Ushauri kwa rais

Tongue blister

JF-Expert Member
Jun 19, 2009
362
11
Kwa mara ya kwanza ni ngependa kutoa ushauri kwa wale washauri wa Rais wetu.
Nimetafakari kwa muda mrefu, Kutokana na misukosuko mingi iliyopo ndani ya nchi yetu kwa sasa,tukianzia katika swala la kuanguka kwa Uchumi wa Tanzania, Maswala mbali mbali yahusushwayo na Ufisadi, Mifarakano kati ya viongozi ndani ya chama Tawala na mengine mengi yenye kufanana na hayo.

Kimsingi Rais wetu hana sababu ya kujiuzuru kama wasemavyo walio wengi kutokana na anguko kubwa la kiutawala ndani ya nchi yetu bali naloweza kuwashauri washauri wa Rais wetu ni kulitazama anguko hili kwa miaka mingine 5 ijayo.

Kipindi cha Urais cha awamu ya pili ianzayo 2010 hadi 2015 Rais wetu tungemshauri kutokuchukua form za kugombea nafasi hiyo na kujaribu kuwapisha wengine kutokana na hali halisi ya kisiasa ndani ya chama hicho na Tanzania kwa ujumla.

Na kwakutokuchukua form haimaanishi tu kwamba Rais wetu kashindwa kuliongoza Taifa bali yawezekana uongozi wake umeshindwa kukidhi matakwa ya waliomchagua ambao ni watanzania.

Kwa sasa imedhihirika wazi kabisa kwamba Tanzania inahitaji viongozi walio wasomi , viongozi walio wawazi, Viongozi wenye kufuata maadiri ya kitanzania na wenye uwezo wa kuyasikiliza na kuyatatua matatizo ya watanzania. Kitu ambacho ni tofauti kabisa kwa Uongozi tulio nao kwasasa.

Ukijaribu kutafakari kwa kina utaweza kugundua kabisa kwamba Kile kipindi cha Watanzania GIZA kimepita , Tanzania imekuwa na wasomi wengi wengi kabisa ndani na nje ya nchi wenye uwezo mkubwa wa kuchambua maswala mbali mbali yakiwemo maswala ya Kisiasa na utawala bora , Watanzania walio wengi kwa njia moja au nyingine wameweza kuzitambua haki zao kupitia vyombo vya habari ndani na nje ya nchi. Watanzania wengi wamekuwa wakipata habari za ndani ya nchi kwa kuambizana pia.

Kwa misingi hiyo na mingine, Awamu ijayo ya Uongozi haitakuwa lele mama ya mpeni kula Rais. Itakuwa ni Awamu yenye kuhitaji kiongozi jasiri,Muwazi ,mwenye kuipenda nchi yake, kiongozi asiye mbinafsi ,mwenye kusikiliza matatizo ya watanzania ,kiongozi mwenye uwezo wa Kubuni na kuzitafakari njia zenye kuleta maendeleo na kuamsha uchumi wa Watanzania kwa msaada wa Watanzania.

Pasipo Msaada kutoka kwa wananchi wa Kitanzania ni vigumu kabisa kabisa kuliongoza Taifa hili kubwa lenye mshikamano na amani.


Imeandikwa: Nanukuu !!! SIMAMA UKAITENDE SHUGHULI HII YAKUHUSU WEWE, UWE NA MOYO MKUU KWA MAANA MUNGU YU PAMOJA NAWE..!!
 
Tongue blister,
Unaposema Tanzania inahitaji viongozi walio Wasomi nadhani unamainisha Wenye Shahada za juu. Kwa hiyo wasio na shahada hizo au za kiwango hicho hawana HAKI ya kuwa vingozi?? Kumbuka tuko milioni 40 give or take, na nusu yawezekana kuwa Watoto, na hiyo nusu ya wakubwa Ikawa Ngumbaro au Walioishia Darasa la Saba. Bado utoe Wenye shahada wanaostahili kuongoza,kutoka katika Robo iliyobaki Naamini utakuwa umetujengea Tabaka jipya na la HATARI SANA.
 
Tongue blister,
Unaposema Tanzania inahitaji viongozi walio Wasomi nadhani unamainisha Wenye Shahada za juu.

Mkuu Nadhani sijatamka Degree au shahada za juu, Nimetamka wasomi nikimaanisha hata Darasa la saba ni usomi. Sasa kama waona yawezekana kuwa kiongozi kwa Elimu hiyo uitakayo wewe it´s OK.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom