Ushauri: Huyu mwanamke nimemzoea sana nitawezeje kuwa naye?

mzee wa misele

JF-Expert Member
May 17, 2015
366
46
Wakuu habarini,

Kuna mwanamke nimetokea kumpenda sana ila tumezoeana sana kama marafiki tu zaidi miaka minne ananiheshimu sana nifanyaje ili niweze kumpata awe mke wangu?

Naogopa anaweza kukata mawasiliano na mimi nikamkosa kabisa, namhitaji wakuu nifanyaje sitaki kumkosa?




 
Friendzone 101. Kama kweli mko karibu, utakuwa unajua ni washkaji wa aina gani wanamvutia, so jipime kama una-fit. Ama jitose tu regardless, kuliko kusubiri aje Mshkaji mwingine abebe mbele yako.
 
Anza kumpa nafasi ya girlfriend like outing.. kama kuna kitu unaweza kwenda double be with her ,.. mwalike kwako ataeleka tu
 
wakuu habarini, kuna mwanamke nimetokea kumpenda sana ila tumezoeana sana kama marafiki tu zaidi miaka minne ananiheshimu sana nifanyaje ili niweze kumpata hawe mke Wang , naogopa anaweza kukata mawasiliano na Mimi nikamkosa kabisa , namhitaji wakuu nifanyaje sitaki kumkosa

Usisubiri kuambiwa ni too late.
Jiongeze, show kwa vitendo. Toka nae sehem mbalimbali, hasa jion, au nyt.
Muulize ulize maswali ya mitego kuhusu kama mngekuwa kwa uhusiano angeonaje…? Then utagundua yy anakuchukuliaje.
Usimtongoze directly ili hata kama hana hisia nawew usiharibu urafiki wenu.
 
anza kumpa nafasi ya girlfriend like outing.. kama kuna kitu unaweza kwenda double be with her ,.. mwalike kwako ataeleka tu

Kwangu huwa anafika Mara kwa Mara ila amenizoea kama kaka nitafanyaje ili haisi nimevutiwa na yeye na hatujawahi zungumzia kuhusu mapenzi na ni mwanamke mwenye msimamo sana naisi nikimweleza ndo hata kanyaga tena kwangu
 
Jitose mkuu jilipue tu mwambi it have bee long time I need but I wose just killing myself in my soul heat and I wose sceard to tell you in 4 year has my friend but to day I fill to tell you that I need you in my beautiful life and you will be and your dream in my life bla bla bla bla nenda sasa.


swissme
 
Jitose mkuu jilipue tu mwambi it have bee long time I need but I wose just killing myself in my soul heat and I wose sceard to tell you in 4 year has my friend but to day I fill to tell you that I need you in my beautiful life and you will be and your dream in my life bla bla bla bla nenda sasa.


swissme

huwez kizungu tumia kiswahili utaeleweka. HUWEZ KIZUNGU
 
Mi naona bora ufunguke tu moja kwa moja, kwani naamini kama anakupenda anakupenda tu na atakupa jibu zuri, na kama hakupendi hakupendi tu na atakupa jibu baya au kuwa na wewe kinafiki na mwisho wa siku akaolewa na ampendaye. Outing na mambo mengine ni mazuri, lakini upendo wa dhati ni kitu cha pekee ndani ya mtu.

Hivyo usitafute mazingira ya kumlazimisha akupende, bali wewe funguka tu na kama anakupenda ni wako, halafu outing zitafuata na ndoa pia.
 
Mkuu enedelea hivyohivyo mpaka aoteshwe unampenda.....

Kaa hivyohivyo Ipo siku utamwona na mtu mwingine usiumie wee endelea kukaa kimya
Siku itafika ataolewa wee piga kimya tuu endelea kuweka mazoea hivyohivyo labda atakapoachika atakuja kwako

....na ujinga wako
 
mzee wa misele

Kama mmezoeana, hebu jaribu kuwa unapata muda wa kuwa nae maeneo yanayoashiria faragha. Na muwe na mazungumzo ya jumla tu ila ujaribu kugusia kuhusu mapenzi na mahusiano. Umsikilize mtazamo wake kuhusu mapenzi na mahusinao, je ana mtu katika maisha yake au na yeye yupo tu? Na nini mtazamo wake kuhusu ndoa na kadhalika. Yaani mruhusu afunguke, na wewe ufunguke. Kisha utajua kama mko kwenye ukurasa mmoja, au lah.

Angalizo: Kuna baadhi ya wanawake wanafaa sana kuwa naye katika urafiki wa kawaida tu. Pindi mkivuka mstari na kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi, mnajikuta mmefarakana ndani ya muda mfupi. Kwa hiyo uwe mwanagalifu kama kweli unataka kuingia katika uhusiano wa kimapenzi na yeye.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom