Ushauri kwa Dr. Steven Ulimboka

OLEWAO

Member
Jan 27, 2012
89
78
Wana JF,

Nimefikiria sana juu ya mustakabali wa Dr. Ulimboka mara Mungu atakapomjalia afya njema na akarejea nyumbani.

Japo sijui msimamo wake binafsi na familia yake, reaction ya serikali (badala ya kujibu hoja) ya KULIFUNGIA KWA MUDA USIOJULIKANA GAZETI LA MWANAHALISI lililofichua mpango mzima (na wahusika wakuu) wa kukamatwa kwake,kuteswa na hatimaye kutupwa katika msitu wa pande wakidhani angekufa tu kunadhihirisha mambo mawili makubwa.

Mosi serikali ndiyo iliyohusika na unyama aliofanyiwa Ulimboka;

La pili, kwakuwa hajafa till now,hayuko salama.

Ushauri:

Hukohuko aliko,arejee maelezo yake juu ya unyama aliofanyiwa kwa undani na ufasaha na yahifadhiwe kwenye formats mbalimbali na yasambazwe kwenye vyombo vyote vya habari (vya ndani na nje) kwa ajili ya kumbukumbu. Na mara tu atakaporejea nyumbani afanye press conference juu ya tukio lake na pia kutangaza kuacha kazi serikalini.

Kama anaweza siasa ajiunge na chama cha upinzani. Kwenye uchaguzi ujao atapata kura za kishujaa.

Wana JF mnasemaje?
 
Mkuu dr ulimboka, afanyi kazi serikalin! Alafu pili yule ni professional dr, sio madokta wakuiba iba, ivyo haitakuwa busara kuwa mwansiasa ni mapema mno, tena akienda huko kwenye siasa ni sawa na kumkabidhi paka samaki akulindie, yani hato chukua hata siku 1,watu wanatangaza msiba.
 
Ushauri wako ni dhaifu sana...sijui pia msingi wa ushauri wako ni nini.
 
Ulimboka yupo kwenye shinikizo kubwa now kuliko hata alipokamatwa na kufanyiwa ufedhuli. Msukumo wa maamuzi yake ukitokana na woga ataishi maisha ya taabu sana ila akifanya maamuzi bila woga na kuamua litakalo kuwa na liwe ataishi kama shujaa kwasababu atapambana na litakalotokea na litamjengea confidence yakupambana na mengine.

Waliomfanyia unyama ule wapo hai na wanabackup kubwa ila wote ni binadamu wana mwili na damu as it has been said what's goes around comes around.
 
Kwanza ni upotoshaji kudai ni mtumishi wa serikali. Lakini anatakiwa atakapopata afya njema, nasi tunamuombea, afikishwe mahakamani na ajibu mashitaka ya uhujumu uchumi na mauaji ya raia wasio na hatia. Halafu afunguliwe mashitaka kwa kuisingizia na kuidhalilisha serikali wakati kinachoitwa unyama kimefanywa kwa mambo yake binafsi.
 
  • Thanks
Reactions: MI6
Kwani kuna jipya la kusikia kutoka kwa uli?si alitekwa,akateswa na kutupwa pande na mtu anaedai anaitwa rama wa ikulu,KUNA JIPYA GANI TENA?
Au wakati wanamteka walikua wanamhadithia na life history zao na za family zao?.
Yaani jinsi watu wanavyospin hii issue utadhani ni bonge la issue.
 
Hawezi itisha press conference coz swala lipo mahakamni,pili afanyi kazi serikalini.
 
Kwanza ni upotoshaji kudai ni mtumishi wa serikali. Lakini anatakiwa atakapopata afya njema, nasi tunamuombea, afikishwe mahakamani na ajibu mashitaka ya uhujumu uchumi na mauaji ya raia wasio na hatia. Halafu afunguliwe mashitaka kwa kuisingizia na kuidhalilisha serikali wakati kinachoitwa unyama kimefanywa kwa mambo yake binafsi.
hii ya kwako ni kali mkuu wangu,hata MKUU WA MAFIA hakutumia lugha kali hivi kukanusha kitendo!
 
ulimboka ana akili za kushinda mauti.naamini anajua the way foward.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Ahsante kwa kunisahihisha. Edson ushauri wako please!atakaporejea nchini afanyeje?
 
Kwani kuna jipya la kusikia kutoka kwa uli?si alitekwa,akateswa na kutupwa pande na mtu anaedai anaitwa rama wa ikulu,KUNA JIPYA GANI TENA?
Au wakati wanamteka walikua wanamhadithia na life history zao na za family zao?.
Yaani jinsi watu wanavyospin hii issue utadhani ni bonge la issue.

Mhhhh! hilo jina lako nikimkumbuka na Elungata kwenye vitabu vya Kipelelezi vya Musiba nadhani kikosi cha kisasi UNANITISHA!!!!
 
Namshauri asirudi bongo atafute maisha kwingine na asahau na kusamehe yote yaliyotokea kwa sababu asitegemee haki kutendeka
 
Kwanza ni upotoshaji kudai ni mtumishi wa serikali. Lakini anatakiwa atakapopata afya njema, nasi tunamuombea, afikishwe mahakamani na ajibu mashitaka ya uhujumu uchumi na mauaji ya raia wasio na hatia. Halafu afunguliwe mashitaka kwa kuisingizia na kuidhalilisha serikali wakati kinachoitwa unyama kimefanywa kwa mambo yake binafsi.
Ooooops you have way to irritate. I can see why people in Libya could sodomise Ghadafi with a knife. It is obvious because Ghadafi was thinking differently from the people. Trust me you fit that profile..the question will be is it worth it when it comes to you? Remember what comes around goes around.
 
Wakuu JF,
Nimetafuta katika hazina yangu ya busara nimeshindwa kupata ushajri kwa Dr Ulimboka pindi akitua TZ. Siwezi kukosa ukoko hata hivyo, Napenda kumshauri Ulimboka akitua bongo asisikilize hasira ama jazba akae akijua kunusurika kwake haikuwa ajali ama good fortune. Ajue Ulimboka kwamba kila kona na kila mtu yuko na shauku kumsikiliza hasa wote wakitarajia atoe ukweli halisi ili kupigilia msumari wa mwisho ktk jeneza la Police wetu. Dr awe na busara atende yote kuilinda roho yake ama sivyo atakuwa footnote kwenye Tanzania patriotic era. Kukomoana na dola utaumia wewe, Watanzania watakusifu vijiweni tuna baada ya miaka miwili you are done my comrade. Hakuna vipuri vya uhai ila kila mtu anao uhuru wa kujilunda na kuitetea nafsi yake. Mpumbavu hunena ila mwenye busara hufikiri, hakuna atakayemlaumu Ulimboka ila wapo watakaomshangaa Ulimboka. Serikali inajua iendapo ila waumini hatujui uelekeo wetu, Ulimboka awe na busara akajue maana ya mafumbo haya.

GKassanga
Tabora.
Wana JF,

Nimefikiria sana juu ya mustakabali wa Dr. Ulimboka mara Mungu atakapomjalia afya njema na akarejea nyumbani.

Japo sijui msimamo wake binafsi na familia yake, reaction ya serikali (badala ya kujibu hoja) ya KULIFUNGIA KWA MUDA USIOJULIKANA GAZETI LA MWANAHALISI lililofichua mpango mzima (na wahusika wakuu) wa kukamatwa kwake,kuteswa na hatimaye kutupwa katika msitu wa pande wakidhani angekufa tu kunadhihirisha mambo mawili makubwa.

Mosi serikali ndiyo iliyohusika na unyama aliofanyiwa Ulimboka;

La pili, kwakuwa hajafa till now,hayuko salama.

Ushauri:

Hukohuko aliko,arejee maelezo yake juu ya unyama aliofanyiwa kwa undani na ufasaha na yahifadhiwe kwenye formats mbalimbali na yasambazwe kwenye vyombo vyote vya habari (vya ndani na nje) kwa ajili ya kumbukumbu. Na mara tu atakaporejea nyumbani afanye press conference juu ya tukio lake na pia kutangaza kuacha kazi serikalini.

Kama anaweza siasa ajiunge na chama cha upinzani. Kwenye uchaguzi ujao atapata kura za kishujaa.

Wana JF mnasemaje?
 
Kwanza ni upotoshaji kudai ni mtumishi wa serikali. Lakini anatakiwa atakapopata afya njema, nasi tunamuombea, afikishwe mahakamani na ajibu mashitaka ya uhujumu uchumi na mauaji ya raia wasio na hatia. Halafu afunguliwe mashitaka kwa kuisingizia na kuidhalilisha serikali wakati kinachoitwa unyama kimefanywa kwa mambo yake binafsi.
Kwanza sheria za uhujumu uchumi zilishafutwa na akina Chenge enzi za Mkapa. Waliosababisha mauaji ya raia ni watawala elitists ambao wanajipangia mishahara mikubwa na marupurupu bila kujali kama hospitali zetu zina vifaa vya kutosha na madaktari wanafanya kazi katika hali gani. Sote tunajua serikali ya Kikwete ina umafia. Jibuni kwanza shutuma zilizotolewa na Mwanahalisi ndipo tujue kama kweli serikali imezingiziwa na kudhalilishwa. Kuna mtu kataja hapa mfano wa Gadafi na Mkuu wa Mafia. Serikali yenu is not too far from that truth.
 
Mbona unaumiza kichwa mzee, wewe muombee apone vizuri arudi nyumbani halafu yeye ndo ataamua, aongee au asiongee. Yeye ndo anajua cha kusema na cha kuacha kusema!
 
Mhhhh! hilo jina lako nikimkumbuka na Elungata kwenye vitabu vya Kipelelezi vya Musiba nadhani kikosi cha kisasi UNANITISHA!!!!
just a name i liked,ukichukulia kitabu cha KIKOMO ni moja ya vitabu vya mwanzo kabisa kuvisoma katika uhai wangu na nilikua darasa la tatu.
 
Back
Top Bottom