Elections 2010 Ushahidi wa wizi na udanganyifu kwenye matokeo ya kura huu hapa

jamani mi nashauri habari ya uchaguzi tuachane nayo.
wengine tunapata hasira sana lkn ndo hivyo hatuna la kufanya.

Lakufanya lipo, mwanamapinduzi huwa hakati tamaa mapema, na kama tusipochukua hatua sasa 2015 hawa jamaa watarudia upuuzi huu. Tutaandamana, tutakaa vikao, tutajadili mpaka kieleweke. Ni bora kufa tumesimama kuliko kuishi tukiwa tumepiga magoti. Ulimwengu mzima unatakiwa ujue kuwa ccm wameiba kura.
 
Ni kweli kama kuna ushahidi ni kukomaa,unajua viongozi wetu huwa wanajua watanzania ni watu wa kuchukulia kila kitu poa sasa wale wananchi wa mwanza wangechukulia poa basi jimbo la nyamagana na ilemela leo yasingekuwa chini ya upinzani.
 
Watu wamepiga kelele sana na kumponda Dr Slaa kuwa anaongopa kuhusu wizi na udanganyifu kwenye kujumlisha matokeo ya uraisi. Ushahidi wazi kuwa matokeo ya kura haya ni ya uongo ni huu hapa: Waosha vinywa pingeni na hili pia
Mistake of fact or mathematical errors which are not fatal
 
Watu wamepiga kelele sana na kumponda Dr Slaa kuwa anaongopa kuhusu wizi na udanganyifu kwenye kujumlisha matokeo ya uraisi.

Ushahidi wazi kuwa matokeo ya kura haya ni ya uongo ni huu hapa:



Waosha vinywa pingeni na hili pia

It was a mistake. They copied and pasted and 4got to change
 
Watu wamepiga kelele sana na kumponda Dr Slaa kuwa anaongopa kuhusu wizi na udanganyifu kwenye kujumlisha matokeo ya uraisi.

Ushahidi wazi kuwa matokeo ya kura haya ni ya uongo ni huu hapa:



Waosha vinywa pingeni na hili pia
:smile-big::smile-big::smile-big: mnajuwa kuna pahala mtu aliuliza INAKUWAJE pro azidiwe na mtu kama KUGA!! mimi nilimbabaisha babaisha na kumuacha kwanza, watu wengi hawajui matokeo yanavochakachuliwa. Watu wa Tume wametengeneza data base ya kijinga sana, inaweza kuchezewa kwa namna nyingi, na walioko majimboni wanatuma data kama walivoziingiza, kisha zinaenda makao-makuu ya wizi kama zilivyo, kule tayari formula inakuwepo yani data zikiingia tu zipo zinazozidishwa na zipo zinazopunguzwa, haijalishi siku hiyo MCHAKACHUAJI KALALAJE! NDIO MAANA KUNA WAGOMBEA HAWAKUONEKANA MAENEO MENGINE KABISA WAMEWAZIDI WALIOENDA HUKO!!

YANI AIBU TUPU KWA WATU WA IT nchi hii. Ila matokeo ya ukweli yatapatikana karibuni kama yalivyokuwa ya Zenji:A S angry:
 
jamani mi nashauri habari ya uchaguzi tuachane nayo.
wengine tunapata hasira sana lkn ndo hivyo hatuna la kufanya.

Nilikuwa sijui kama kuna watu wepesi wa kukata tamaa haraka kiasi hiki katika karne hii! Haki huwa inapiganiwa usisubiri kuletewa! Hili hata wanao chakachua kijinga wanalijuwa. Kupigania haki siyo mpaka ushike sime au mkuki, jifunze kwa watoto wachanga-analia kuita msaada! Hata KUPIGA KELELE ili watu wasikie kilio chako nayo ni mapambano! Waliopo karibu watasikia watamwambia anaye kuonea ama kukuminya awache mchezo wake! Huwezi kumkomoa mlevi kwa kuasusia pombe! Bora uimwage!
 
Hakuna siri ya watu wawili.

NEC hawakulijua hili.

Kwa nini vyombo vya ulinzi na usalama wanafumbia macho vitendo hivi vya wanasiasa?

Kwa nini? Kwa nini? Kwa nini?

---------------
vyombo gani?...embu rudia??.
vyombo sahihi ni mimi na wewe na yule, period! ambao hatushiriki kuiangamiza nchi, tulichokosa ni kukaa kambini au mgwanda tu...!
ogopa sana mwenye dhamana anapotenda chini ya kiwango cha asiye na dhamana yoyote, kurejesha hiyo title ni siku ya ufufuo..kama atakuwepo!
 
Back
Top Bottom