Ushauri kwa KIKWETE na NEC/ Makame

Tusiwe manabii wa uongo kama Shehe Yahya, tusubiri matokeo yatangazwe, na kisha matamko ya Dr Slaa na Kikwete yatoke. Kuna uwezekano tamko la Kikwete au Dr Slaa ku-trigger mambo makubwa sana katika nchi. Endeleeni kuombea nchi, hali bado sio shwari.

Kuhusu NEC na CCM
Si kila mara unaweza kufanya dhuluma katika kura za uchaguzi na kupeta. Dhuluma hujenga chuki, na chuki inayotokana na uchaguzi huwa si ndogo kwasababu inahusu watu wengi kwa pamoja. Chuki ya uchaguzi inaweza kuleta maamuzi ya ghadhabu kali ya watu wengi.

Lakini pia huwqezi kutawala watu ambao hawakupendi na walishakukataa katika mioyo yao. Hutapita salama mitaani mwao, na ukipita watakusengenya na kukuzomea. Afadhali wakiishia kuzomea na kusengenya na omba isiwe zaidi ya hapo.

Tamko la Dr Slaa linaweza kuifanya nchi kutengwa na jamii ya kimataifa, tunaweza kufika kwenye hali ya Zimbabwe kiuchumi na mahusiano ya kimataifa. Kikwete hataweza kutawala kwa amani, utulivu na ustawi katika nchi yetu tena.

Tusubiri tuone...

Sungura
 
Wazushi wote wasio ona uchafu unaochezwa . miondo mbinu dar unalinganisha na kijijini ? wapi hadhi ya jiji? waache hizo .
 
Back
Top Bottom