Ushamba: Simu za Gharama

DASA

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
1,031
301
Mi nafikiri lengo la kuwa na simu ni kuwa na uwezo wa kutuma ujumbe mfupi, uwezo wa kuwasiliana na mtu wa pili kwa haraka kwa ajili ya maongezi, labda tuweke na matumizi ya Internet ambapo unaweza kuhabarisha watu na kupata taarifa mbalimbali kama za hapa JF. Lakini mi point yangu ni kwaba kweli kuna ulazima wa kuwa na simu ya bei mbaya sana kuanzia laki 3 na kuendelea wakati unaweza kupata simu yenye hizo huduma zote kwa elfu 50 mpaka laki??, huu sio ushamba kweli!!, kinachofurahisha zaidi hao wanaotengeneza hizo simu wenyewe hata hawazitumii hizo za bei mbaya!!!,
Utakuuta mtu una simu ya milioni moja halafu anasema maisha magumu!!.
 
images


Unaona kitu hicho!!.
 
Si faida kama unanunua simu ya gharama halafu hata hujui kuitumia to its full potentials.

Katika dunia ya leo, ni vizuri ukanunua simu ile utakayo tumia katika shughuli zako za kimaendeleo. Kama huwezi kuitumia au huna kazi nayo na unataka uonekane tu kuwa una kifaa.............!!!!!!!!! Huo ni ulimbukeni...!!!
 
Huko unakoelekea mkuu ndo ile habari ya nini kuwa na wake wengi wakati kitu ni kile kile.Kwa hiyo mkuu jua binadamu tuko tofauti sana.Cha ajabu kwako kwa mwenzako poa sana.
 
Mi nafikiri lengo la kuwa na simu ni kuwa na uwezo wa kutuma ujumbe mfupi, uwezo wa kuwasiliana na mtu wa pili kwa haraka kwa ajili ya maongezi, labda tuweke na matumizi ya Internet ambapo unaweza kuhabarisha watu na kupata taarifa mbalimbali kama za hapa JF. Lakini mi point yangu ni kwaba kweli kuna ulazima wa kuwa na simu ya bei mbaya sana kuanzia laki 3 na kuendelea wakati unaweza kupata simu yenye hizo huduma zote kwa elfu 50 mpaka laki??, huu sio ushamba kweli!!, kinachofurahisha zaidi hao wanaotengeneza hizo simu wenyewe hata hawazitumii hizo za bei mbaya!!!,
Utakuuta mtu una simu ya milioni moja halafu anasema maisha magumu!!.

Basically matumizi ya simu ni hayo uloyataja ila yapo mengine mengi kama GPS,COMPASS,ENTERTAINMENT na services nyingine kibao kutegemea na aina ya simu na Apps zilizomo.Hata hivyo nakubaliana nawe ni ulimbukeni kununua simu expensive wakati wewe bado ni hohehahe,mlo wa mchana unapata kwa shemeji,hata chumba hauwezi kupanga bado unalala sebuleni kwa kaka yako,hata naiuli ya daladala wapewa na mjomba...ila siku ukiotea milioni eti yote unanunulia simu baadae unanitafta mimi nikutoe hela ya kununua jeans..weweeeee...:mad: Wale mliojiimarisha kiuchumi sina shida na ninyi,nunua hata ya bilioni,ila sasa na wewe kumbuka ndugu zako wanavyotaabika kijijini kidogo kabla ya kufanya hivyo!!!!!!
 
Mi nafikiri DASA kama ilivyo avatar yako, u are really HIGH right now. Unachanganya mambo mawili kwa wakati mmoja. Ishu kama ni ushamba, basi u need to argue in favour of ushamba, lkn kama nimekuelewa vizuri, huoni haja ya mtu kuwa na simu ya milioni if simu ya laki or 50K can do the same. Where have u seen such a thing, since when a 50K worth of bidhaa can worth 1,000K bidhaa, u must be out of ur mind buddy. It is either huna hela au u just can understand why phones are priced for a million and more. sio ushamba kijana, its all about quality, elegance and meeting your needs. if u think u can do all what u want for a 50K mobile phone, well and good go for it. If you can afford a 1,000K mobile phone, shut your **** up, kaa pembeni and watch.
 
mmh may be hii ni kwa wale wanaonunua blackberry halafu hawawezi kuweka kkifurushi cha kila mwezi he he he he
 
simu sasa ni kila kitu
Simu
Msg
Emails
Internet..info..social networks
Saa..Alarm
Scanner
Mass storage device
Camera
Diary Planner
Mini bank
Torch
Radio
TelevisioGames gadget
Notebook
Voice recorder etc etc
Hivyo kama unaweza kuitumia vizuri ni bora kuwa nayo yenye uwezo
 
Bora kama mtu ananunua kwa pesa yake...Kuna wengine wanaenda kuomba pesa (kupiga mzinga) ili wanunue simu za bei mbaya ambazo ki-ukweli hawazihitaji!!

Babu DC!!
 
Wee ni pumbavu, simu yangu ni Samsung Galax2. Nenda kaulize bei yake ukiwa umeshiba sawasawa vinginevo utaonekana mshamba ni wewe.
 
Tukianza kufatilia mambo ya anasa ni mengi sana,
Kwa mfano. Mtu unaish kwenye nyumba kuuubwa peke yeko,
ni kwa nini usijenge chumba kimoja chakukutosha?
Mtu m1 unamiliki nguo nyiingi kwa nini usiwe na nguo 6 tu?suruali 3 shati 3 kwisha,
Mtu m1 anamiliki kochi set nzima,
kwa nini usichonge stuli moja tu ya kukalia wewe mwenyewe?
Tehe tehe tehe tehe ntarudi baadae.
 
Kuwa na simu si vibaya kama unaweza.
Kibaya ni kuwa na kitu bila sababu zaidi ya kujionyesha kuwa unauwezo, na
kibaya zaidi ni pata kitu kwa kutumia jasho la wengine na kujionyesha kuwa una uwezo.
Mfano:

  1. kiongozi wa umma kuwa na simu, gari, nyumba, n.k kwa kuiba mali za umma au kupokea rushwa. au
  2. mtu kuwa na vitu vya gharama wakati ndugu na jamaa wanaishi maisha ya shida
  3. au serikali kutumia mabilioni ya hela kutoa huduma zisizo za lazima kwa watu wenye uwezo wakati wananchi wasiojiweza wanashindwa kupata huduma za muhimu.
 
Pamoja na kuwa kuna wengi wana simu za bei kubwa wakati hawatumii hata nusu ya huduma zinatopatikana kwenye simu hiyo, lakini haimaanishi watu wote wanaotumia simu za bei mbaya wana ulimbukeni. Simu za kisasa si kama traditional phones ambazo kazi yake ilikuwa kupiga na kupokea basi. sasa hivi bei ya simu inabebwa kwa kiasi kidogo sana na voice part but rather huduma nje ya hizo za kupiga na kupokea.

Mfano smart phones zinaweza kupokea emails, kuunganisha (synch) kalenda yako ya ofisini na simu yako, kuandaa presentation, kusoma baadhi ya documents (word, pdf), kuchukua matukio kama picha au video au sauti, radio, TV, kuunganisha na mfumo wa mahali (GPS) na huduma nyingine nyingi ambazo kuna baadhi ya wamiliki wa hizo simu wanatumia.
 
Ww ndo mshamba kweli tangu lini simu ya elfu 50 ikawa sawa ba ya milioni 1..nenda hata kkoo ukaangalie..ndo wale wanaosema gari la cc 1000 sawa na la cc2000 kwani si unaenda tu mjini..issur muhimu it is why u like the phone n its functions.
 
Nina laptop na modem lakini simu yangu inanifanya nisione umuhimu wa hivyo.
Kwenye hii simu nina Microsoft office 2010
Opera Mobile 10
Internet exploler
Radio
Currency converter ya kila fedha internet based SPB SHELL
facebook application
Twitter application
Myspace ''
Operating system yake ni Microsoft Windows Phone 7.5
Adobe reader
Bei yake kwa Dar 1.6 M
japo kwa sasa inaweza patikana hata kwa milion 1.3
na ina mambo mengi sana na kii kipana sana kama palm top.

MIMI BORA UNINYIME KOMPUTER ILA SIMU IWEPO TENA SIMU NZURI SANA HATA IWE YA 3M NITANUNUA.

mtoa mada huna hoby na simu au hujui pocket technology.
Hapa nadhan hoja si ushamba bali interest.
 
Back
Top Bottom