futikamba
JF-Expert Member
- Jan 18, 2010
- 243
- 13
- Thread starter
- #21
Asanteni sana kwa michango yenu wadau. Kwa waliouliza kama huyu jamaa aliripoti polisi baada ya tukio, jibu ni ndio. Alifanya taratibu zote hadi kukabidhiwa mtoto. Huyu mwanamke alishuka kwenye dalala kabla ya mshkaji na kwa maelezo ya mshkaji, huyu mwanamke alipandia njiani gari ikiwa imejaa, akamwomba mshkaji ambebee mtoto coz ye alikaa siti ya mbele. Mwanamama ye akasimama nyuma. Kwa hali ya kawaida, yule mama alitakiwa kumchukua mtoto wake akishuka. Ila sasa mshkaji akajikuta anaenda na yule mtoto hadi kituoni kwake. Akamtafuta huyo mwanamke na hakumwona. Kaulizia watu waliokuwa karibu yake wakasema keshashuka! Na ukumbuke alikuwa amesimama nyuma wakati mtoto kapakatwa mbele, so wale abiria wenzake wa nyuma si rahisi wajue kama aliingia na mtoto. Story nd'o iko hivo..