Naomba ushauri na tiba ya kikohozi na mafua kwa watoto

jamani naombeni msaada,
mtoto wangu anasumbuliwa sana na kikohoz mara kwa mara na ana umri wa miaka miwili,nimempleka hosptal mbalimbali na kunywa dawa lakini hamna matumaini.mara ya mwisho nilielekezwa kwa dr.mmoja wa watoto kariakoo akaandikiwa sindano na dawa, cha ajab ni kua baada ya kumaliza doz tu, hali imerud kama zamani. asanten

Na wangu ana tatizo kama lako

Alikua akianza kukohoa hawezi kula ni kutapika hadi unamuonea huruma, tukampa dawa za kikohozi kinapungua kwa muda kisha kinarudi tena, akianza kukohoa usiku hamlali, afya ikazorota vibaya mno.

Kila tukifanya vipimo vya kifua wanasema kipo sawa, akalazwa Aga khan kwa uchunguzi zaidi hawakuona kitu, baadae wakasema ni pumu japo kifua hakibani wala hana shida ya kuhema.

Tuliishia kumpa dawa flan unachanganya na asali japo wanashauri uweke na yai bichi, imemsaidia kwa kweli namshukuru Mungu.
 
Kikohozi cha muda mrefu kwa watoto kinaweza kusababishwa na v2 vingi ila kimojawapo inaweza kuwa pumu (asthma ), inahitajika kufahamu pia Kikohozi hicho anatoka na makohozi ama ni kikavu na kinazidi hasa wakati upi wa msimu au wa siku .je huwa anatumia dawa gani walau kukituliza na je anapata homa ?maelezo haya yatasaidia daktar kujua tatizo na vipimo gani afanye.. pole sana naomba utupatie mrejesho wa matibabu
 
mpe asali mbichi. alambe kutwa hata mara 4.
Kama kuna dawa anazotumia basi tofautisha angalau saa moja kati ya mda wa kunywa dawa na kulamba asali.
 
Alikua akianza kukohoa hawezi kula ni kutapika hadi unamuonea huruma, tukampa dawa za kikohozi kinapungua kwa muda kisha kinarudi tena, akianza kukohoa usiku hamlali, afya ikazorota vibaya mno.

Kila tukifanya vipimo vya kifua wanasema kipo sawa, akalazwa Aga khan kwa uchunguzi zaidi hawakuona kitu, baadae wakasema ni pumu japo kifua hakibani wala hana shida ya kuhema.

Tuliishia kumpa dawa flan unachanganya na asali japo wanashauri uweke na yai bichi, imemsaidia kwa kweli namshukuru Mungu.

hiyo dawa ni gan,mana hata hilo yai na asali nnampa asubuh, uck ucpompa bac hatulal,kifup inamsaidia kwa mda
 
Ninda kwa Dr. Anthon daktari bingwa wa watoto pale Kinondoni dispensary hilo ni tatizo dogo sana kwake.
 
hiyo dawa ni gan,mana hata hilo yai na asali nnampa asubuh, uck ucpompa bac hatulal,kifup inamsaidia kwa mda

Ntaiulizia jina nikutumie kama sio kuiweka hapa kwa faida ya wengine pia, ni majani ya mti ilikua uamuzi mgumu sana lakini hatukua na jinsi. Unachemsha kisha unachanganya na asali. Huyu ilikua ukiweka yai hataki hata kusikia harufu yake.
 
Bwana Ndea,
asante sana,kikohozi chake ni kikavu, na kuhusu dawa kwa sasa anatumia phamacoff ,lakn ameshawah kutumia ,zecuf ,na mara ya mwisho niliongezewa dawa inaitwa ,alerid, na kuhusu msimu ni marazote sema kinazidi sana ucku akiwa amelala ,asubuh ile anaamka na kwakua knamsumbua anawah sana kuamka yani saa kumi yuko macho na mchana akijaribu kulala basi balaa atakohoa na hawezi lala zaidi ya robo saa,mara ya mwisho waliniambia damu yake imejaa bacteria,lakin mbona walimchoma hzo sindano na dawa kanywa lakin hali ndo hivyohivyo yani ilitulia tu pale alipokua amatumia dozi
 
Ntaiulizia jina nikutumie kama sio kuiweka hapa kwa faida ya wengine pia, ni majani ya mti ilikua uamuzi mgumu sana lakini hatukua na jinsi. Unachemsha kisha unachanganya na asali. Huyu ilikua ukiweka yai hataki hata kusikia harufu yake.

asante,yai bich anakunywa bila tatzo sema ndo hivyo
 
Mpeleke Muhimbilia kwa specialist wa koo, amenisadia sana tatizo hilo, mwanangu kwa sasa anaendelea vizuri.
 
jamani naombeni msaada,
mtoto wangu anasumbuliwa sana na kikohoz mara kwa mara na ana umri wa miaka miwili,nimempleka hosptal mbalimbali na kunywa dawa lakini hamna matumaini.mara ya mwisho nilielekezwa kwa dr.mmoja wa watoto kariakoo akaandikiwa sindano na dawa, cha ajab ni kua baada ya kumaliza doz tu, hali imerud kama zamani. asanten

Dawa na dose kiboko ya hilo tatizo la mwanao ni: 1. mpatie mboga za majani na azile kama mbuzi/ ng'ombe/ sungura, 2. mpatie maziwa ya kutosha, 3. mpatie matunda ya kutosha, 4. mpatie mayai ya kuku wa kienyeji, 5. mpatie nyama ya kuku, ngo'ombe, na samaki mara kwa mara ikiwemo dagaa, 6. anywe maji ya kunywa mengi kwa siku mpaka uone mkojo wake unafanana na maji wala sio kahawa, 7. hakikisha nyumba yako kwa ndani hakuna vumbi, na hachezi kwenye vumbi nje (kama unaweza weka pavement stones kwenye uwanja wa nyumba yako).
 
Back
Top Bottom