Ushabiki kumpamba Lowassa leo: Ujinga halisi wa Watanzania au laana ya fedha?

Sasa CCM imekuwa safi baada ya Lowassa kutoka? Chenge, Ngeleja na wengine vipi? Halafu kama mnaamini ni mchafu kwanini hakushughulikiwa? Maana yake CCM ni dhaifu haiwezi kupambana hata na mtu mmoja tu kwa faida ya Taifa-hakika imechoka, ipumzishwe.

Wapi nimetaja CCM?Kwangu mimi mchafu ni mchafu awe CDM au awe CCM.....
 
Hawamchagui Lowasa Wamechagua mabadiliko nje ya ccm ni vigumu sana kubadilisha maamuzi ya watu Kwa sasa

Ndo tunajenga tunabomoa? mabadiliko gani nje ya ccm toka kwa mtu asiyejiweza kiafya,nguvu na hata akili? mwenye kuleta mabadiliko c pesa tu bali kuwa na afya,nguvu na akili! ndo maana wahenga walixema,!"KOSA MALI PATA AKILI".ni bora zaidi
 
Wizi unaonekana ni ujanja na mashabiki wake wote ni wale wapiga diri
 
Siamini! siamini! siamini!

Ushabiki huu ulipoanza nilidhani kejeli. Baadhi walianza kwa kusema Lowassa bado ana nguvu sana ndani ya CCM nikaamini (nakubaliana na hilo 100%), Wengine wakasema yeye ni mkali kidogo kuliko JK nikakubaliana na hilo na mengine mengi yakaja ya ukweli na ya uongo. Sikudhania itafika siku watokee watu wa kumkweza Lowasa kufikia hatua ya kuanza kampeni za kumtafutia urais mapema kiasi hiki.

Mmoja kaamua kumlinganisha Lowassa na Dr. Slaa akidai mmoja kati ya hawa pekee ndiye angefaa kuongoza nchi yetu (kama itakuwapo bado) ifikapo 2015 Oktoba. Nimeshtuka sana kuiona hali hii ya ushabiki wa ghafla-ghafla kumuunga mkono Lowasa.

Hawa watu wanaotaka Lowassa (ambaye yupo tayari kufanya lolote kupata urais) awe na hadhi sawa na Dr. Slaa (aliyesubiri watu wengine waseme anafaa urais na kumwomba agombee) wanatumia kigezo gani?

Lowassa aliyedai wabunge wamemwandama kwa habari za magazeti ya udaku na kushindwa kuthibitisha hilo leo anafaa vipi kuwa rais wa Tanzania? Kwanini kama tunaipenda nchi yetu kwa dhati tusimtupilie mbali jumla ili akija kiongozi mwingine awe na nidhamu na kujua kuwa watanzania ukiokosea wanakutimua na ajizuie kukosea maksudi?

Je, ni kweli kwamba tumefilisika viongozi wanaofaa na kubakiwa na Lowasa pekee huko kwenye Magamba? Is it possible kwamba tu wajinga kiasi hicho au ni laana ya fedha ili tuamini kuwa wanaompigia debe wanatarajia kupata fadhila zake mzee huyo, asiyecheka na wanyonge kama watendaji katika wilaya na kuwanyenyekea wenye fedha kama Rostam hata kufikia kupindisha sheria maksudi ili watajirike zaidi kwa gharama za wanyonge? Ya Richmond si madogo lakini naamini vyombo vyetu vya dola vingekuwa huru vingegundua madudu mengine zaidi.

Nawatahadharisha watanzania kutofanya kosa la kumfagilia Lowassa, si kwa ajili ya kumwadabisha tu bali kuweka msingi imara kwa waroho kama yeye endapo watajitokeza next time. Viongozi wajao wanatakiwa kujifunza kutokana na adabu tutakazoamua kuwatia kina Mkapa, JK na wapambe wao kwa makosa ya kukusudia waliyofanya ili kujitajirisha.

Tuendelee kumwomba Mwenyezi Mungu atuasaidie kupata viongozi bora na kutuepusha na watu wa "Zamu Yetu" kama Ridhiwan, JK, Lowassa na wengine wengi ambao tutazijua habari zao vema baada ya serikali ya wanamtandao kuondoka madarakani.

mwaka huu mtatupa mengi ila mwisho october 25
 
kuna ID nyingi sana humu ndani ambazo zilifunguliwa na watu waliopewa hela na huyu fisadi ili wamdafishe jf. Bahati mbaya sijui aliewanyia interview hakuwapima akili maana hata hoja hawana zaidi yakutukana watu.
 
Wewe unataka hoja gani

Wewe Wa ccm sio muda wako Wa kuomba ridhaa tena

Huu ulikuwa muda Wa kuonesha Yale uliyo yafanya na uliyoyashindwa ni kwasababu zipi

Sio uneleta manunguniko na hii mizoga yako
 
Attachments

  • 1444396265002.jpg
    1444396265002.jpg
    53 KB · Views: 222
Nguvu za nyani, uwezi sema awamchagui Lowasa, eti wanachagua mabadiliko nje ya ccm.
Nje ya ccm ndipo alipo mtu waliye mmsema fisadi atakuleteaje mabadiliko? Chadema ndiyo chama kilicho kemea ufisadi nilitegemea wale waliopinga ufisadi ndiyo wagombee urais mfn Dr Slaa ndiyo alkuwa mtu wa mabadiliko ya kweli.
 
Kwa hiyo kumshabikia Lowassa ni ujinga ila kuishabikia CCM iliyomlea na kumfikisha hapo alipo ni busara?
Kwamba shule inayotoa wahitimu wabovu ndio rahisi kubadilika kuliko kumbadilisha mhitimu mmoja!Huu ni uendawazimu.
Tunamchagua Lowassa kwasababu hayupo CCM basi! Na hatumchagui Magufuli kwa sababu yupo CCM,basi!
Tuiteni Mafala,Malofa,Wapumbavu poa tu ila tuna kisirani na CCM.
Tuna kisirani na CCM iliyoua viwanda,iliyoua reli,shirika la ndege,iliyosafirisha twiga,iliyoharibu ubora wa elimu.Waambieni hao wanaopiga pushup ovyo kuwa tumeamua kuwanyima kura,mimi pia napiga sana pushups ila nampigia mke wangu anayenipikia.
Tena mwambieni hatuhitaji mpishi wa taifa,tunampenda kama waziri aliyejitahidi kutimiza baadhi ya majukumu yake ila Urais hatumpi.
CCM ndio adui yetu na sio Magufuli.
 
Lowasa out......!
 
Upumbavu ni kuona ccm wasafi kwakua wamemteua magufuli hapo ndo utaona uboya wa majitu ya tanzania yanasahau kuwa mafisiem ndo yaliyotufikisha hapa yani kama wamelogwa vle
 
Muachelongolongo,safari hii mtaongea yote,na mwisho wa siku raisi ni lowasa, kwani hata huyo pombe hafai kuwa raisi
 
Back
Top Bottom