255Texter
Senior Member
- Aug 31, 2007
- 150
- 8
Kwa siku nyingi wananchi wa Tanzania tumekuwa tukisikia madai kwamba Rais wa nchi ni mtetezi au ni swahiba au anakumbatia watu wanasadikika kuhusika na vitendo vya rushwa, lakini madai hayo yamekuwa yakikanushwa na watu mbali mbali katika serikali na ndani ya CCM.
Lakini hivi karibuni tumeona kwa uthibitisho, vitendo ambavyo vinaashiria bila kupingwa kwamba kiongozi huyu wa CCM ambaye anataka aongezewe muda mwingine wa miaka mitano ya uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni kigeugeu inapokuja swala la kuonesha msimamo dhidi ya vitendo vya rushwa na wahusika wa vitendo hivyo. Uthibitisho wa picha na taarifa za wanahabari zimeonesha jinsi JK alivyowapigia chepuo tena bila aibu, wahusika wa vitendo vya rushwa kama Bw. Basil Mramba na Bw. Edward Lowassa, huku akimsafisha bila wasiwasi Bw. Lowassa toka ile kashfa ya Richmond.
Sasa, cha ajabu kupita vyote, ni pale JK ambaye ni mwenyekiti wa CCM na ndiye aliyeongoza vikao vya NEC-CCM ambayo alitoa 'hukumu' dhidi ya watu mbalimbali akiwamo Bw. Frederick Mwakalebela ambaye alienguliwa toka nafasi ya kugombea ubunge wa Iringa mjini kwa madai kwamba alihusika katika rushwa. Bw. Mwakalebela hivi sasa anakabiliwa na mashtaka ya kuhusika na vitendo vya rushwa, mashtaka ambayo pia yanamkabili na mkewe.
Cha kustaajabisha ni kwamba huyu huyu mtuhumiwa wa rushwa ambaye CCM amemhukumu na kumuondoa kabisa katika nafasi ya kugombea ubunge, leo amekuwa ni mtu wa kukumbatiwa na JK.
Ingawa mimi na wewe ambao tunaamini utawala wa sheria na haki ya kila binadamu, Bw. Mwakalebela tunamchukulia kwamba hana hatia hadi hapo itakapothibitishwa na mahakama kwamba kweli alihusika na vitendo vya rushwa na kuhukumiwa. Hivyo, mimi binafsi simhukumu. Ila NEC-CCM na huyu JK tayari walisha muona huyu bwana hafai, kwamba ni mtoa rushwa na ndiyo maana wakamuengua. Sasa huu unafiki wa JK kumkumbatia mtoa rushwa unaashiria nini? Je, ni mwendelezo wa kile kitabia cha JK cha kujichanganya na watoa rushwa? Au hii ndiyo inaashiria kwamba kesi ya Mwakalebela itapigwa zengwe na jamaa ataachiwa huru, kwa sababu ni "mwenzetu" ?
Waingereza wanasema - picture speaks louder than words.
Rais mkumbatia watoa rushwa(according to NEC-CCM).