Naomba ushauri na tiba ya kikohozi na mafua kwa watoto

asante,nitajaribu kumuongezea idadi ya kumpa mara mm nilikua nampa mara mbili

haswaa mara mbili haitoshi mkuu.asali ni dawa nzuri sana. pia usimpe vinywaji vya baridi.

Angalizo: kikohozi kwa watoto ni kitu cha kawaida ila kinaweza kuleta madhara makubwa kisibitibiwa mapema kikaisha, matatizo hayo ni pamoja na ya moyo, yanaweza kujitokeza hata miaka 10 baadaye.
 
Yaaa mie nlimapa dawa zote....kuanzia za hosp...za kichina...za kienyeji...za kisuna....lakini wap
...mtoto akila anatapika...anakohoa mpaka napata wendawazimu.....maspeshalist wengi wako bize hata hawachunguzi deeply.....sasa nikakutana na kijana flan....a doctor...with a lot of concerns...kwa watoto...akamcheki akanambia ni matezi...nikaenda...wakamtoa....loh...mtoto yuko fit sana sasahv....yaaan i can see life in her....!! My take....nenda akachekiwe matezi tu....huenda ndo shida....
 
Yaaa mie nlimapa dawa zote....kuanzia za hosp...za kichina...za kienyeji...za kisuna....lakini wap
...mtoto akila anatapika...anakohoa mpaka napata wendawazimu.....maspeshalist wengi wako bize hata hawachunguzi deeply.....sasa nikakutana na kijana flan....a doctor...with a lot of concerns...kwa watoto...akamcheki akanambia ni matezi...nikaenda...wakamtoa....loh...mtoto yuko fit sana sasahv....yaaan i can see life in her....!! My take....nenda akachekiwe matezi tu....huenda ndo shida....

nimekupata
 
Je, pana history yoyote ya ugonjwa huo au wenye kufanana na huo kwa upande wa familia za wazazi (AU HISTORIA YA UGONJWA WOWOTE WA KURITHI) ?
 
Dada yangu pole kwa tatizo hilo la mtoto, ila kwa ufupi kama umetumia dawa zote na hakuna mafanikio, na pum na minyoo wamepima hakuna. apo kilicho baki suspect kubwa sana ni TB, nenda kwa dor wa watoto tena uongee naye kama mnawaza kupima TB. Mtoto mdogo kupata TB ni rahisi sana haswa maeneo anayoshinda kama yatakuwa hayana hewa ya kutosha na vumbi pia au na watoto anao kaa nao. na zuria nyumbani linaweza kuwa linampa vumbi mbaya. suspect kubwa zaidi ni TB. Jaribu kupima hiyo ila kuwa na imani atapoma kabisa nimemuona mtoto wa ndugu yangu naye ilikuwa hivyo kila sehemu wameangaika kumbe mwishoe wakaja kugundua ni TB. Kwana Jina la Yesu na apone mtoto wako AMEN
 
jamani naombeni msaada,
mtoto wangu anasumbuliwa sana na kikohoz mara kwa mara na ana umri wa miaka miwili,nimempleka hosptal mbalimbali na kunywa dawa lakini hamna matumaini.mara ya mwisho nilielekezwa kwa dr.mmoja wa watoto kariakoo akaandikiwa sindano na dawa, cha ajab ni kua baada ya kumaliza doz tu, hali imerud kama zamani. asanten
Ushauri uliopewa ikiwa kama mwanao bado hajapona nitafute mimi Dawa ya kumtibu mwanao ninayo ukiweza kunitafuta kwa What's App +905013460377
 
Hili ni tatizo kwa mtoto wangu pia. Ana miaka miwili nimetumia kila dawa.kwasasa anatumia asali na magadi kidogo inampa nafuu.
 
bigstock-afro-american-male-pediatricia-440174711.jpg

Kikohozi na Mafua kwa watoto


Maradhi haya mara nyingi husababisha na virusi. Virusi hawa husambaa kwa urahisi kwa njia ya hewa.Mgonjwa akipiga chafya au akikohoa wadudu husambaa kwenye hewa. Mtoto anaweza kuugua mafua na kikohozi kati ya mara 3-8 kwa mwaka. Wakati mwingine mtoto anaweza kupata maradhi haya kwa kufuatana. Hata hivyo mtoto anayeishi nyumba moja na mtu anayevuta sigara yuko hatarini zaidi kupata mafua na kikohozi.


Dalili
Dalili kuu za ugonjwa huu ni kukohoa na kutoa kamasi laini kama majimaji. Kikohozi husumbua zaidi wakati wa usiku.Dalili nyingine ni homa,kukosa hamu ya kula,uchovu na maumivu ya kichwa. Wakati mwingine mtoto anaweza kutapika baada ya kukohoa.


Matibabu ya mafua na kikohozi.
Hakuna miujiza katika kuponyesha matatizo haya. Siku ya 2-3 dalili husumbua zaidi,lakini hupungua makali siku zinazofuatia baada ya kinga ya mwili kuwashambulia wale virusi.

Antibiotiki haziuwi virusi hivyo haziwezi kusaidia kutibu virusi.
Matibabu hulenga hasa kupunguza dalili. Paracetamol hutumika kutibu homa na maumivu. Epuka kuwapa watoto Aspirin.

Pia maji yenye chumvi (saline) hutumika kuzibua pua zilizoziba. Kuna maji ya namna hii kwenye maduka ya dawa unaweza kununua na kuminya matone machache kwenye pua.

Hakikisha mtoto anakunywa maji ya kutosha pia anapata lishe bora wakati huu anapokuwa ana maradhi haya.

Katika nchi nyingine dawa za kikohozi na mafua zinapigwa marufuku wa watoto walio chini ya miaka sita ,lakini zinaweza kutumika kwa watoto kati ya miaka 6-12.

Usafi wa mikono ni wa msingi kuzuia maambuki ya mafua na kikohozi kwa watoto.


Credit: Dr. Masua
 
Majani 2 au 3 ya mbaazi ambazo hazijakomaa kama anaweza atafune kama jojo au big g ila asiya meze,

muda wa kulala asukutue adi kooni kwa mafuta ya habati soda!

Hakika kwa muda wa siku 3 tatizo litakuwa limekwisha
 
Nauliza kama kuna uwezekano wa mtoto mdogo wa siku 11 kupewa dawa ya mafua japo ya syrup,au kama kuna madhara kufanya hivi.
 
Nauliza kama kuna uwezekano wa mtoto mdogo wa siku 11 kupewa dawa ya mafua japo ya syrup,au kama kuna madhara kufanya hivi.

Kama mama yake ananyonyesha maziwa ya kifuani mama ale matunda yenye vitamin c kwa wingi na atapass kwa mtoto, hii ni dawa nzuri.
 
Ukiona yamembana sana unayanyonya kutoka kwenye pua zake. Mtoto wa umri huo akiumwa mafua lazma uchanyanyikiwe!
 
Nauliza kama kuna uwezekano wa mtoto mdogo wa siku 11 kupewa dawa ya mafua japo ya syrup,au kama kuna madhara kufanya hivi.

ImageUploadedByJamiiForums1431498953.455389.jpg


Dawa hii ilimsaidia sana mwanangu ni ya kuspray. Unaspray katika pua ya mtoto kainunue itamsaidia sana. Tafadhari usiruhusu mama amnyonye pua bado ubongo haujakomaa. Hiyo ni 5000 tu.
 
Back
Top Bottom