Ushahidi wa serikali yetu kufilisika huu hapa

tuko busy kuandaa sherehe za miaka 50...tumethubutu...wananchi kazeni mikanda wakati tunaendelea kuthubutu...subira huvuta heri! mbona miaka ya 80 Mwalimu aliwaambia tufunge mikanda mkakubali...tusubiri tisa disemba ipite...mambo yatakuwa mswanoo!
 
Wacha tushikishiwe adabu tndio tutaelewa kuwa kuendelea na CCM ni kujichimbia kaburi letu wenyewe bana. Wajinga kweli CCM huku wananunua majengo ya kifahari (gorofa sita halafu kwa bei ya kupaisha. Sijui na huyu balozi atafanyiwa kama za mahalu).
 
Kaka asante kwa data lakini tunaendelea kuishi na osia wa baba wa taifa.Serikali ya kihuni hata siku moja haiwezi kuwa makini
 
Duh! Serikali yetu bana, sasa kipi kinatangulia salary slip au mshahara wenyewe??????? How do you pay someone kabla ya salary slip!!!! Hii yote ni dalili ya ubabaishaji!

Mkuu mara zote watu wanakunja kabisa mishahara yao kwanza Salary Slip huwa zinatoka baadae kidogo,unaweza uipate mwezi unaofuata. Kuhusu mada hii watumishi wa Halmashauri na hatimaye serikalini kwa ujumla ndo wamekuwa wakituangusha sana katika vuguvugu la mabadiliko acha wangátwe kidogo
 
hakuna muhuri wala msikubaliiii wakuuuu ,na poleni kwa yaliyowapata.....
 
hapo haihitaji usome sanaaa! hakuna uhusiano wa unachotaka kusema na hiyo attachment yako!! nafikiri unapenda sana kuona unawachonganisha wananchi na viongozi wao si vizuri anza upya tafadhali
 
hii kamwe haikubaliki,lazima tutafute njia ya kuwawajibisha hawa manyangau.
 
Madiwani Kiteto walifanya jaribio la kumtema Mkurugenzi kisa Posho...ila bwana!kaaazi kwelikweli
 
unampa mfanyakazi pesa pungufu unategemea nini kama sio akimbilie kuiba?pia atakapolipwa atalipwa na riba?hili liserikali lakijinga sana.Hivi mtu na akili zako unathubutu kutoa tangazo la namna hii unachezea riziki za wafanyakazi.wafanyakazi wataiba mpaka karatasi za A4 maana wakauze mtaani siku hizi ni sh 13000 per rim kusogeza siku
 
Kwanini serikali za mitaa zisiwalipe wafanyakazi wake?.... wawafukuzie mbali hao wafanyakazi wa serikali kuu, hawana tija!
 
Nadhani haukuelewa ,taatizo halikuwa pesa , inaonekana kulikuwa na makosa yawezekana katika mfumo wa Compyuta na vitu kama hivyo usipotoshe watu. Kati ya Serikali ambayo imejitahidi kujali watu wake na hasa suala a kuwahisha mishahara.
Una utapiamlo wewe!!!!!
 
Louis Ottaru,
Ni vugu kuelewa ni vipi serikali imefulia kama ufuatilii kwa umakini kile alichokisema Zitto last time kuhusu serikali kukopa pesa zaidi ya US$ 700 Million (kama sikosei) kutoka Stanbic Bank kwa ajili ya kulipa mishahara.

Hata hivyo, kwa wenzetu ambao hamfanyi kazi serikalini nadhani ni vugumu pia kuoanisha ushahidi huu na yale yanayoendelea serikalini hivi sasa.

Ukweli ni kwamba kwa mwezi huu wa October 2011 serikali imelipa kwa mbinde sana mishahara ya watumishi wake. Kwa mara ya kwanza katika utumishi wangu serikalini this month tumelipwa mshahara tarehe 28 badala ya tarehe 19 hadi 23 kama ilivyozoeleka.

Ukiwauliza wa idara ya mishahara wanakwambia serikali imeshaleta payroll lakini exchequer kwa ajili ya malipo bado haijaleta kwa sababu bado wanaendelea kukusanya fedha. Hata sasa hivi ninavyokwambia OC (Operating Cost) exchequer ya mwezi wa kumi haijaja katika kituo changu cha kazi. Exchequer iliyokuja ni ya mishahara tu.

Pia tunasema serikali imefilisika kutokana na mazoea tuliyoyapata katika serikali zilizotangulia. Mfano wakati wa utawala wa Mkapa, OC zilikuwa zinakuja kwa Quarter tena in advance wakati sasa hivi zinakuja kwa Mwezi. Na zikija ni kidogo sana na saa nyingine haziji kabisa. Ukiwauliza watu wa Hazina wanasema hawana pesa. So kwa nini tusisema serikali yetu imefilisika wakati vitendo vinajionyesha??

Mfano kwa sasa hivi tunakaribia kumaliza nusu ya financial year ya 2011/2012. Nakwambia hakuna idara au taasisi yoyote ile ambayo ikifika tarehe 31 December itakuwa imepewa fedha za nusu ya bajeti yake. Hii ndiyo hoja na huo ndio ushahidi ndugu.

Hata ukitaka tukubali kwamba kuna makosa yametokea kwenye payroll system kwa mwezi huu bado inatakuwa ni vigumu kuturidhisha baadhi yetu maana uzoefu wetu unaonyesha hakuna mwaka ambao matatizo haya yametokea. Na kama yametokea kwa nini watumishi wapunguziwe tu? Iweje hiyo system haikuongeza kwa baadhi yao? Na kwa nini itokee katika sehemu nyingi? Huoni kama ilikuwa ni tactic ya ku-offset deficit ya mishahara kwa mwezi huu ambayo imeshindwa kukusanya?
[/QUOTE
Mkuu upo sahihi kabisa.Mimi mpaka sasa sijalipwa mshahara wa mwezi Oktoba na leo ni tarehe 29. Haijapata kutokea na tunakoelea sio kuzuri. Kuna watu wengi ninao wajua mpaka leo tupo ndani ya mkumbo mmoja kitu ambacho hakijapata kutokea kwa kweli!!!! Kuna shughuli nzito miezi ijayo
 
hapo haihitaji usome sanaaa! hakuna uhusiano wa unachotaka kusema na hiyo attachment yako!! nafikiri unapenda sana kuona unawachonganisha wananchi na viongozi wao si vizuri anza upya tafadhali
Asiyejua maana haambiwi maana. Haya niambie wewe kwanini mpaka sasa sijalipwa wakati mwezi umekwisha? au nalo ni tatizo la computer?
 
Eh! kumbe aliyosema Mkulo kuwa serikali ina fedha za akiba ilikuwa geresha!

Akiba ipi kiongozi!!!!!Hii serikali ni full magumashi fedha ya kuservice bajeti ya 2011/2012 yenyewe haipo ndo itakuwa na Ziada/surplus????Mwezi June/July Budget analysts waliliweka suala hili vizuri tu, kuwa bajeti yetu kwa zaid ya 50% ni tegemezi kwa wahisani, na hiyo fedha kidogo (less than 50%) inayotegemewa kutoka Serikalini haipo yote mkononi/hazina, yaani Serikali ilikuwa inategemea kukusanya kwanza (mwaka 2011/2012) ndiyo itoshe kuservice bajeti ya mwaka huu wa fedha 2011/2012.

Kwa hiyo inamana makusanyo yakichelewa tu basi hapo watumishi wa umma kukopwa ni nje nje, miradi mingi haitatekelezwa sio tu kwa wakati, bali haitatekelezwa kabisa, huduma muhimu zitarashiwarashiwa na mengine mengi tu yatabanwa, isipokuwa Safari za Rais na viongozi wengine ndo hazitaathirika na budget cut.

Tusipige mayowe, tuvumilie tu ndiyo faida ya kuchezea Kura, maana hakuna ambacho hatukuelezwa mwaka jana ila tuliamua kuirudisha serikali babaishaji madarakani, twendeni tu huko mbele tutaelewana tu. Wenzetu wapo Oyster bay mida hii wanagonga mvinyo ktk birthdays za wajukuu zao, sisi tunasumbuana na mabank teller na kuhangaisha ATM wakati cheques za mishahara hazijawa deposited kwenye Mabank. Hakuna Rangi tutaacha ona. Mbona hii intro tu!!!
 
mkuu umenikumbusha ya Tarik Aziz akitangaza kuwa majeshi ya adui yanazidiwa na kurudi nyuma wakati ni kinyume chake, mpaka alipokamatwa na jeshi la upinzani

Yah!!Yule jamaa kwa kweli alikuwa kioja sana kwenye ile vita ya Ghuba,mwishowe alikamatwa kama Bata na Wamarekani. Huyu Mkullo anaongea sana kupita vitendo kiasi kwamba anapoteza sifa ya nafasi yake, kama Waziri mwenye dhamana ya Uchumi wa nchi yetu.

I guess Mkullo ni mbabaishaji ila Suti anazovaa na kipara vinamlinda. Rais anatakiwa ajue kuwa kuna masuala mengine hayaitaji uswahiba. Yanahitaji really professionals/experts to run them. Suala la Uchumi wa nchi hii tukiendelea nalo kama tunavyofanya sasa, litatupeleka walipo Zimbabwe leo hii.
 
mwisho wa siku watasema kopesheni nguvu serikali,wamesahau kuwa mtu apewe chake kabla jasho halijakauka?watumishi wanaishi kutegemea mshahara wanategemea nn wanapotoa mshahara nusu au wanadhani watu wote ni mafisadi wana pesa za ziada kuendesha maisha?hii serikali imeoza kabisa,mishahara yenyewe midogo bado mnatoa nusu hii nchi sijui imekumbwa na balaaa gani eeh mungu tunusuru utuondolee hawa watu wanaozidisha maisha kuwa magumu kwa wenzao wakati wao wanakula na kusaza hawana habari nasi.
 
Back
Top Bottom