Ushauri kwa Dr. Steven Ulimboka: Usifanye kosa la "Kukuingiza kaburini"

OLEWAO

Member
Jan 27, 2012
89
78
Baada ya kurejea toka Afrika kusini alikokuwa anatibiwa baada ya kufanyiwa unyama na watu wa TISS,Ulimboka anataka kufanya kile waingereza wanachoamini kuwa ni sawa na Grave mistake. Niliwahi kushauri siku chache kabla hajarejea kuwa mara atakapotua tu uwanja wa ndege wa JKNIA atuambie kwa ufasaha wale waliomteka na kumtesa. Kitendo cha kuendelea kukaa kimya hakiwezi kumuacha salama. Iwe ametishwa,amehongwa ama ameogopa yeye mwenyewe. Jambo moja litakalomtokea kwa yeye kuendelea kukaa kimya ni kuuawa. Ajue kila kukicha majitu ya TISS yanapanga namna ya kummaliza. Kama anafikiri natania akaulize kilichomtokea mkosoaji mashuhuri wa Kenya wakati wa utawala wa Moi ambapo baada ya mitego mingi ya kumuua kugonga mwamba alitekwa na watu wa usalama, akauawa na hatimaye kumwagiwa acid mwili mzima na kutupwa msituni. Aliokotwa na wawindaji ambao walitoa taarifa polisi na mwili wake kupelekwa mochwari. Wakati mhudumu wa mochwari akiuandaa mwili wa marehemu alikuta kitambulisho na ndipo alipogundua kuwa alikuwa ni Muruiki ambaye siku chache alikuwa amepotea. Mhudumu yule alituma sms kwa mmoja wa wabunge wa upinzani wakati bunge likiendelea. Moto uliwaka katika bunge la Kenya. Mpaka leo Muruiki ni marehemu na hakuna aliyekamatwa.

Ulimboka, Don'nt do what the British call as Grave Mistake. Usiposema sasa utakufa hakika. Tafakari.
 
Sure, ili asalimike hana budi kuweza a,b,c za utekaji wake full detailed. Awataje kwa majina watu wa TISS waliohusika. Akiendelea kukaa kimya kuzimu inamwita, maana akina rama watamuwinda wamuangamize kuhofia kutajwa. Pili lazima atoe tamko la kutomtambua mkenya wa gwajima. Silence is the best enermy.
 
Azungumze mara ngapi? Kwani aliyozungumza youtube hayatoshi? Me naona kamaliza kila kitu kwenye mahojiano ya mara ya kwanza, ambayo Mwanahalisi waliyachapisha, lakini hakuna jipya lililoendelea zaidi ya kulifungia gazeti.. Tusiwe wavivu tutafute mahojiano kwenye mtandao wa youtube.. Dr Ulimboka kafunguka mambo yote..
 
Mwacheni apumzike wala hawatamfuata tatizo ni mashabiki wake, utafikiri kucheza huo mpira wanauweza, km ni Filamu ilishaisha mambo ya kurudia nyuma ni kutafuta nani ana musuli kati ya tiss na yy wala sio MaDr tena
 
Ukwaju hiyo avatar yako inatisha ka nini!!!!!!!! Nikiiangalia nakosa amani naona kama waliomteka Dr Ulimboka wanafanana na avatar yako hiyo. Du! Mambo mengine bwana siyo!
 
Sure, ili asalimike hana budi kuweza a,b,c za utekaji wake full detailed. Awataje kwa majina watu wa TISS waliohusika. Akiendelea kukaa kimya kuzimu inamwita, maana akina rama watamuwinda wamuangamize kuhofia kutajwa. Pili lazima atoe tamko la kutomtambua mkenya wa gwajima. Silence is the best enermy.

Inamaana unataka amtaje Lema na wenzake? Maana ndio hao waliomteka.....kisha akishawataja muanze kumkana humu jamvini si ndio?
 
Mwacheni dokta wa watu apumzike... Hata ingekua ni mimi nisingesema kitu ningekaa kimya maana kwann niishi maisha ya taabu wakati madaktari aliokua anawatetea wote wameogopa wamerudi kazini? Chukua hela dokta pumzika
 
....Mpeni muda, atakapokuwa tayari basi atasema kila kitu kilichojiri na sidhani kama ataacha chochote alichofanyiwa na hii Serikali dhalimu.
 
nahisi kama ashaahidiwa mijisenti ya kumfunga mdomo vile
afu hatazila amalize kabla ya kumaliziwa kabisa
tumwache atafakari kama atazichukua ama la.
msiposikia kauli mjue mambo tayari keshazikamata
 
....Mpeni muda, atakapokuwa tayari basi atasema kila kitu kilichojiri na sidhani kama ataacha chochote alichofanyiwa na hii Serikali dhalimu.

Serikali dhalimu ama CHADEMA wauaji wasaka madaraka hata kwa damu za watu?
 
Jana niliota ndoto, eti kama vile watengeneza movie wanavyoweza kufanya, kukuonyesha mwili wa mguu wa Actor / Actress umeoza kwa kuumwa na nyoka wakati hakika ni mzima; basi hili tukio la Dr. Ulimboka, eti lilitafutiwa locations ( Leaders Club, Mabwepande, Muhimbili (nje & ICU) , Airport na South Africa) na Actions! Sasa eti mimi nilipomwona Dr. Ulimboka amerudi nikarukia mic na kumuuliza kwa sauti, “was it a staged stunt?” “Tell us the………”. Lakini, kabla ya kumalizia “motive behind” nikanyangánywa mic na kuzabwa kibao na mtu nisiye mjua. LOL nikashtuka kutoka usingizi!!
 
Sure, ili asalimike hana budi kuweza a,b,c za utekaji wake full detailed. Awataje kwa majina watu wa TISS waliohusika. Akiendelea kukaa kimya kuzimu inamwita, maana akina rama watamuwinda wamuangamize kuhofia kutajwa. Pili lazima atoe tamko la kutomtambua mkenya wa gwajima. Silence is the best enermy.
Ni kweli kabisa akina zomba, ritz na zemacopolo watamuangamiza muda si mrefu. Bora amwage hadharani kila kitu.
 
Hakika umenena tena huenda sasa akagongwa na gari kama sio kujumiwa majambazi nyumbani kwake. Usalama kwake ni pale atakapoweka mambo hadhalani kwakuwa atajiweka ktk ulinzi zaidi wa umma na serikali .
 
Similar Discussions

10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom