Ushauri kwa CHADEMA mkoa wa Mwanza

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,761
71,145
Ninafurahiswa sana na vuguvugu la mageuzi ya kisiasa linaloongozwa na Chadema mkoani Mwanza. Na ninauhakika sio mimi pekee ila tupo wengi tuu.
Sina uhakika kuwa hiki nitakacho kusema kama tayari kuna mipango makini ambayo tayari inafanyiwa kazi.
Chadema ndio chama kinachoendesha serikali ya halmashauri ya jiji la Mwanza na kinapaswa kuwa na mahali(ofisi) safi,panapofikika kirahisi na penye nafasi ya kutosha kufanya uratibu wa shughuli za kila siku.
Tukirudi kwenye mada, ofisi ya Chadema mkoa iliyoko Nyamanoro kwa kweli haikidhi mahitaji na hadhi ya chama chenye wanachama wengi na kinachoongoza serikali ya jiji. Ofisi iko katika uchochoro.
Nashauri Chadema kwa mtaji wa rasilimali watu ilionao Mwanza, kabla hata haijajipanga kujenga ofisi yake inaweza kupanga nyumba yenye nafasi na hadhi yake na kulingana na bei za nyumba Mwanza wanaweza kupata nyumba ya kodi ya shilingi milioni tatu kwa mwaka.
Kwa niifahamuvyo Chadema Mwanza, wanachama wake na wapenzi wanao uwezo wa kukilipia chama chao kodi kwa harambee ya saa moja tuu.
Nawashauri viongozi walifikirie hilo kwani Chama sio mikakati ya mikutano ya hadhara tuu,bali ofisi za kuratibia shughuli nazo ni muhimu sana.
 
Ushauri mzuri viongozi muufanyie kazi.
Na ni muhimu kulifanyia kazi mapema maana hili wimbi la watu kwa maelfu kujiunga na chama lazima kuwe na sehemu inayokidhi shughuli za uratibu.
 
Hapo umenena kamanda, chadema ina umaarufu mkubwa mwanza; inapaswa kufunguliwa ofisi hapa nami nitachangia kwa kuwa mimi pia ni mkazi wa Mwanza
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom