canon wanaunganisha mirija na mitungi mpaka kwenye catridges na wewe unachofanya inakuwa unajaza mitungi nje wino ukiisha badala ya kusumbuka na sindano... (ila hapa nakushauri zaidi kama utapata canon nzuri sababu epson kama isipofanya kazi kwa muda huwa zinaziba..) na hizi CISS sina uhakika kama Dar zipo ila Nairobi kuna watu wengi sana wanauza..., ila kama wewe ni mtu wa kuprint kazi chache nakushauri chukua tu cheapest printer available ambayo catridges zake sio bei mbaya alafu utakuwa unajaza kwa sindano

Dont forget for Black and White laser printer is Cheaper (jamaa yangu ana wino wa kurefill hizi catridges zake pia...) lakini kama unayo copier ir series na unatoa copies kufanya hii kama printer is even cheaper.

Lakini for prints za rangi tumia inkjet printers
TUNZA HESABU VYEMA. KILA SENTI NI MUHIMU

Mkuu kwanza nikupongeze kwa kutobweteka na kazi za kuajiliwa pekee. "You are on the right track" kuendelea kufanya kazi huku ukitafutafuta kipato cha nje.

Hati ya kimila kwenye baadhi ya benki inafanya kazi lakini hakikisha kijiji husika kimeshajiliwa. Kuhusu kiasi cha kuanzisha biashara hii, sina data lakini jaribu kupita pita kwenye maduka yanayouza mashine kama hizi upate bei. Pia usisahau kujaribu kuomba ushauri kwa wazoefu wa biashara hii ili wakwambie kipi kinafaa - e.g Printer gani nzuri, za kudumu lakini za bei poa. Wapi kuna mafundi wazuri wa kutengeneza mashine zikisumbua, etc.

Mbali na hilo nikuongezee ushauri wa bure tu:

1. Hakikisha hii biashara katika eneo unapoiweka kuna mzunguko mzuri zaidi wa biashara ya aina hii mfano karibu au ndani ya vyuo ni sehemu nzuri zaidi kuliko maeneo ya viwanda.

2. Tunza hesabu zako vema utakapokuwa umeanzisha biashara yako. Kila senti inahesabika. e.g kuuza karatasi moja au kutoa copy moja sh. 50 ni kidogo lakini ni kubwa pia maana (ndogo) x (idadi kubwa) x (muda) = Utajiri. Hivyo zingatia na kuheshimu kila mteja anayepiga hodi kwako, kila akiingia amini kuwa ni biashara mpya anakuongezea.

3. Zunguka (unguza sori) ukijalibu kunadi biashara yako na kueleza wazi kwa marafiki, mashule, maofisi, etc ili biashara yako ijulikane.

Kumbuka: Wakati kuna watu wengi sana wanatafuta mahali pa kuuza huduma na bidhaa zao, wapo watu wengi zaidi wasiojua pa kupata huduma au bidhaa hizo

Above all: Mtegemee Mungu katika kila kitu, inalipa.
USHAURI WA VIFAA NA UENDESHAJI
Ingawa wengi wanakushauri ununue hiki na kile na kile ila mimi nakushauri jaribu kupunguza overheads as much as possible yaani kwa kuanzia nunua hata vitu used wakati unajifunza na kuzoea kazi.

Computer
K
wa kazi za kawaida za kuchapa hauitaji computer ya kisasa hata zile za CRT na Pentium IV au chini ya hapo inafaa sana tena hata used, kwahio kwa hapa hata chini ya laki mbili unaweza ukapata.

Scanner
Ni bei rahisi ila hata kama hauna unaweza ukaanza kazi.

Photocopy
Hapa chukua used tena ukichukua IR series unaweza ukapata ambayo ina-print kwahio una-connect inakuwa inaprint hence bei ya printing inakuwa sawa sawa na photocopy ila nakushauri ununue pia laser printer sababu opc ya copy inaweza ikawa chafu kidogo mtu akakubali hio kama photocopy ila asikubali uki-print (quality yake ikawa sio kubwa)

Printer
Hapa angalia wateja wako kama unaprint sana kadi za harusi na rangi unahitaji inkjet printer (ambayo unaweza kununua epson yenye mitungi ya nje) au kama haufanyi printing kwa sana unaweza kununua hata hp tu ila catridge bei kubwa sana hivyo itabidi uwe unafanya refilling kwa sindano.. (kwa mwendo wa kununua catridge mpya huwezi ku-break even sababu hizi catridge ni bei ya juu sana kulinganisha na soko/bei wateja wanayotaka).

Kama una-print sana black and white ni muhimu kuwa na laser printer (nadhani hizi zinaanzia kwenye laki mbili au chini kidogo) tatizo la hizi catridge yake bei mbaya nadhani mtaani unaweza kuipata kwa kwenye elfu 70 mpaka laki na nusu.., ila dawa hapa kila wino ukiisha unafanya refilling na sio kununua mpya unaweza hata ukafanyiwa refilling kwa elfu 15.., na hii inaweza kutoa kama copies 2000.

Mengineyo
Sababu hii biashara imeshaanza kuwa saturated watu wengi wanafanya kwahio bei ni za chini sana usipokuwa mwangalifu au kujua undani wa biashara unaweza ukafunga baada ya muda mfupi, mafundi wanachakachua sana pindi vitu vikiharibika pia wafanyakazi wanaiba vile vile unaweza ukashaangaa matumizi yanazidi mapato, hivyo kuwa mwangalifu kufuatilia kazi (mfano mashine za ir series zina count hivyo unaweza ukajua ni copies ngapi zimetoka) as well as jifunze mashine ujue makosa madogo madogo sio kila mashine ikikwama unaita fundi (bei utapigwa kubwa as well as kuibiwa spare)

Subsidize na Vingine
Usitegemee dukani faida ya copy na kuchapa kazi peke yake (ukizingatia bei za copy zinaenda as low as tshs 30 na printing as low as 100 na kuchapa kazi hata chini ya 500/=) ongezea na vitu vingine kidogo kidogo mfano kuuza pen, madaftari, karatasi (ingawa faida yake ndogo sana), mmpesa (kama mzunguko ni poa hii inaweza kulipia hata chumba na mfanyakazi), luku, voucher n.k.
ANZA NA VIFAA VYA GHARAMA NAFUU VYENYE UBORA
Siongelei used kutoka bongo kwa photocopy sababu photocopy nyingi zinazotoka dubai na nje ni used, alafu kuna copier zinaweza zikawa mpya ila sababu sokoni hazijatumika sana haujui matatizo yake au spares zake sio nyingi.

Pili kuweka labda mtaji wa 1.5m au laki nane kuchukua PC mpya wakati ya Laki Mbili ingefanya kazi sioni kama ni kutumia rasilimali vizuri, bora hizo pesa zinazobaki ungeongezea kwenye mtaji mwingine wa vitu vidogo vidogo.

Labda kwa swali nikuulize unapanga utumia kama tshs ngapi kwa kununua vifaa? na huenda ukanunua vifaa kibao kwa kuanzia kabla haujajua soko la hapo, huenda ukachukua lamination machine ya bei mbaya kumbe pale wateja wengi ni wa binding au ukanunua epson yenye mitungi ya nje ku-print color kumbe hapo wateja wa printing rangi ni wachache na mashine kukaa bila kazi inapelekea kuziba.. (kumbe kwa kuanzia hata hp ya kawaida ingetosha)

Sababu kwa kazi ndogo ndogo kuchapa hauhitaji sijui icore 3 au nini ni basic PC inatosha, kwahio kama kuna uwezekano wa kuanzisha biashara kwa 2m kwa used alafu unajiongeza unavyokua ni vema kuliko kutumia 5m ambayo itakuchukua miaka ku-break even kitu ambacho huenda yule aliyeanza kwa 2m ataanza kupata faida mapema na kujiongeza.
VIFAA UNAVYOHITAJI NA BEI ZAKE
Printer Epson L850 (3 in 1)ni 1,100,000 bei inaweza kuwa chini au zaidi ya hapa kutegemea na mkoa uliopo
Epson L805 ni 875,000/= print only (heavy duty)

Epson l382 (3 in 1) matumizi ya kawaida 495,000-550,000/=

Ofisi nyingi wana L382 na L805 kuna ambao wana L850 pekee. L850 inasafisha picha kutoka kwenye memory card, pia inapata command kutoka kwenye PC. L805 inapata command kutoka kwenye PC na inaprint pekee. Ndiyo maana ukiwa na l805 inabidi uwe na l382 kwa ajili ya scanning na coloured copying

Canon IR 2320 inauzwa 2,350,000/= inapiga copy na kuprint

Laminanion A3 inauzwa 120,000/=

Paper cuter A3 inauza 34,000/= A4 17,000/=

Kuna mashine ya binding ingawa sikumbuki bei yake

Camera sijawahi kuwa nayo ila kutoka hapo mengine unaweza kuongeza. Ila ili uanze kwa amani inabidi uwe na kama milioni 7 angalau.
 
I think the business now is just about saturated, kama upo mikoani unaweza kuagiza bidhaa kutoka Dar..., lakini kama upo Dar Unaweza ukaagiza eitheir China au South Africa.

Now inategemea kama unauuza rejareja just agiza hapo hapo dar ila kama unataka kuuza jumla inabidi uagize from China au South Africa.., na angalia hapa kwa kucheki bei www.alibaba.com lakini beware too many scammers

Kuhusu soko inabidi uangalie market sehemu ulipo. Another market segment ni kupata tender kusupply kwenye mashirika na halmashauri lakini pia beware hawa jamaa mpaka upate tender mpaka uonge sana na sometimes malipo yanachelewa.

Kumbuka kwamba profit margin especially kwenye karatasi ni ndogo so its all about volume you need to sell a lot, kuhusu mtaji start as small as you can then build your way up then utajifunza through the process.
 
Kuna rafiki yangu anafanya hiyo b'ness. Ngoja niongee nae kama vipi nitakuconnect nae akuelezee zaidi.
 
Thanks Mkuu. Lakini nimecheck alibaba A4 paper per caton zina range from USd 2.00 - 2.80 in China sasa hapa Dar ukinunua Caton unauziwa almost Ts. 29000 equivalent to 20 USD nadhani bado karatasi profit margin ni nzuri. mimi nimeanza this business huu ni mwaka wa pili naona inalipa kiasi fulani.
I think the business now is just about saturated, kama upo mikoani unaweza kuagiza bidhaa kutoka Dar..., lakini kama upo Dar Unaweza ukaagiza eitheir China au South Africa.

Now inategemea kama unauuza rejareja just agiza hapo hapo dar ila kama unataka kuuza jumla inabidi uagize from China au South Africa.., na angalia hapa kwa kucheki bei www.alibaba.com lakini beware too many scammers

Kuhusu soko inabidi uangalie market sehemu ulipo, another market segment ni kupata tender kusupply kwenye mashirika na halmashauri lakini pia beware hawa jamaa mpaka upate tender mpaka uonge sana na sometimes malipo yanachelewa.

Kumbuka kwamba profit margin especially kwenye karatasi ni ndogo so its all about volume you need to sell a lot. kuhusu mtaji start as small as you can then build your way up then utajifunza through the process
 
Biashara yoyote unayotaka kufanya itategemea na wewe mwenyewe kama unaipenda,unaijua,umefanya utafiti wa kutosha wa soko na kiasi cha mtaji ulionao. Ili mtu akushauri unatakiwa uwe muwazi zaidi. Kwa mfano hujatuambia una mtaji kiasi gani unataka kuuza jumla au rejareja uko Dar au mikoani nk.

Pia usiangalie wenzako wanafanya biashara hiyo na kufanikiwa na wewe ukafikiria kuwa ukianzisha biashara hiyo utafanikiwa. Mara nyingi hakuna mtu atakaye kupa siri zake za biashara kirahisi. Tupe details tukushauri zaidi. Kwanza kwa nini unataka kuanzisha biashara ya stationery kitu gani kimekuvutia mpaka ukaamua kufanya biashara hiyo?
 
Thanks Mkuu. Lakini nimecheck alibaba A4 paper per caton zina range from USd 2.00 - 2.80 in China sasa hapa Dar ukinunua Caton unauziwa almost Ts. 29000 equivalent to 20 USD nadhani bado karatasi profit margin ni nzuri. mimi nimeanza this business huu ni mwaka wa pili naona inalipa kiasi fulani.

Ndio ni kweli kama anataka kuuza jumla na mtaji ni mkubwa then anaweza akaagiza china au South Africa (nadhani wengi wanaagiza huko) ambapo nadhani CIF price mpaka dar Double A inaweza ikawa about 5usd per carton hapo container linaweza likawa na ream 8000 bila pallet (20f Container) i.e. 1600 boxes without pallet au 1560 boxes with pallet.

So kama clearing ikienda vizuri anaweza aka-end up with a good package. Nadhani mikoani kwa sasa karatasi carton its about 35,000/= so akinunua dar kwa 29,000/= gross profit ni 6,000/= before transport, am not sure about transport hapa itacost ngapi.

Therefore afanye research it might pay lakini asisahau duty and taxes sina uhakika karatasi wanatax at what percentage, pia gharama za clearing na upuuzi wa pale bandarini kuhonga hapa na pale. For sure akijipanga there is a good package to be made, especially aki-cut the middle men.
 
Hii thread ni nzuri ikiwa utapata feedback kwa walionza biashara hiyo.

Mimi binafsi bado nina nia ya kuanzisha biashara hii na kilichonivutia zaidi ni kuwa nilikuwa nanunua vifaa vya ofisi pale Pran Pen Corner kwa kweli jamaa wanauza vitu in very reasonable price na kwa kuwa sasa nimehamia Tanga kimaisha ndio imenijia Idea hii ya kutaka kufungua biashara hii na kuwaweka wao kama main supplier wa vitu vingi vya stationery.

Mtaji bado unasumbua na kama nitapata feedback nzuri itanosaidia sana na nitapata mawazo mazuri zaidi jinsi ya ku approach biashara hii.

Tunasubiri michango yenu wana JF
 
Duty ni 25% and VAT is 18%. Shughuli inakuja kwenye clearing sasa Hivi TRA wanauplift value kwa hiyo kodi inakuwa kubwa uanze kubishana nao usubmit proof of payment na blaa blaa nyingi kwa hiyo kunausumbufu mkubwa na ucheweleshwaji kwenye clearing. Mtu usipokuwa makini profit inamegwa na cost za clearing.
Ndio ni kweli kama anataka kuuza jumla na mtaji ni mkubwa then anaweza akaagiza china au South Africa (nadhani wengi wanaagiza huko) ambapo nadhani CIF price mpaka dar Double A inaweza ikawa about 5usd per carton hapo container linaweza likawa na ream 8000 bila pallet (20f Container) i.e. 1600 boxes without pallet au 1560 boxes with pallet.

So kama clearing ikienda vizuri anaweza aka-end up with a good package..., nadhani mikoani kwa sasa karatasi carton its about 35,000/= so akinunua dar kwa 29,000/= gross profit ni 6,000/= before transport, am not sure about transport hapa itacost ngapi...,

Therefore afanye research it might pay lakini asisahau duty and taxes sina uhakika karatasi wanatax at what percentage..., pia gharama za clearing na upuuzi wa pale bandarini kuhonga hapa na pale...., for sure akijipanga there is a good package to be made..., especially aki-cut the middle men
 
Kaka kuwa makini hapa ni 2usd-2.8usd per ream and not carton so if is 2.4usd +50%of2.4=3.6usd *1500=5350tsh per ream kwahiyo wewe utauza bei gani? so the profit is not good but you can try. lla kuwa muangalifu usije poteza hela yako kufuata vya bei rahisi kwa scammers.
 
Duty ni 25% and VAT is 18%. Shughuli inakuja kwenye clearing sasa Hivi TRA wanauplift value kwa hiyo kodi inakuwa kubwa uanze kubishana nao usubmit proof of payment na blaa blaa nyingi kwa hiyo kunausumbufu mkubwa na ucheweleshwaji kwenye clearing. Mtu usipokuwa makini profit inamegwa na cost za clearing.

Just happen to me niliagiza mzigo a week ago, customs ilikuwa 30,000/= lakini waka-uplift wakasema eti nilipe 300,000/= nilikuja juu mpaka nikawapa website ya sehemu niliyonunua proof of payment nikawaambia I Have an account na suppliers huwa ninatransfer pesa through paypal/credit card mpaka zikiisha ndio naendelea. Hawa watu wapuuzi sana. Hii nchi ishaoza kabisa.
 
Kaka kuwa makini hapa ni 2usd-2.8usd per ream and not carton so if is 2.4usd +50%of2.4=3.6usd *1500=5350tsh per ream kwahiyo wewe utauza bei gani? so the profit is not good but you can try. lla kuwa muangalifu usije poteza hela yako kufuata vya bei rahisi kwa scammers.
Hapana mkuu ni per carton.
 
Thank you Very Much.

I think the business now is just about saturated..., kama upo mikoani unaweza kuagiza bidhaa kutoka Dar, lakini kama upo Dar Unaweza ukaagiza eitheir China au South Africa...,

Now inategemea kama unauuza rejareja just agiza hapo hapo dar ila kama unataka kuuza jumla inabidi uagize from China au South Africa.., na angalia hapa kwa kucheki bei www.alibaba.com lakini beware too many scammers

Kuhusu soko inabidi uangalie market sehemu ulipo. Another market segment ni kupata tender kusupply kwenye mashirika na halmashauri lakini pia beware hawa jamaa mpaka upate tender mpaka uonge sana na sometimes malipo yanachelewa.

Kumbuka kwamba profit margin especially kwenye karatasi ni ndogo so its all about volume you need to sell a lot, kuhusu mtaji start as small as you can then build your way up then utajifunza through the process
 
Asante kwa Mchango wako.

Niko Arusha, Nimeifikiria hii biashara Kwasababu ninahitaji pesa (Something to generate income). Sasa najaribu kuangalia ni biashara gani atleast itanizungushia pesa, hapo hapo kwenye hiyo stationary niweke kama workshop ya ICT.

Kuna baadhi ya Vifaa vya kuanzia ninavyo. Computers/Binding etc. Bado Mzigo. Ila ninategemea kuanza na kama 3.5 Millions hivi.Na kimsingi nimewaza Stationary bse as you said naona kuna watu pia kama wamefanikiwa hivi through this business ( Ingawa hai-sound vizuri kufanya bse watu wanafanya).

Stand to be advised and corrected.
Biashara yoyote unayotaka kufanya itategemea na wewe mwenyewe kama unaipenda,unaijua,umefanya utafiti wa kutosha wa soko na kiasi cha mtaji ulionao. Ili mtu akushauri unatakiwa uwe muwazi zaidi. Kwa mfano hujatuambia una mtaji kiasi gani unataka kuuza jumla au rejareja uko Dar au mikoani nk.

Pia usiangalie wenzako wanafanya biashara hiyo na kufanikiwa na wewe ukafikiria kuwa ukianzisha biashara hiyo utafanikiwa. Mara nyingi hakuna mtu atakaye kupa siri zake za biashara kirahisi. Tupe details tukushauri zaidi. Kwanza kwa nini unataka kuanzisha biashara ya stationery kitu gani kimekuvutia mpaka ukaamua kufanya biashara hiyo?
 
Asante kwa Mchango wako.

Niko Arusha,
Since upo Arusha jaribu kucheki vifaa Nairobi they might be cheaper kuliko Dar, ingawa hapa linaingia suala la ushuru unless unajua njia za panya, Fanya Research kama hii biashara inalipa Arusha. Kuhusu mambo ya photocopies na typing kama upo karibu na chuo (universities) unaweza ukapata constant customers, Internet watalii ni wengi Arusha utapata watu bila shida., anyway sometimes its all about LOCATION, LOCATION LOCATION.

Anyway with workshop ukiwa mkweli na ukabuild customer base. Utapata repeat customers na wataambiana na watakufata anywhere you are, ont look for a quick buck Honest people are hard to find siku hizi, its better to have 10 satisfied customers they will keep on coming back kuliko..., kila siku akija mteja mpya unamdissapoint and he never return (I mean kuwa mkweli kama huwezi unasema huwezi na ukimwambia mtu njoo kesho kweli akija kesho akute issue yake tayari)
 
I salute you kiongozi. Unamwaga very constructive ideas.

Since upo Arusha jaribu kucheki vifaa Nairobi they might be cheaper kuliko Dar ingawa hapa linaingia suala la ushuru unless unajua njia za panya. Fanya Research kama hii biashara inalipa Arusha kuhusu mambo ya photocopies na typing kama upo karibu na chuo (universities) unaweza ukapata constant customers, Internet watalii ni wengi Arusha utapata watu bila shida. Anyway sometimes its all about LOCATION, LOCATION LOCATION.

anyway with workshop ukiwa mkweli na ukabuild customer base, utapata repeat customers na wataambiana na watakufata anywhere you are... dont look for a quick buck Honest people are hard to find siku hizi, its better to have 10 satisfied customers they will keep on coming back kuliko, kila siku akija mteja mpya unamdissapoint and he never return, (I mean kuwa mkweli kama huwezi unasema huwezi na ukimwambia mtu njoo kesho kweli akija kesho akute issue yake tayari)
 
Back
Top Bottom