Usanii wamponza Mnyika - Uhuru

Anastahili kupopolewa, bora wangemnyuka kisawasawa, amekalia kupiga domo tu huyu.
 
katika viongozi wa kisiasa wote hapa tz (na pengine East Africa yote).. ni John Mnyika pekee yake ambae anafanya kazi zake kisasa.. anaweka taarifa ya kazi zake katika mtandao.. akiorodhesha kero na jinsi ya utatuzi wa matatizo yanayolikabili jimbo lake na tz kwa jumla..! najua hili linawakera wengi ambao kwao uongozi umepotea njia.. so watajaribu kila wawezalo kum-discredit John.. Naomba wale wote wenye mapenzi mema na nchi hii waendelee kumlinda John dhidi ya hawa wasio na vision.. Peke yake hataweza bila ya msaada toka kwe2 maana hawa ni watu ambao wako tayari kuwaua hata wazazi wao..
Mkuu nimependa mchango wako. Mimi binafsi namkubali sana John Mnyika. Ni kweli anafanya siasa tena za kistaarabu na za kihoja. Amejipambanua kwa hilo na kwake maslahi ya Taifa na watu wake huwa mbele. Hufikia hata wakati akasema twende kwenye win win situation badala ya kuvutana bila sababu. Hilo bila shaka limemjengea maadui wa NDANI na NJE ndani ya Tanzania.
 
Hi thread imeshajibiwa na mnyika mwenyewe humu jamvini mchana,naona umeamua kuirudisha tena na chanzo chake cha gazeti la chama cha CCM uhuru,habari hizo ni uongo mtupu na Mh mnyika ameshakanusha humu jamvini! Haya nenda ofisi za CCM ukachukue posho baada ya kumaliza kazi uliyotumwa na masaburi wako Nape.

nilikuwa sijaona kama alikwisha ijibu lakini mi ndio nimeiona mida hii kwenye gazeti la uhuru! Hizo posho kwa Nape hapo mi sijui, labda we unaweza ukawa unafahamu sana kuliko unaemsadikisha anachukua posho!
 
Umeita tetesi halafu umetoa hitimisho kama vile ni ukweli, hizi sasa ni siasa chafu. Ni vizuri ukaeleza nilipigwa mayai viza lini na wapi? Vyombo vya habari unavyovisema ni vipi na weka hapa habari kamili ijadiliwe. Niko tayari kupokea ushauri, lakini si vyema kuleta uzushi na propaganda nyeusi.
JJ

Mkuu Mnyika Pole na Majukumu kwa kweli Wakazi wa Ubungo tunajivunia kuwa nawe kama Mbunge wetu. Mkuu Mnyika Kwa Akili za CCM siwezi kabisa Siku Nikisikia Wamekupiga Mawe ama Kukuzomea "Ili Ionekane kwamba Umeshindwa Kazi" Juzi nilisoma Thread Moja hapa kwamba "Wana CCM wanaojiita Wakazi wa Ubungo wataandamana Kukupinga"

Mimi Nakushauri hao jamaa kama wana Mpango wa Kuandamana wasaidie Kupata Kibali Cha Polisi na Pokea Maandamano yao Wape Eli ya Uraia halafu Baada ya Hapo Gawa Kadi kwa Sababu kinachoonekana kwa wana CCM hao ni Ukosefu wa Elimu ya Uraia

Please Usiwakimbie, Wasaidiie Kupata Kibali cha Maandamano, Wape Mabango na Markapen za Kuandika Ujumbe wao,Pokea Maandamo Mwisho TOA ELIMU YA URAIA
 
Ni uzushi tu.

Uwe uongo ama uzushi kazi yetu ni kuchukulia hiyo kama changamoto KWANI ni kweli kuna negative response kutoka kwa public kwa mtazamo wa poor performance ya wabunge wetu vijana kote, mfano mbeya ukuacha mh. silinde kule mbozi anaonyesha uhai. siwezi sema sana kwa myika ingawa nimepita maeneo ya mbezi lwis na kwa msuguri nk sijaona malalamiko yoyote. lakini hata hivyo asije na kukataa bali afanyie kazi
 
kuna baadhi ya mijitu humu ni mapu...kabisa, yaani yanakuja na post za ajabu ajabu sijui yamelipwa shilingi ngapi na napee yawachafue watu!
 
Mkuu wa chuo, chanzo cha Habari kama ni Uhuru hapa huwa hakiheshimiki kwasababu ni gazeti la magamba.
 
Uwe uongo ama uzushi kazi yetu ni kuchukulia hiyo kama changamoto KWANI ni kweli kuna negative response kutoka kwa public kwa mtazamo wa poor performance ya wabunge wetu vijana kote, mfano mbeya ukuacha mh. silinde kule mbozi anaonyesha uhai. siwezi sema sana kwa myika ingawa nimepita maeneo ya mbezi lwis na kwa msuguri nk sijaona malalamiko yoyote. lakini hata hivyo asije na kukataa bali afanyie kazi
Umesema mkuu. Ni kweli Mnyika asitegemee tu kujenga hoja ndani ya Bunge. Kwa kujenga hoja namkubali ila akumbuke wanaubungo huwa hawasilizi hoja wanataka matendo hivyo basi aendelee kutenda. Nakumbuka Mwaka 2010 kabla ya kura za maoni ndani ya CCM nilikuwa Kyela. Katika pitapita yangu nikagundua kulikuwa na watu wanamwaga bia na soda kwenye vijiwe, wakati watu wanaendelea kunywa jamaa wakawa wanatumbukiza hoja na kusema: Jamani huyu mbunge wetu sisi tunataka atuletee maendeleo jimboni kwetu lakini yeye amekuwa akiongelea mambo ya kitaifa kuhusu ufisadi, hatufai huyu! Mnyika nawe usije ukajengewa hilo zengwe!
 
Duh!!!!!
Gazeti la uhuru lipo mtaani?


nilikuwa sijaona kama alikwisha ijibu lakini mi ndio nimeiona mida hii kwenye gazeti la uhuru! Hizo posho kwa Nape hapo mi sijui, labda we unaweza ukawa unafahamu sana kuliko unaemsadikisha anachukua posho!
 
learning by doing!we unadhan watapractice wap kulinda kura zao!safi sana,vjn wapige tizi jingine shabaha ya kulenga tyr wanayo!
 
kiongozi mnyika jibu maswali na kero za wananchi acha propaganda.ni vyema mambo kama haya uyafanyie kazi kwenye field ujiridhishe ujue ukweli kama ni uzushi au kweli.
 

[h=6]John Mnyika
[/h] [h=6]Katika jiji la Dar es salaam kuna changamoto kubwa ya ubora na bei ya maji kwenye sekta binafsi; bei ya maji iko juu sana hali ambayo inashawishi biashara haramu yenye kuhusisha hujuma katika miundombinu ya maji na ufisadi wenye kuharibu ratiba ya mgawo wa maji ili kupanua soko holela kinyemela.

EWURA ina wajibu kama ilivyo kwenye mafuta na umeme kusimamia sekta ya maji siyo ya umma tu hata bin...afsi, hata hivyo kwa sasa inasimamia zaidi bei na ubora kwa upande wa mamlaka za umma. Hivyo, nimewataka ndani ya wiki moja watoe kauli kuhusu hatua iliyofikiwa katika kuandaa kanuni za usimamizi wa sekta binafsi ya maji juu ya mfumo wa bei elekezi na viwango vya ubora kama ambavyo mamlaka husika iliahidi kwenye Kongamano la Maji Ubungo mwaka 2011.


[/h]
 
Mh. Naomba nitoe kero yangu inayohusu kufunguliwa na makanisa kwenye makazi ya watu. Jirani yangu kafungua kanisa, ambalo husalisha kwa kutumia loud speaker Mchana kutwa na hata usiku wa manane. Miiundombinu ya barabara na choo ya sehemu ye...tu hawezi kuhumili umati wa waumini wa kanisa hili, Nimepeleka kero hii kwa Diwani wangu Single, pia kwa kushirikiana na majirani wengine tumeandika barua ya malalamiko kwa afisa mipango miji wilaya ya Kinondoni mpaka sasa hatujapatiwa ufumbuzi sasa ni mwezi wa tatu. Tunashindwa kujipumzisha na pia kero kwa wagongwa pia. Tunaomba utusadie kwa hili kwa ofisi za watendaji serikali za mitaa na kata zinapata kigugumizi kituambacho hatukielewi.
 
Back
Top Bottom