Usanii wamponza Mnyika - Uhuru

huku kimara stop over kuna vijana kazi yao ni kufukua na kuunganisha mipira na kuwajazia matank watu wenye uwezo. wamehalalisaha kama ndo shughuli yao halali na hakuna hatua zinazochukuliwa. yaani hawana shughuli nyingine zaidi ya hiyo
 
Wana JF magezeti ya leo asubuhi kupitia Clouds FM yameripoti Mbunge wa Ubungo apondwa mayai viza kisa hajawaletea maendeleo.Wabunge wanapswa kutekeleza ahadi zao kwa matendo na sio kwa maneno.

Huyu Kijana mpambanaji anahitaji ushauri wa kulinda polical performance yake.

mbunge afanyiwe fujo na uhuru tu ndo waandike? of all magazine in town? i dont buy this clap
 
unataka mbunge asambaze mabomba kwa hela yake,kazi ya serikali ni ipi na kazi ya mbunge ni ipi? Mbona hatutofautishi majukumu ya mbunge na majukumu ya serikali? Ndo maana wabunge kila siku wanaamkia posho aafu tunaanza kupiga kelele. Kama serikali ya wahuni haitaki kuhudumia wananchi wake unadhani mbunge ni taasisi ya kufanya kazi badala ya hilo genge la majambazi? Kwani mbunge ndo anapokea na kukusanya kodi za mapato? Tuwalaumu wabunge wakishindwa kutekeleza majukumu yao ya kuibana serikali iwatimizie wananchi kile kinachotakiwa.

next likes this
 
hizi habali zimeandikwa na gazeti la ccm....linaloitwa uhuru lakini kiukweli huu ni uzushi mtupu.....na ambao umeandaliwa na kundi flani la vijana wa ccm kuna dogo anaitwa salumu huyu jamaa ni kimbelembele sana hata malumbano ya hoja huenda pale na kubwabwaja hovyo....hovyo halafu anajiita mwanaharakati wa amani......ndugu mnyika achana nao.....hawa jamaa tunawafahamu wana ganga njaa ccm....baada ya kumaliza udsm...na kukosa ajira sasa wanatafuta channel za kutoka kimaisha kwa kuendekeza propaganda....za uongo hadi facebook on jamii forum wamepost hii mada.....hawa jamaaa
 
Sasa napata picha kuwa haya magagazeti tangu enzi zile tunakua yakiwa ndo magazeti pekee tanzania yalikuwa yanatupa habari za uongo. Nina imani hata wa ccm wenyewe hawayasomi. hata muuza maandazi atakuwa hataki kufungia maandazi yake
 
Mkuu Mnyika Pole na Majukumu kwa kweli Wakazi wa Ubungo tunajivunia kuwa nawe kama Mbunge wetu. Mkuu Mnyika Kwa Akili za CCM siwezi kabisa Siku Nikisikia Wamekupiga Mawe ama Kukuzomea "Ili Ionekane kwamba Umeshindwa Kazi" Juzi nilisoma Thread Moja hapa kwamba "Wana CCM wanaojiita Wakazi wa Ubungo wataandamana Kukupinga"

Mimi Nakushauri hao jamaa kama wana Mpango wa Kuandamana wasaidie Kupata Kibali Cha Polisi na Pokea Maandamano yao Wape Eli ya Uraia halafu Baada ya Hapo Gawa Kadi kwa Sababu kinachoonekana kwa wana CCM hao ni Ukosefu wa Elimu ya Uraia

Please Usiwakimbie, Wasaidiie Kupata Kibali cha Maandamano, Wape Mabango na Markapen za Kuandika Ujumbe wao,Pokea Maandamo Mwisho TOA ELIMU YA URAIA

Wakuu,

Nashukuru sana kwa imani ambayo mmeonyesha kwangu, tuendelee kushirikiana. Ilipotolewa taarifa huku kuwa kuna 'wananchi' wa Makuburi wanataka kuandamana kuja kwa mbunge, niliandika hapa JF kuwa nawakaribisha sana; na kama wanakwama kupata vibali waniambie niwasaidie kupata.

Nilipoona kimya, nikaenda mwenyewe eneo husika ili nikutane na wananchi wa Makuburi wanaoelezwa kutaka kuandamana. Nilikuwa Kata ya Makuburi Machi Mosi, na nilifanya mkutano katika ofisi ya kata nikakutana na wanawake, vijana na wazee; ukweli ni kwamba walianza kurusha lawama kwa DAWASCO na mamlaka zingine za kiserikali na kumshukuru mbunge kwa hatua ambazo amekuwa akichukua kuhusu maji katika kata husika. Wakaeleza maeneo ambayo bado yana matatizo kuhusu mabomba na wachina na maeneo ambayo hayakuwekewa mtandao wa maji kabisa miaka 50 toka Uhuru, ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa.

Nitaendelea kujibu hoja kwa hoja nikirejea katika majukumu ya kawaida; nashauri kero hizo pia zifunguliwe mjadala wake ili nizitolee majibu na maelezo huko maana mjadala huu unajadili kuhusu 'mayai viza' na 'gazeti la uhuru'.

Kuna mitazamo miwili katika maoni ambayo yametolewa hapa kuhusu habari hii:


Wengine mmesema niipuuze hii habari baada ya kuwa nimetoa ukweli hapa. Wengine mmesema ni vizuri nikatoa kauli pana kwa kuwa habari hii ya uzushi imesomwa kwenye baadhi ya TV na radio na hivyo propaganda hizi nyeusi kuenezwa.


Wengine mmetoa mtazamo kwamba ni vizuri nikachukua hatua zaidi dhidi ya gazeti husika na wengine mmeshauri nisichukue hatua zozote kuepusha kupotezewa muda na badala yake niendelee na kazi za utumishi wa umma.

Kwa kuwa maoni yamekuwa tofauti tofauti kuhusu suala hili, mjadala uendelee.

JJ
 
Mnyika hizi habari za uwongo si za kuacha hata kidogo maana binafsi zilinishtua sana! Wape gazeti la uhuru siku 3 kukanusha front page kinyume na hapo wapeleke mahakani kuwafunza adabu.nina uhakika kama lingekuwa gazeti lingine dhidi ya mbunge wa ccm ingekuwa hivyo hivyo.Lazima wakutake radhi front page maana wamekudharirisha kihuni! Habari hii wanachama wa JF ndio wanajua ukweli lakini imesomwa na kusikiwa na watanzania wangapi? Yapo ya kupuuza lakini si habari ya uwongo ya kuwachonganisha wananchi na mbunge wao tena kwa uwongo wa kihuni kabisa.usiwape siku nyingi za kuomba radhi siku tatu zinatosha kabisa mkuu.Mhariri wa Uhuru ni m.puuzi anae penda kujikomba kwa wakubwa sasa this time lazima ile kwake.MAHAKAMANI TU W.AJINGA HAWA!
 
Mi nahic ni Mnyika mwingine kama tulivyozoea kusikia timu za mpira Argentina ya Manzese au Bacelona ya Mbagala
 
Siasa za Chichiem za maji taka hizo; sawa ni zile propaganda za Te ndwa kwamba washili walimng'ata sikio eti G. Lema asifike Arumeru kwa ajil kampeni uchaguzi mdogo na kwamba akifika watamuua, UZUSHI MTUPU.

Na inakuwaje habari kubwa namna hiyo ya *Mbunge kutupiwa mayai viza' ilipotiwe na gazeti moja tu? Halafu Dar Es Salaam kwenye magazeti na blogu nyingi?
Kweli magamba wamechoka
 
John washtaki,vinginevyo watarudia au wape agizo la kukanusha seriousely mkuu.Usiache hili lipite hivi hivi.
 
Wana JF magezeti ya leo asubuhi kupitia Clouds FM yameripoti Mbunge wa Ubungo apondwa mayai viza kisa hajawaletea maendeleo.Wabunge wanapswa kutekeleza ahadi zao kwa matendo na sio kwa maneno.

Huyu Kijana mpambanaji anahitaji ushauri wa kulinda polical performance yake.


Ni ahadi gani alizotoa na hajatekeleza?
Ziorodheshe tuzijue, na yeye azione, sio kutoa general statement tu.
 
Umeita tetesi halafu umetoa hitimisho kama vile ni ukweli, hizi sasa ni siasa chafu. Ni vizuri ukaeleza nilipigwa mayai viza lini na wapi? Vyombo vya habari unavyovisema ni vipi na weka hapa habari kamili ijadiliwe. Niko tayari kupokea ushauri, lakini si vyema kuleta uzushi na propaganda nyeusi.
JJ
mheshimiwa tuko nyuma yako achana na hao majitaka!
 
Kwakuwa JK na CCM yake hawajatelekeza ahadi na Chadema nao wasitekeleze???

Kwa kweli huku tunapoelekea kipenda roho hula nyama mbichi.

Kweli Chadema wanatakiwa kutekeleza ahadi zao.
Ziwekeni hadharani ahadi hizo tuzione, sio kutoa general statement tu kuwa hawatekelezi ahadi zao.
 
Back
Top Bottom