Usanii wa sales kwenye nchi dunia ya kwanza

Limbukeni

Senior Member
Feb 27, 2009
117
1
Kumekuwa na kamtindo cha kupandisha bei ya bidhaa kwa kuwavutia wateja na kuwapotosha bei halisi na kusema ni bei punguzo ili kuwe na nafasi ya kuongeza gharama za ununuaji wa bidhaa hiyohiyo kwa kipindi kijacho. Kwa mfano bei halisi ya bidhaa ni shilingi 100 anasema bei halisi ni sh 200 okoa asilimia 50 nunua kwa sh 100 kumbe ndio bei yake. Baadae ukija unakuta ni sh 200. Sale imekwisha. Labda ninapotosha naomba maoni zaidi juu ya hili swala.
 
ni kweli mkuu, maduka karibu mengi tu ya dar hasa ya nguo kila ukipita kuna vibao vya sale! sale!discount, sale! 50%off! wizi mtupu, hii imekuwa inatumika kama sales strategies lakini imekaa kiwizi zaidi, kwa asiyefahamu anaweza kimbilia kwenye maduka haya akadhani kweli bei ni pungufu kumbe changa la macho
 
Kumekuwa na kamtindo cha kupandisha bei ya bidhaa kwa kuwavutia wateja na kuwapotosha bei halisi na kusema ni bei punguzo ili kuwe na nafasi ya kuongeza gharama za ununuaji wa bidhaa hiyohiyo kwa kipindi kijacho. Kwa mfano bei halisi ya bidhaa ni shilingi 100 anasema bei halisi ni sh 200 okoa asilimia 50 nunua kwa sh 100 kumbe ndio bei yake. Baadae ukija unakuta ni sh 200. Sale imekwisha. Labda ninapotosha naomba maoni zaidi juu ya hili swala.

Kwa huko ughaibuni kuna kitu kinaitwa REBATE. Jisomee hapa kwa maelezo zaidi.
Pengine kuna wasanii wachache wa mfano uliyoeleza hapo juu, hata hivyo, discount nyingi ughaibuni si za kilaghai. Kipindi cha summer kwa mfano, unaweza kuona discount ya nguo za winter, nguo ambazo sio rahisi kupata soko baadae katika kipindi kijacho cha winter.
 
rebate au rudishio ni punguzo la bei unalolipata baada ya kulipa bei yote. mfano bidhaa ni sh 200 wanasema wanakupa punguzo la sh 50 lakini ni rebate wewe unalipa 200 halafu baada ya muda kama mwezi wanakurudishia hamsini. lakini wengi au wote huwa hawarudishi keshi. wanakutunia kadi yenye thanmani hiyo kwa hiyo unaenda kuchanja kufanyia matumizi.
 
Back
Top Bottom