Naomba ushauri na tiba ya kikohozi na mafua kwa watoto

Slave

JF-Expert Member
Dec 6, 2010
5,314
2,635
1624004312984.png

Heshima kwenu wakuu wa jukwaa hili.

Jamani mtoto wangu ana tatizo la kikohozi kisichopona.Nimejaribu kumpa kila aina ya dawa ninazoshauriwa na madaktari matokeo hupata nafuu kwa wiki moja tu.

Mtoto huyu ana miaka 3 na nusu tangu kuzaliwa amekuwa na tatizo la kunyonya vidole hali inayonifanya nidhani kuwa pengine vidole ndio chanzo cha tatizo lake,maana kama mnavyojua watoto anaweza ashike hiki mala kile.

Kwa ufupi mimi na shemeji/ wifi yenu tumefika mahala tunamuonea huruma mwanetu juu ya kumnywesha madawa ya kila aina.

Naombeni msaada wakuu.



BAADHI WADAU WENYE TATIZO KAMA HILI
Wataalamu nisaidieni,

Mwanangu anasumbuliwa na kikohozi zaidi ya miezi miwili sasa! Nimetumia dawa za hospitalini lakini wapi na mara ya mwisho niliandikiwa sindano kwa muda wa siku tano (sikumbuki aina ya dawa)! lakin bado haponi ANABANJA SANA cha ajabu mafua akitibiwa anapona na baadae yanarudi tena nilijaribu kumtengenezea dawa ya kienyeji kwa kuchanganya na kuchemsha asali mbichi, malimao, tangawizi iliyosagwa na vitunguu saumu nimempa dose hiyo hajapona mpaka sasa!

Dawa za hospitalini alizowahi kutumia ni pamoja na AMOXILILIN SYRUP,CEFAMOR SYRUP, ELYCLOX SYRUP,zingine sizikumbuki.

Naombeni msaada wenu.

Mwanzoni nilikuwa naishi sehemu za joto na kwa sasa naishi sehemu ya baridi sijui kama nayo ni sababu lakini najitahidi kuwavalisha masweta lakini hakuna nafuu.

Jamani naombeni msaada,

Mtoto wangu anasumbuliwa sana na kikohozi mara kwa mara na ana umri wa miaka miwili.Nimempleka hospitali mbalimbali na kunywa dawa lakini hamna matumaini.

Mara ya mwisho nilielekezwa kwa daktari mmoja wa watoto Kariakoo akaandikiwa sindano na dawa, cha ajabu ni kuwa baada ya kumaliza dozi tu, hali imerudi kama zamani.

Asanteni.

Kuna mtoto wa miaka 6 anasumbuliwa sana na kifua tangu alipokuwa mdogo. Hasa usiku ndio anakohoa zaidi. Chanzo: siku moja alipokuwa na umri wa miezi 9 mama yake alikuwa anamuogesha. Kwa bahati mbaya sabuni ikamwingia puani na kumpalia. Tangu hapo amekuwa akikohoa hadi leo hii. Huwa kinatulia baada ya kupata dawa halafu baada ya muda kinaanza tena. JF doctors msaada tafadhari.

Za leo wandugu,

Mtoto wangu anasumbuliwa sana na mafua, yanamfanya kushindwa kupumua na kukosa raha kabisa hata ya kula. Nimejaribu dawa za hospitali za kuzibua naona hazimsaidii. Nini nitumie mbadala kinakachoweza kuzibua hizo pua!.

Asanteni.:embarassed2:

Jamani naombeni msaada,

Mtoto wangu anasumbuliwa sana na kikohozi mara kwa mara na ana umri wa miaka miwili. Nimempleka hospitali mbalimbali na kunywa dawa lakini hamna matumaini.

Mara ya mwisho nilielekezwa kwa daktari mmoja wa watoto Kariakoo akaandikiwa sindano na dawa, cha ajabu ni kuwa baada ya kumaliza dozi tu, hali imerudi kama zamani.

Asanteni.

BAADHI YA USHAURI ULIOTOLEWA NA WADAU
View attachment 246003

Kikohozi na Mafua kwa watoto


Maradhi haya mara nyingi husababisha na virusi. Virusi hawa husambaa kwa urahisi kwa njia ya hewa.Mgonjwa akipiga chafya au akikohoa wadudu husambaa kwenye hewa. Mtoto anaweza kuugua mafua na kikohozi kati ya mara 3-8 kwa mwaka. Wakati mwingine mtoto anaweza kupata maradhi haya kwa kufuatana. Hata hivyo mtoto anayeishi nyumba moja na mtu anayevuta sigara yuko hatarini zaidi kupata mafua na kikohozi.

Dalili
Dalili kuu za ugonjwa huu ni kukohoa na kutoa kamasi laini kama majimaji. Kikohozi husumbua zaidi wakati wa usiku.Dalili nyingine ni homa,kukosa hamu ya kula,uchovu na maumivu ya kichwa. Wakati mwingine mtoto anaweza kutapika baada ya kukohoa.

Matibabu ya mafua na kikohozi.
Hakuna miujiza katika kuponyesha matatizo haya. Siku ya 2-3 dalili husumbua zaidi,lakini hupungua makali siku zinazofuatia baada ya kinga ya mwili kuwashambulia wale virusi.

Antibiotiki haziuwi virusi hivyo haziwezi kusaidia kutibu virusi.
Matibabu hulenga hasa kupunguza dalili. Paracetamol hutumika kutibu homa na maumivu. Epuka kuwapa watoto Aspirin.

Pia maji yenye chumvi (saline) hutumika kuzibua pua zilizoziba. Kuna maji ya namna hii kwenye maduka ya dawa unaweza kununua na kuminya matone machache kwenye pua.

Hakikisha mtoto anakunywa maji ya kutosha pia anapata lishe bora wakati huu anapokuwa ana maradhi haya.

Katika nchi nyingine dawa za kikohozi na mafua zinapigwa marufuku wa watoto walio chini ya miaka sita ,lakini zinaweza kutumika kwa watoto kati ya miaka 6-12.

Usafi wa mikono ni wa msingi kuzuia maambuki ya mafua na kikohozi kwa watoto.

Credit: Dr. Masua

Hakuwezi kuwa na uhusiano kati ya kikohozi cha sasa akiwa na miaka 6 na kupaliwa maji ya sabuni miaka mi5 iliyopita. Huwa mnampeleka hospitali? Ameshaonwa na Paediatrician (daktari bingwa wa watoto)?

Nadhani kuna umuhimu wa mtoto huyo kuonwa na Paediatrician akamsikiliza vizuri kifua kwa kutumia stethoscope na pia kumfanyia X-ray ya kifua. Kuna magonjwa mawili ambayo huwa mara nyingi dalili yake ni kikohozi cha mara kwa mara kwa watoto, nayo ni Pumu (Asthma) na magonjwa ya moyo ya kuzaliwa (Congenital Heart Diseases).

Haya magonjwa daktari anaweza akayahisi kirahisi tu kwa kusikiliza kifua kwa umakini na/au kufanya X-ray.

Jaribu hii dawa; Mchanganyiko wa Asali ya nyuki wadogo, kiini cha yai bichi la kienyeji, magadi ya asili (yapo sokoni), binzari, limao, na kitunguu saumu punje mbilimbili ziponde ponde. Changanya kwa kipimo chochote then mpe mtoto kijiko kidogo cha chai kila siku asubuhi, mchana na jioni kwa siku saba. Pia akilala usimfunike na Blanketi, mfunike na Duveti. Pia asile vitu vyenye asili ya utamu kama lollipop, pipi na banzoka.
 
Kwanini usimpeleke mtoto kwa daktari akapimwe? tena ukizingatia kikohozi chenyewe ni cha muda mrefu.

daktari atachukua history na kufanya physical exam, halafu kushauri vipimo vipi vya maabara vifanyike na hatimaye kumwandikia dawa ya kutumia.

Nakushauri peleka mtoto apimwe na daktari, kulikoni kusubiri ushauri kutoka hapa.
 
Futota

Mkuu mpaka nafika hapa ujue tayari nilishafanya kumpeleka hospitali ndio maana nahisi pengine dawa zinaweza kuja kumdhuru. Kumbuka huwezi kufika hospitali ukapimwa na ukatoka bila dawa.
 
Last edited by a moderator:
Mpeleke kwa Daktari bingwa wa watoto Mkuu. Pengine anaweza kuwa na TB. Usipoteze muda.
 
Pole kwa tatizo hilo. Mimi pia nilishapata tatizo kama hilo kwa watoto wangu. Dactari mmoja akaniandikia dawa kama kawaida na kunishauri niwe nawachanganyia Asali mbichi na Limau niwape kadri niwezavyo huku wanakunywa dozi yao aliyowapa.

Huu ni mwaka wa 10 sasa hajaumwa tena kikohozi cha namna hiyo. Hivyo jaribu kumpa Asali na Limao nyingi kadri uwezavyo lakini usiache kumpa dozi ya hospital kama ameandikiwa.
 
Asali ya nyuki wadogo kijiko cha chakula kimoja, changanya na punje 5 za kitunguu swaumu kilichotwangwa then mpe. Fanya hivyo mara 3 kwa siku.
 
UPOPO

Mpendwa naanza kupata picha kwamba limao+asali+vitunguu swaumu. Shukrani sana ndugu.
 
Last edited by a moderator:
Anatumia maziwa gani? kama ya ngombe simamisha mpe ya soya!kama ya unga badilisha!chunguza na vyakula anavyokula kila siku ubadilishe!Asali nyuki wadogo changanya na tangawizi mbichi iliyosagwa chemsha kwa muda mfupi kisha mpe mtoto asubuhi na jioni kijiko cha chai
 
kitu athma kwetu sijawahi ona labda kwa wale ma babu kizaa babu siwezi jua.

ok,anaweza kua na allergy. Plz mpeleke hospitali akafanyiwe full blood picture na allergy test ili mjue. Inawezekana kuna chakula kinamletea hyo kikohozi.
 
ok,anaweza kua na allergy. Plz mpeleke hospitali akafanyiwe full blood picture na allergy test ili mjue. Inawezekana kuna chakula kinamletea hyo kikohozi.
Okey ndugu nadhani ngoja nianze na hilo then nifuatie hayo mengine. Nashukuru.
 
Nilisikiaga eti mtoto akikohoa sana na kikohozi hakitibiki ni kwamba ana kimeo. Sina uhakika na hilo
 
Hii imekuwa na matokeo mazuri sana kwa hali uliyoisema ya huyo mwanao 1.kata slace za Limao 2 (siyo ndimu) pamoja na maganda 2. Vitungu maji 2, 3. Vitungu saumu 2, 4. Tangawizi 2. Saga mchanganyiko huo kwa brenda au kinu
Chemsha mchanganyiko huo na lita 2 za maji safi mpaka upate uji mzito. Acha u poe then chuja then weka kwenye chombo safi, iweke kwenye fridge.

Chukua kijiko 1 cha chai cha asali changanya na vijiko 2 vya chai vya mchanganyiko huo mpe asubuhi mchana na jioni wiki moja pia ni kinga na hata watu wazima wanaweza kuitumia
 
mkuu mpaka nafika hapa ujue tayari nilishafanya kumpeleka hosptl ndio maana nahisi pengine dawa zinaweza kuja kumzuru. Kumbuka huwezi kufika hospital ukapimwa na ukatoka bila dawa.

sasa basi kama ni hivyo, inabidi mtoto aonwe na daktari bingwa wa watoto,

hivyo basi nenda hospitali hizi za halmashauri ya jiji au kwenye dispensaries za serikali hata private clinics, wakupe referral letter (barua kusema kuwa ugonjwa wa mtoto unahitaji utaalamu zaidi.

Muhimbili national hospital wana clinics za watoto utapewa tarehe yako.
kama mtoto ni mgonjwa sana (emergency case) basi moja kwa moja utafika pale emergency department na atalazwa wodini, na daktari bingwa huwa zamu kila siku, ataitwa kumuona mtoto.
 
Futota,

nilitaka kuuliza swali ila maelezo yako yamejibu maswali yangu yote.

Thanks
 
Back
Top Bottom