Ushauri - Mtaji wa Mradi wa Kufuga Kuku wa Kienyeji

Riwa

Platinum Member
Oct 11, 2007
2,607
3,065
Nina shamba la ukubwa wa hekari 4 katika kijiji cha Vikawe karibu na Mapinga Bagamoyo ambalo nimelisajili kwa hekari mbili mbili (yaani lina hati mbili), ambalo nataka kuanzisha mradi wa ufugaji kuku wa kienyeji (lakini kwa njia za kisasa). Nahitaji mtaji wa si chini ya Tshs 15m ikijumuisha kuweka mabanda na uzio.

Swali: Je, ninaweza kutumia hati hizo za umiliki ardhi hiyo kama bond kuweza kupata mkopo benki kwa ajili ya mradi huo? Kama jibu ni ndio, basi ni benki ipi/zipi hizo?
 
La mkopo sijui...........vipi kuhusu maarifa ya ufugaji hao kuku, kama wahitaji ujuzi tunaweza kushauriana.
 
Ninahitaji...nimeshaperuzi thread nyingi tu humu JF zinazozungumzia masuala ya ufugaji, nimepata elimu ya kutosha lakini pia nitahitaji msaada wa kitaalamu kudesign mradi mzima. Nimeona contacts za Consultants wanaotoa msaada huo, na naplan kuwasiliana nao iwapo nitapata uwezekano wa kusecure loan kwa ajili ya huo mradi.

Naitahitaji ujuzi wako pia. PM.
 
  • Thanks
Reactions: ABB
Bank nyingi hazitoi mikopo ya ufugaji ila jaribu TIB kwenye dawati la Kilimo Kwanza. Majibu utakayopata tushirikishane kaka.
 
Bank nyingi hazitoi mikopo ya ufugaji ila jaribu TIB kwenye dawati la Kilimo Kwanza. Majibu utakayopata tushirikishane kaka.

Kama utaenda TIB ujiandae kuweka uvumilivu na stress.. maana inaweza ikakuchukua miaka 3 mpka 5 kufanikisha kupata loan pale. TIB sijui wapo kwa ajili ya nani ila wako wanaurasimu wa hali ya juu sana mpaka wakupatie loan..hata zile disbursements hawatoi kwa wakati, wakati miradi ya kilimo unatakiwa uwe makini sana kwenye timing..
 
Nina shamba la ukubwa wa hekari 4 katika kijiji cha Vikawe karibu na Mapinga Bagamoyo ambalo nimelisajili kwa hekari mbili mbili (yaani lina hati mbili), ambalo nataka kuanzisha mradi wa ufugaji kuku wa kienyeji (lakini kwa njia za kisasa). Nahitaji mtaji wa si chini ya Tshs 15m ikijumuisha kuweka mabanda na uzio.

Swali: Je, ninaweza kutumia hati hizo za umiliki ardhi hiyo kama bond kuweza kupata mkopo benki kwa ajili ya mradi huo? Kama jibu ni ndio, basi ni benki ipi/zipi hizo?

hebu jaribu kwenda offisi za sido wanatoa hi mikopo ya ujasilia mali wakati mwingine unapewa jumla si mkopo kuna wafadhili pale nusanusa upate the right personal
 
Re: Ushauri - Mtaji wa Kufuga Kuku wa Kienyeji.
Hebu nenda pale kanisani Mikocheni B - Mama Lwakatare, wana programu ya kusaidia wajasiriamali kama wewe na wanatoa mafunzo na mikopo au wasikilize kila Jumamosi saa 3-4 asubuhi Praise Power Radio wana kipindi chao kinaweza kuwa enlightener kwenye issue hii. WAONE THEN GIVE US FEEDBACK!
ALL THE BEST!
 
Ahsante kwa michango yenu wandugu, nitaifanyia kazi. Sehemu nilizojaribu so far zinaonyesha kwamba si kazi rahisi kupata loan kwa ajili miradi ya kilimo na ufugaji, hata mradi wako uwe umechrwa perfect vipi.
 
I hope utapata right place kukopa. Ila epuka kukopa kwa watu kama wakina Papaa Msofe.
Kila la heri kwenye biashara yako.
 
Mkuu,
ni wazo zuri sana la kijasiriamali. Andaadodoso lako kisha uende pale DSE (Dar Stock Exchange) nilimsikia mkurugenzi wao akiongea kwenye media kwamba wanatoa mikopo tena yenye riba nafuu kuliko bank. Na alit
abainisha kwamba Bank nyingi zinakopa fedha ambazo zinakwenda kutumika kama mikopo kwa watu.

Mkuu hii ilikuwa ni two yrs ago naamini policy haijabadilika na kibaya tunahofia sana kujaribu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom