DSN
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 2,837
- 1,674
Pamoja na kuusifu ujasiri wa Msemakweli na kumpongeza sponsor wake, ni mahali pamoja tu panaponikatisha tamaa juu yao, hili la kujikomba kwa CCM, sioni kwa nini msemakweli na sponsor wake wanahangaika sana kuonyesha kwamba fedha hiyo haina uhusiano na urais wa Kikwete, hapa nao wanakua kama hao hao wezi, wanabaka demokrasia, ni vizuri kama wanajikomba sana kwa JK, waache watanzania waamue kama hizo hela zilitumika wapi, kama msemakweli ni mkweli na msomi kama ninavyoamini, aache kabisa kukubali kuwa mpumbavu kwa kujiingiza kwenye unafiki wa sponsor wake, tunamjua na huyo sponsor pamoja na kufanyakazi nzuri tunamjua mnafiki kwa kuwa anajikomba kwa CCM tu kwa sababu ya maslahi yake binafsi. Huwezi kuwa popo kwenye ukweli na hiki ndio kina water down arguments nzuri na evidence nzuri za msemakweli. Hivi utasemaje eti hela hazikutumika kwa kuwa tarehe ya kuzihamisha ilikua baada ya uchaguzi? crap stop this rubbish, what is the relationship between tarehe ya uchaguzi na ya kuhamisha hela? hapa mngekazana na nani mwizi na yoyote aliyeshiriki ni culprit, mtatetea lakini tanzania ni ya watanzania wote siku ya siku bila kujali vyeo wala nini watafungwa tu jela watu hawa, hata mkiwauma na kupuliza, kumbuka hamuwezi kupambana na wakina Rostam na Manji mkitegemea eti kumwokoa JK, fanyeni maamuzi magumu kama mnajikomba sana kwa JK waacheni wakina Manji na Rostam wapumzike, hamuwezi kuwagusa hawa na kumponya JK wakati huo huo. neno linasema, mafuta na maji havichanganyiki, giza na mwanga vile vile, poleni sana
Kwenye Red ni kweli asilia kubwa Fedha hiyo aina uhusiano na CCM wala mgombea wa CCM,tulitaka kupumbazwa na MAFISADI kuwa ina uhusiano na CCM kumbe ndio ilikuwa iwe pona yao na kichaka chao cha kujificha.Manake Wezi wa mali ya Tanzania walio wengi wamekuwa wakijipanga na kujificha chini ya kivuli cha CCM [Kosa la Sumaye na usemi wake "Ukitaka kufanikiwa ingia CCM"].Aksante Mungu nae alimuhukumu mapema mapema na kisha sasa ni mmoja wa wafuasi wa kupigia kelele haki.
Mimi binafsi uwa nachukia sana na sipendi kusikia wakina kasuku wakilazimisha kusema pesa za EPa eti zilitumika kumuingiza Kikwete madalakani wakati kiongozi mmoja mkuu zama hizo hata yeye aliingizwa chaka bovu aliposikia taarifa hizo alipiga ukete mkubwa kushangaa maovu hayo.Mimi binafsi na jamaa zangu tulio wengi na na si ajabu hata wewe tulimchagua Kikwete asilimia 80% bila ya kupewa hata senti tano,kama wewe ulihongwa ututhibitishie.Sasa mabilioni hayao yalitumika wapi kama sio kikundi cha watu wachache,tena yakapelekwa kwao India na wanakojua wao.
Walitupumbaza sana na style ya kusema mabilioni hayo ndio yaliyomuingiza mgombea wa CCM madalakani na kuyafanya kuona ni sehemu ya Serikali na mipango ya kihayawani.
Hakika ili pia litakuwa ni fundisho kwa CCM kuanza kujitoa kwenye mikakati ya Kiserikali zaidi ibakize kuwa ni chama kinachounda Serikali na si kuacha watumishi wake [Viongozi wa CCM na Wafanyabishara majangili] kuhujumu Umma kwa mgongo wa chama Serikali au chama madalaka.
Na hakika tungeendelea kuimbishiwa na kukalilishwa nyimbo za kuwa fedha za EPA ndio zilimuingiza Rais wa tiketi ya CCM madalakani na hakika hatutafika na tusingefika hapa tulipofikia kwa akina Msemakweli.Njia sahihi ya kupambana na watu wa aina hii ya UFISADI ni kutenganisha wao na hicho cha kusema ilikuwa ni kwa faida ya CCM.
Wenzetu Nchi zingine uovu wa kitaasisi au kundi la watu au mtu mmoja mmoja daima una mtu wa kuwajibikana tatizo au kosa husika [Somone to be blame or someone is to be responsible to the matter]. Kwanini sisi uwa tunatabia ya kuweka lawama kitaasisi na sio mtu. Lawama za kitaasisi uwa wanaweka kwenye vyombo vya ulinzi na usalama,lakini pia nao aliyejua uwajibishwa ili liwe funzo kwwa walio juu kuwa makini kila wanapokuwa na crisis situation yoyote kuitazama kwa jicho kali,na kuwawajibisha wa chini yao.Lakini bongo ni tofauti hakika.