Ushahuri wa bure kwa wamiliki wa Clouds na Mh. Sugu

Kule usukumani...hahahah....naona umechanganyikiwa hujua hata u-pst nini kazi unayo mkuu.................

Mti wenye matunda daima ndo hupopolewa mawe. Mpende msipende Clouds wako juu kama mawingu (with pun intended). Na mtaendelea kuumia sana watakapozidi kufanikiwa.
 
Kwanza Clouds!
Hakuna ubishi kwamba mnasikika kwa wengi na hasa katika vijana. Mmejipatia umaarufu kutokana na ubunifu wenu wa kutoa burudani na kutangaza. Bado kwa kiasi kikubwa mnaheshimika katika tathnia ya Muziki na Habari! kwa bahati mbaya sana ni kama mnaanza kupoteza mwelekeo wa mlichokusudia au mnachokusudia katika jamii ya Watanzania kwa kutaka kuwa na malumbano au kwa kujitetea katika misingi ya kuwakandamiza wapinzani wenu! Msifanye kosa hilo kwani litawaghalimu sana! mnaweza kutoweka kabisa katika akili za watanzania mkajikuta mnaharibu business zenu! kwani mkikosana na mtu katika jambo lolote hamuwezi kukaa chini na kumaliza tofauti zenu?! hivyo arrange na Mh. Sugu ili mmalize tofauti zenu la sivyo Sugu atawamaliza maana kajipanga na anakubalika!. Kingine pia, inaonekana kama mko kwa karibu sana na Sysytem kwa maana ya Serikali au kuna watu wanaonufaika na System kiasi cha baadhi ya watangazaji kushindwa kuficha hisia zao!. Si vibaya kushirikiana na System ila katika tathnia ya habari na hasa Radio jitahidini kuwa neutral maana mnawatangazia walio wengi. Hisia zako za moyoni zisitawale matangazo ila mwongozo na ethics mlizojiwekea ndizo zitangulie kama wanavyofanya Radio nyingine!. Jaribuni kusoma nyakati, pimeni mwelekeo wa kisiasa maana kuna watu wanazama hata ikipita miaka 10 dalili hazionyeshi kwamba watapona na wakati huo mtajiweka katika mizani gani?.

Mh. Sugu!
Hongera zake maana hakuna ubishi kwamba mh Sugu nyota yake inazidi kung'ara! ana supporters wengi kwelikweli na hii ni tangu nilipomfahamu tukiwa tunasoma wote pale Mbeya Day, maana shughuli ya Muziki kaianza mapema wakati ule akiwa ana-rap na kudanc na wakati huo akivalia suruali kifuani! checkbob kwelikweli wakati huo na chunusi kwa wingi BUT really Smart!. BIG UP MEN umetoka mbali!. Namshauri yafuatayo; Achana na malumbano yatakupunguzia sifa! ili uendelee kukubalika na watu wa kaliba zote fanya jitihada zote na wakati wote kujitengenezea heshima!. najua ni mpiganaji na wakati mwingine huwa hukubali jambo kirahisi na pale unapoonewa! badilika kwa sasa maana unao supporters wa kutosha likiharibika jambo wambie supporters nao watahukumu!. Tumia muda wako kuleta na kutafuta mbinu za kuleta maendeleo jimboni kwako maana 2015 si mbali hata kama hutapenda kuendelea wewe lakini usikiangushe chama chako! Bila shaka umeishajitengenezea kamati ya kuleta maendeleo na pengine kutokana na muongozo wa Chama chako!. Achana na upuuzi wa kulumbana maana unaweza kukasilishwa ukajikuta unazungumza mambo yatakayokuondolea heshima. Mwisho burudani yako tunaitaka, ukiwa unapata nafasi kama ilivyojitokeza juzi, tuite tutakuja!

Ni ushauri mzuri bt hawa wafu fm wanajifanya wajuaji sana tunakomaa nao tu hadi wawalipe vizuri wasanii kwenye matamasha yao ndo wataongea na sugu. Na huyo ruge amlipe sugu hela za maralia no more
 
Kabla ya uchaguzi mwaka jana nlikuwa nikiisikiliza clouse ila baada yakuona mambo yao hasa jahaz na walivyokuwa warogokaji sijawahi kuisikiliza wala sipendelei kuisikiliza tena
 
Back
Top Bottom