Naomba ushauri na tiba ya kikohozi na mafua kwa watoto

4X4byfar,

Jaribu kumpa juice ya machungwa au limao uliyotengeneza mwenyewe km hali bado,
Ni vema ukawaona Madaktari wa E.N.T huwenda mtoto ana nyama za puani (ADENOIDS)kwani mtoto wangu aliwah kuwa na tatizo la mafua kila siku na mwisho wa siku ikagundulika hizo nyama.
 
Dah! Kuna waganga humu ndani! Tatizo liko kwenye pua vitunguu vipakwe kwenye nyayo za miguu, mmmh hii kali

Mwaya mpeleke mtoto kwa ENT Surgeon

anga vitunguu swaumu mpake ktk nyayo za miguu
 
Pole aise, kwahiyo hunusi chochote? Rudi tena kwa Daktari may be watakushauri ufanye nini ili uweze kunusa tena

Kuwa makini na dawa zinazopendekezwa. Miezi miwili iliyopita niliugua mafua na pua kuziba. Nilipowaona Hospitali nikaandikiwa dawa fulani hivi ya matone. Kweli ukiweka tone moja tu pua mwaaaaa zinazibuka . Lakini amini toka wakati huo sisikii/sinusi harufu yeyote. Nimepoteza uwezo wangu wa kunusa. Kabla nilikuwa sensitive sana kwa harufu lakini sasa hata harufu ipi siinusi!
 
Mfukize tu utaona mtoto anakua safi sana. kama ukiona bado nenda kwa specialist wa watoto anaitwa Kuboja yuko Mhimbili na pia anakua Aghakhan siku za weekend...
 
twanga kituungu swaumu mpake kwenye nyayo ila usimvalishe na soksi ataungua,, kisha loweka vicks kwenye maji moto kisha mjifukize kwa ku- inhale mvuke mpaka maji yapoe,, vicks nyingine mpake kifuani na chini ya pua. mwanangu ana miaka miwili inamsaidia kila anaposhikwa na mafua koz dawa za hosp zilichemsha.
 
kama ulivyosema yawezekana ana allergy, kitalaamu inaitwa allergic rhinitis yaweza tibiwa vizuri na daktari wa watoto au physcian.
 
Wataalamu nisaidieni,

Mwanangu anasumbuliwa na kikohozi zaidi ya miezi miwili sasa! Nimetumia dawa za hospitalini lakini wapi na mara ya mwisho niliandikiwa sindano kwa muda wa siku tano (sikumbuki aina ya dawa)! lakin bado haponi ANABANJA SANA cha ajabu mafua akitibiwa anapona na baadae yanarudi tena nilijaribu kumtengenezea dawa ya kienyeji kwa kuchanganya na kuchemsha asali mbichi, malimao, tangawizi iliyosagwa na vitunguu saumu nimempa dose hiyo hajapona mpaka sasa!

Dawa za hospitalini alizowahi kutumia ni pamoja na AMOXILILIN SYRUP,CEFAMOR SYRUP, ELYCLOX SYRUP,zingine sizikumbuki.

NAOMBENI MSAADA WENU.

Mwanzoni nilikuwa naishi sehemu za joto na kwa sasa naishi sehemu ya baridi sijui kama nayo ni sababu lakini najitahidi kuwavalisha masweta lakini hakuna nafuu.
 
Tiba nyingine unaweza kuzipata kutokana na mazingira anapoishi hasa nyakati za usiku hali ya hewa hua sio nzuri sana kwani baridi inaongezeka,jaribu kuhakikisha mwanao anapunguza au kutokuvuta kabisa hewa yenye ubaridi,kwa kumlaza katika chumba chenye joto,pia jitahidi kumexpose mahali pasipokua na dalili yoyote ya vumbi wala harufu harufu hiyo yaweza msaidia sana.
 
wanapona baada ya muda wanaanza tena! kukoroma alikua anakoroma sana

sasa nenda hospital kubwa kama KCMC kapige Xray ya kichwa. naamini atakutwa na nyama za puani. hizi nyama za puani huwa zinaleta sana infection isiyoisha kwa watoto,... mafua wakati wote kikohozi n.k
 
sasa nenda hospital kubwa kama kcmc kapige xray ya kichwa.. naamini atakutwa na nyama za puani. hizi nyama za puani huwa zinaleta sana infection isiyoisha kwa watoto,... mafua wakati wote kikohozi n.k

ok! nashukuru kiongozi kwa ushauri wako
 
Jamani anayeijua tusaidiane tu, kama ni hospitali tumeenda sana, but dawa anazopewa either hazimsaidii au anapona kwa wiki moja tu kinaanza tena.Tusaidiane jamani yamenishinda mwenzenu
 
Ana umri gani,mazingira uishiyo yakoje,ww umewahi ugua kifua kikuu au mtu wa karibu,mbali na kikohozi kuna dalili nyingine aonyeshazo?Haya maswali ni muhimu sana uende kujadili na daktari hospitali
 
Jamani naombeni msaada,

Mtoto wangu anasumbuliwa sana na kikohozi mara kwa mara na ana umri wa miaka miwili. Nimempleka hospitali mbalimbali na kunywa dawa lakini hamna matumaini.

Mara ya mwisho nilielekezwa kwa daktari mmoja wa watoto Kariakoo akaandikiwa sindano na dawa, cha ajabu ni kuwa baada ya kumaliza dozi tu, hali imerudi kama zamani.

Asanteni.
 
jamani naombeni msaada,
mtoto wangu anasumbuliwa sana na kikohoz mara kwa mara na ana umri wa miaka miwili,nimempleka hosptal mbalimbali na kunywa dawa lakini hamna matumaini.mara ya mwisho nilielekezwa kwa dr.mmoja wa watoto kariakoo akaandikiwa sindano na dawa, cha ajab ni kua baada ya kumaliza doz tu, hali imerud kama zamani. asanten
Pole sana,kwa mara ya mwisho kumpatia dawa ya minyoo ni lini?
watoto wa umri huo kama hajanywa dawa ya minyoo muda mrefu
huwa ina tabia ya kufuata njia ya chakula hadi kooni na hapo huanza kumkereta
mtoto na kumsababishia kikohozi,unaweza kumaliza dawa zote za kifua usione matokeo mazuri.

Nakushauri mpime na minyoo au nunua dawa za watoto za minyoo,inaweza kumsaidia.
 
Pole sana,kwa mara ya mwisho kumpatia dawa ya minyoo ni lini?
watoto wa umri huo kama hajanywa dawa ya minyoo muda mrefu
huwa ina tabia ya kufuata njia ya chakula hadi kooni na hapo huanza kumkereta
mtoto na kumsababishia kikohozi,unaweza kumaliza dawa zote za kifua usione matokeo mazuri.

Nakushauri mpime na minyoo au nunua dawa za watoto za minyoo,inaweza kumsaidia.

asante,ila katika hizo dawa ambazo amewah kula ya minyoo nayo imo na amekunywa kama mwezi na nusu hv.
 
jamani naombeni msaada,
mtoto wangu anasumbuliwa sana na kikohoz mara kwa mara na ana umri wa miaka miwili,nimempleka hosptal mbalimbali na kunywa dawa lakini hamna matumaini.mara ya mwisho nilielekezwa kwa dr.mmoja wa watoto kariakoo akaandikiwa sindano na dawa, cha ajab ni kua baada ya kumaliza doz tu, hali imerud kama zamani. asanten

anatoa makohozi? km anatoa makohozi mpe expectorant cough ni dawa nzuri tu kwa watoto. pole xna
 
Back
Top Bottom