Ushauri; matumizi sahihi ya laptop

Prince Nadheem

JF-Expert Member
Feb 25, 2012
1,253
1,028
Habari za kazi wanjamii?? jamani mwenzenu nilinunua ka laptop kangu kapyaa ni hp 635 kama miezi 7 iliyopita,sasa kuna kama vitu 2 nilikuwa naomba msaada kiushauri wenu maana huku ndio kimbilio letu watu kama sisi.
Ishu yenyewe ni hivi;
1. kwanza hivi karibuni kama wiki hivi mashine imekuwa ikiheat upande wa kushoto ambapo ndio kuna mashine yenyewe tofauti na mwanzo wakati bado mupya kwani ilikuwa hata iwashwe siku nzima kitu baridii na hata mvuke wa feni ya pembeni ulikuwa ni wa baridii kama wa AC ila sasa hali ni tofauti kwani kila sehemu linatoka joto sasa. Je hali hii ni sawa?
2. Pili katika matumizi yake ni njia ipi iliyokuwa sahihi kwa matumizi kati ya kuweka katika umeme muda wote hata pale betri inapokuwa full kwa maana ya kwamba betri lipo designed for emergence use pekeake au kila mara betri likijaa unatakiwa ku unplug from the power source ndio matumizi mengine yaendelee?? tafadhali mchango chanya wenu unahusika sana hapa katika kutimiza ile falsafa ya kitunze kidumu.


 
jaman wale wa IT kazi kwenu me nitakusadia la kwanza ni hivi kama inaheat tatizo litakuwa kwenye prosesa
 
Hakuna haja ya kuichomoa betri ikijaa, zimetengenezwa kujua hilo, ikiwa imechomekwa inatumia umeme wa kawaida na betri inapojaa inaacha kucharge betri.

Tumia betri wakati hauna umeme wa kamawaida.

Kuhusu joto, itakuwa imejaa vumbi chukua mrija kisha puliza kwenye matundu ya feni uone kama vumbi linatoka na kama joto linapungua, au feni imepata matatizo au unatumia programs ambazo zinatumia sana CPU.
 
Back
Top Bottom