Ushauri kwa CHADEMA -- Ondoeni kansa (Zitto Kabwe) ili chama kisonge mbele

Ohh I know I know I know I know......

Wakati wa uchaguzi nilianzisha thread ya kusifia kazi ya Zitto. Yeah, ni kweli Zitto ni mwanasiasa machachari (kwa mujibu wa vyombo vya habari Tanzania), and yes, Zitto amekuwa mwanachadema tokea enzi za Kaburu (mwanachadema aliyehamia ccm).

Pamoja na kujua haya yote, nimefikia hitimisho kuwa Zitto ni kikwazo kikubwa sana cha maendeleo ya CHADEMA. Mara kwa mara, Zitto amekuwa anaua momentum za mageuzi Tanzania. Fuatilia yafuatayo kwa makini:

1. Zitto aliua momentum ya wapinga ufisadi nchini pale alipokubali kuingia kwenye tume ya raisi ya madini. Wabunge wengi (wakiwemo wa ccm) walitaka iundwe tume huru ya bunge ili ifanye kazi yake kwa uhuru bila mwingiliano wa serikali lakini Kikwete na mafisadi wenzake wakataka iundwe tume ya raisi (isiyokuwa na nguvu yoyote kisheria). Matokeo yake wote tunayajua.

--- issue ya buzwagi ilikufa
--- Andy Chande alijua mapendekezo ya tume ya madini kabla ya wabunge
--- Zitto alipata pesa za kutosha kununua hammer (maneno ya zitto haya)
--- Na kadhalika

2. Dowans ni beast linalokula mapesa ya watanzania. Wanachadema na watanzania wengi walianzisha movement ya kuvunja mkataba wa kipuuzi wa Dowans (trust me, this can be done). Wakati mambo yakiwa kwenye high time, Zitto kama kawaida yake, akaua momentum kwa press release yake kuwa Dowans lazima ilipwe pesa na serikali. Ingawa baadaye alikuja na bonge la u-turn kuwa anataka Dowans itaifishwe (what a schit), but wote tunajua kuwa ile momentum against dowans ilikufa right there.

--- Leo hii, Dowans iko mbioni kulipwa mabilioni ya pesa

3. Wakati kampeni za uchaguzi 2010 zimeanza, Zitto kama kawaida yake, alitaka kuleta vurugu la mwaka CHADEMA, pale alipotangaza kuwa anampango wa kugombea uraisi wa Tanzania 2015. Yeye mwenyewe amekiri kwa katiba ya sasa haimruhusu kugombea uraisi mwaka 2015 maana atakuwa hajafikisha miaka 40. Sasa kama sio ubinafsi, Why did he do that?

4. Baada ya NEC kuchakachua matokea ya uchaguzi nchi nzima na kumtangaza Kikwete kuwa mshindi wa uchaguzi. CHADEMA walifanya kitu kilichopelekea vyombo vya habari vingi duniani kutangaza mambo yanayoendelea kwenye bunge la Tanzania - kutoka nje wakati Kikwete akihutubia. Hii iliwapa CHADEMA mtaji mkubwa sana kisiasa. Nasikia hadi leo hii Kikwete amechanganyikiwa na haamini kilichotokea. Wakati hiyo movement ikiwa kwenye high motion, Zitto alifanya kile anachojua best - kuua momentum.

5. Zitto anadhani kuwa chama ni mtu mmoja. Yeye (na Omar Ilyasi) anajihesabu kama the only politician mwenye maamuzi bora ndani ya chadema. Kama ijulikanavyo, Chama ni mkusanyiko wa watu. Anachofanya Zitto, ni kuvunja mkusanyiko huo ili kumpa nafasi yeye binafsi kupata kile anachotaka.

----

Ningeandika mengi sana ila muda hautoshi. Hii mada haina uhusiano na mada zingine zote zinazoendelea hapa JF. Naomba sana mods muiache hapa yenyewe. Ikikosa wachangiaji, itakufa kifo cha kawaida cha JF - itaenda next page... and next ... and next.

Ushauri kwa chadema --- msiogope wapambe watasema nini, mfukuzeni Zitto sasa hivi ili mpate muda wa kutosha wa kujenga chama kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

Asanteni.
Mh! Wajameni!
 
Back
Top Bottom