Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,753
- 7,844
- Thread starter
- #21
Sasa ninaona tatizo.
Shem, opsss kaka mbu huyu shemejio anasumbuliwa na guilty conscious kwani anajichukulia kuwa ndiye chanzo cha wao kukosa watoto (Ile abortion ya ujanani) sasa kung'ang'ania kwake ni denial status hataki kukubaliana na ukweli (na kweli si rahisi kukubali kuwa eyey ndo chanzo) so ana amini iko siku atafanikiwa na ku-prove wrong walimwengu. Isitoshe pengine alikwishaapa kwa mumewe kuwa yeye ujanani alikuwa 'mtoto mzuri' sasa report ya dr imetoa visivyo so anatamani kuprove wrong madr. ili amhakikishie Mr. kuwa kweli yeye alikuwa mtulivu na madr. ndoi waliokosea.
Kwa hali hii Kaka ni ngumu kusolve unless mdada akubali kuwa hata fanikiwa na mume amsaidie kumpa confidence kuwa yameshamwagika hayazoleki but amwonyeshe upendo na kumhakikishia atampenda despite all.
...kwa muono wangu, nadhani huyo bi mdogo hataridhika mpaka Bw'mkubwa roho itapomtoka... Iweje baada ya kutendewa yote hayo yeye bado kang'ang'ana tuuuu apate mtoto wake wa kumzaa mwenyewe?
Ingekuwa Bi mdogo huyo hajawahi kubeba mimba kweli, lakini ripoti za kidakitari tayari zinaonyesha alipata mimba, ikakwama kwenye mirija (ectopic) na ndio ikawa chanzo cha upasuaji ule na kuondoa mrija, ...
Bw'mkubwa yeye keshaona ya kale hayanuki, anampenda mkewe na anamchukulia kama mzazi mwenzake kwa hao mabinti zao, Bi mdogo yeye aahhh... Hataki, hataki, hataki,... anataka mimba yake, na asukume mtoto wake.
Mw'j1, shukran sana. Tuwasubiri na wengine watavyochangia hiyo "Guilty conscious" ya bi mdogo huyo itatibikaje..nawe utuletee tafakari pana zaidi kutatua/kupunguza usongo huo.