Usawahilini kuna vituko

Status
Not open for further replies.

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
864
YANAYO KUFANYA UWE MSWAHILI...

1.Unamwita mtu usiyemjua (wala kukutana nae kabla) 'aunt au anco'.

2.Stoo yako imejaa vitu (makorokoro) kwa kuwa hutupi kwa kuamini kuwa ipo siku utayahitaji kwa mfano karpet ukilitoa hulitupi n.k.<?

3.Una machupa ya maji matupu, shampoo, perfume pamoja na vipodozi vingine umeweka tuu ndani mwako wala huna shughuli navyo.

4.Watoto wako wote wana majina ya utani mfano babu ali,chidi,mamu,dida n.k.

5.Hakuna mtu katika familia yako anayetoa taarifa kwako anapo kuja kukutembelea mfano kaka, shangazi n.k.

6.Mifuko yako imejaa vitu kama vile vijiti vya kusafishia meno,tissue n.k ulivyochukua sehemu kama vile mgahawani.

7.Mama yako ana migogoro na ndugu na hawazungumzi kwa muda wa siku zipatazo 10 au zaidi.

8.Hupigi simu isipokuwa katika muda ambao gharama za kupiga ni nafuu(mfano usiku sana)na mara nyingi huwa una beep tu.

9.Ulipokua mdogo nguo unazonunuliwa pamoja na viatu ni vikubwa mara mbili ili uweze kuvivaa muda mrefu zaidi.

10.Unapomsaidia mtu na akafanikiwa basi utakuwa unasema kama sio mimi asingekuwa vile yule.

NOTE.
Wapelekee waswahili wengine ili wajue ni kitu gani kinawafanya wao wawe waswahili..........................

[FONT=Courier New, courier, monaco, monospace, sans-serif]Please!!! Tubadilike na mambo hayo ya kiswahili.

[/FONT]
 
Ha ha ha Gender sensitive umenifurahisha,

Kwa kuongezea, unapokuwa mswahili unadhani watu wote hawana macho, hata ukiwa na ujumbe wa maandishi unaandika kwa maandishi (fonts) makubwa ili wausomao wasipitwe hata na nukta hahahahaha
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom