Ushauri: Meshack Nzowa wa MagicFM jiandae kabla ya kufanya kipindi

Uswe

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,204
626
Katika hali ya kusikitisha na kuonyesha jinsi gani bwana Meshack Nzowa hajiandai kabla ya kufanya kipindi, leo katika show yao ya asubuhi ameongea vitu vinavyopotosha watu na hivyo kushusha hadhi ya redio yao.

Moja, akiongelea ni kwa nini matumizi ya nyavu ndogo hayaruhusiwi kwa uvuvi bwana nzowa amesema ni kwa sababu zile nyavu zinaweza kuwaponyoka wavuvi kutokana na udogo wake, na zikiwaponyoka inakua ngumu kuzipata, ukweli ni kwamba udogo wa nyavu unaoongelewa ni wa matundu, kwa hiyo kutumia nyavu zenye matundu madogo kunasababisha kuvua samaki wadogo ambao wanatakiwa waachwe wakue.

Mbili
, akiongea kwa uhakika kabisa anasema alimsikia Job Ndugai akimwambia halima mdee 'unawashwawashwa nini?' akasisitiza kwamba eti yeye kwa macho yake alimuona ndugai akipeana mikono na halima mara baada ya bunge kwisha, Ukweli ni kwamba kauli hiyo ilitoka kwa mabuba na sio kwa ndugai, na aliambiwa mnyika na sio Halima mdee.

Ushauri Wangu: Mtu akisilikiliza inam-put off sana, jitahidi kufanya home yako kabla ya kwenda kwenye kipindi.
 
kuweka kumbukumbu sawa hiyo ya job ndugai kwa halima ni kweli kbsa huyo mtangazaji hajakose,ndugai alimwambia halima na si mabumba kama unavosema wewe.
 
Ndugai alitumia neno "kituko" kwa Halima
Mabumba alitumia neno "unawashwawashwa" kwa Mnyika
 
Mbona ni juzi tu Jaslaws, inawezekana umeshahau mara hii?

Ndugai alitumia neno "kituko" kwa Halima
Mabumba alitumia neno "unawashwawashwa" kwa Mnyika

Asante kwa kuweka rekodi vizuri chief
 
Heri ya Meshack Nzowa ana afadhali na akili timamu kuliko Gerard Hando wa radio ya wafu anayefanya mambo kama kichaa. Ni vizuri kumkosoa mtu akikosea bahati mbaya kama Nzowa but Hando anakosea makusudi na kujifanya insane. All in all waandishi wa nchi hii ni wavivu sana kujisomea, amazingly hawajui mambo mengi sana.
 
Mimi nadhani Meshack Nzowa anafaa kuwa kwenye comedy group kuliko mtangazaji wa redio maana hata kunajadiliwa hoja za maana yeye analeta jokes,pia hata uwezo wa kuipangilia mada na kuijadili sawia hana.
 
....... All in all waandishi wa nchi hii ni wavivu sana kujisomea, amazingly hawajui mambo mengi sana.

hiki kitu hata mie nime-note hasa kwa presenters, mambo mengi sana huwa hawajui, sijui ni u-busy wanashindwa kufatilia au sijui ni nini!

sasa we mtu anasema nyavu ndogo zimepigwa marufuku eti kwa wababu zinawaponyoka wavuvi kirahisi, afu yuko serious kabisa
 
Katika hali ya kusikitisha na kuonyesha jinsi gani bwana Meshack Nzowa hajiandai kabla ya kufanya kipindi, leo katika show yao ya asubuhi ameongea vitu vinavyopotosha watu na hivyo kushusha hadhi ya redio yao.

Moja, akiongelea ni kwa nini matumizi ya nyavu ndogo hayaruhusiwi kwa uvuvi bwana nzowa amesema ni kwa sababu zile nyavu zinaweza kuwaponyoka wavuvi kutokana na udogo wake, na zikiwaponyoka inakua ngumu kuzipata, ukweli ni kwamba udogo wa nyavu unaoongelewa ni wa matundu, kwa hiyo kutumia nyavu zenye matundu madogo kunasababisha kuvua samaki wadogo ambao wanatakiwa waachwe wakue.

Mbili
, akiongea kwa uhakika kabisa anasema alimsikia Job Ndugai akimwambia halima mdee 'unawashwawashwa nini?' akasisitiza kwamba eti yeye kwa macho yake alimuona ndugai akipeana mikono na halima mara baada ya bunge kwisha, Ukweli ni kwamba kauli hiyo ilitoka kwa mabuba na sio kwa ndugai, na aliambiwa mnyika na sio Halima mdee.

Ushauri Wangu: Mtu akisilikiliza inam-put off sana, jitahidi kufanya home yako kabla ya kwenda kwenye kipindi.

Haya ndio matatizo ya kuajiri watu bila shule.
 
Hawa watangazaji uwezo wao kwa kweli ni mdogo sana...nadhani nje ya studio hawasomi kitu chochote wala kusikiliza hata radio za nje. Huyo Nzowa amekariri kile kipande kabla ya kuanza kusoma magazeti utamsikia ''Tutaanzia kurasa wa mbele kisha wa kwanza hadi wa nne kama kutakuwa na mwendelezo kutoka ukurasa wa kwanza, baada ya hapo tutayageuza magazeti hayo kuangalia ukurasa wa mwisho kwa habari za burudani na michezo'' hii lazima aseme kila siku kwa mpangilio huu huuu.!!!!!!!!!
 
hahahaaaaa!

baadhi ya watangazaji ninaowaheshimu sana kwa kazi zao

  1. Masoud Kipanya (wa timesfm) - huyu jamaa anajua sana!
  2. Anorld Kayanda (wa clouds)
  3. Fina Mango (wa magic)
  4. Sebo (wa magic)
  5. Michael (wa magic)
  6. Fadhili Haule (wa capital radio)

kibwana dachi ni mtangazaji mzuri na huwa ana data kibao na anajisomea na kujishughulisha sana juu ya habari ...hawa wengine kazi yao ni kupaka rangi upepo
 
yaani hapo nakuunga mkono kwa asilibuku (1000%), huwa nafungulia magic pale ninapojua sasa ni muda wa kibwana dachi kuongea, wengine ni uvundo mtupu!
 
kuweka kumbukumbu sawa hiyo ya job ndugai kwa halima ni kweli kbsa huyo mtangazaji hajakose,ndugai alimwambia halima na si mabumba kama unavosema wewe.
Msiwe mnakurupuka kuongea maswala msiyoyajua,
Mabumba alimwambia mnyika kuwa anawashwawashwa,
Ndungai alimwambia mdee kuwa "wapiga kura wananuona kituko".
Nikirudi kwa huyo mtangazaji inadhihirisha kuwa alikua anadhani anasikilizwa na watoto wake pekee bila kujua kuwa sio watanzania wote wenye vichwa panzi.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Msiwe mnakurupuka kuongea maswala msiyoyajua,
Mabumba alimwambia mnyika kuwa anawashwawashwa,
Ndungai alimwambia mdee kuwa "wapiga kura wanamuona kituko".
Nikirudi kwa huyo mtangazaji inadhihirisha kuwa alikua anadhani anasikilizwa na watoto wake pekee bila kujua kuwa sio watanzania wote wenye vichwa panzi.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
wengi wanapata kazi kimagumashi kwa kuwa wamilik waredio kuwaanjiri wenye taalauma na kuwapa maslahi stahili n kazi,kujua kuongea haikufanyi kuwa mtangazaji mzuri kama uwezo wa kuchambua na kueleza mambo n ziro sie yy karibia redia kibao tu
 
Wasikilizeni na watangazaji wa PRAISE POWER FM ile radio ya mama mbeba maono wanaotangaza kipindi cha magazetini saa 07:30AM mpate uhondo yani kama walifika la 12 Darasa bac kazi ipo
 
Tatizo ni kwamba watangazaji wetu wanadhani wote wanaowasikiliza ni watu wa hovyo
 
Back
Top Bottom