Ushauri: Nampenda ila tatizo ni mwanaume aliyekataliwa kwao

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,013
1,634
Habari wadau,

Nimejitokeza kwenu kuomba ushauri katika jambo hili linalonikwaza. Nimeingia katika Mahusiano na binti ambae alikuwa na mtu wake wa awali ambae walipanga kuja kufunga ndoa baadae.

Lakini wazazi wa binti washamwambia ukweli binti yao kwamba hataolewa na huyo jamaa. Na mimi nilivyomfuata binti akaniambia ukweli wote kwamba yupo mtu ila aliekataliwa kwao na akimwambia jamaa hataki kuelewa.

Binti amekubali kuwa na mimi ila mashaka yangu jamaa akirudi huko aliko kwani yuko mbali hataweza kuniibia?

Nawasilisha
 
Kama jamaaa alikataliwa, unajiaminisha vipi kwamba na wewe hutokataliwa??
 
Mkuu jama alikataliwa kwao na binti hajakataliwa na binti.vp wewe umekubaliwa kwao na binti?
 
Yupo na wewe kwa sababu anajua una vigezo ambavyo kwao hawatavikataa au kwa sababu anakupenda?

anyway maisha ni mafupi mno kuumia sana fanya hivi; mketishe chini mzungumze kinagaubaga akueleze kwa uwazi na wewe umuambie hofu yake msikilize maneno yake na matendo yake pia.

Baada ya hapo utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kufanya maamuzi.

NB: Utasema umeshaungumza naye lakini najua hujamwambia hofu yako. Kuwa open and direct kwake ili awe open and direct kwako. mueleze hofu yako na ninaamini atakueleza ukweli wote hata kama si kwa maneno basi sura na other non verbal cues zitakupa jibu.
 
Kama wameachana,tambua hawajaachana kwakupenda kwahivyo ni vyema uzungumze nae dhamira yako kwake in deep...laasivyo uwezekano wa kuendelea kufanya yao akirudi ni kubwa sana.
 
Ahsante Mkuu huo ndio ushauri ninaohitaji
 
Kama wameachana,tambua hawajaachana kwakupenda kwahivyo ni vyema uzungumze nae dhamira yako kwake in deep...laasivyo uwezekano wa kuendelea kufanya yao akirudi ni kubwa sana.

Huo ndo ukweeli... na mchungu kuusikia.. na kuuamini... maana nishashuhudia mara kadhaa watu wanaoachana kwa style hiyo.. wakiwa wanapendana.. na mwisho wa siku wanalianzisha kwa chini chini... mwisho utalea katoto ka jamaa.
 
Ila 2016 hii ni sababu gani na mamlaka gani inayowapa wazazi uwezo wa kumkataa mpenzi wa mtu kweli?

Unajua pamoja na kukupa ushauri unatakiwa utuelimishe na wewe...binti amekuambia ni sababu gani huyo mchumbake wa awali alikataliwa? ni jamii ya watu wa wapi? au familia ya binti ipoje? Tuelimishe na sisi...sio tukupe ushauri bure bure tu bana! au yuko chini ya miaka 18 kwa hiyo hadi wazazi waridhie?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom