''USANII'' na WAPENZI WETU/WAKO...tukumbushane!

Hii thread mpaka sasa nishazoma uzoefu wa Asprin na Klorokwin.........yaani nyie mnaonekana ndio mlikuwa wahanga wa haya mabomu haswa!

Baada ya kusema hayo.......................namalizia na....

Mpenzi kwako nimefika Kigoma mwisho wa reli, nauli ya kurudia sina wala pa kukopa sipaoni!!
 
daaaaaaaah!......

baba ubaya hapo ulijipangeje sasa mpwa?

Nikarudi home nikapiga akili, kilichofuata nikaenda kwa kinyozi wakati ule hakuna mashine ni kitana na kiwembe ndo mpango, akaninyoa kibwenzi,a kesho yake ilikuwa Jumapili nikaenda kwa dingi yangu mdogo alikuwa anauza mitumba nikamwomba akifungua anichagulie viwalo kama vya The wacko Jacko, Jioni akaniandikia kijikaratasi kwa kama kuwa viwalo vimepatikana na zaidi amepata na T-shirt yenye picha ya Michael Jackson. kesho yake asubuhi nikasonga pale wa mshua mdogo, nkachukua zile nguo nakumbuka aliniambia nimlipe sh.Elfu 7 nikalialia nikampa elfu 4. Bwana kufika nikazifua na sabuni ya mbunju, kesho yake saa nne nikajiweka kwenye kivazi kama michael kwama maelekezo ya mrembo yalivyodai, zaidi nikajipiga na kitu cha Yolanda, nkawa nanukia kishenzi.... mdogo mdogo huyooo kwa mrembo kali wa kitaa. kufika nikamkuta mdogo wake fasta akaniitia mrembo kuniona akatabasamu, kimkwara nikajifanya nacheza kama michael jackson zile za (kuvunja yaa Brake dance,slide na moon walk) mtoto kazinguka akanambia hapa kishotobe umempata!..... mambo hapo ndipo yalipoanza kuwa mazuri ila alikuwa wa mizinga mara nimnunulie dont touch, mara losso mara mafuta ya curl mhhhhhhhhh!!........Those where the days!!!!!



 
Komaa kabisa kaka,

ukija kwangu siku nyingine uje umevaa la kupanda (kiatu), jaketi na suruali nguo zilikuwa na (zipu nyingiiiii) kama la Michael Jackson, mi sio wa kuchezea chezea!

Nilijibiwa hivo wakati namtokea mtoto mmoja Mkali wa kitaani!


View attachment 49382

Aisee picha kali sana.... vijana wa zamani walifaidi kweli, ukiangalia hapo hata trauza ianpigwa kavu bila chupi wala nini! ly.jpg
 
Teamo hayo mbona mpaka leo yapo...
Utasikia "mitaa hii wewe mgeni, sijawahi kukuona mtoto?" wakati kila siku anakuona kituoni sasa siku hiyo kaamua kucheza karata zake. "ulikua wapi mtoto mzuri kama wewe wakati natafuta mchumba, natamani kama nimfukuze mwenzio kule nyumbani. Toto kweli, shepu, jicho, mungu kakupendelea sana wewe mtoto". Ukijiangalia hicho la kawaida, shepu kama umedondoka bafuni lakini unapewa sifa ile mbaya. ACHENI HIZO.....
 
Kuna mwengine anataka hela ya vocha anajifanya kukusimamisha halaf anaanza.

Jamaani! yaani wewe kijana umefanana na lonado di kaprio, khaaa! (wakati mzembe ukijiangalia kwenye kioo unajiona kabisa kwamba umefanana na Kibaki)

we hukutakiwa kuchangia bana! enzi hizo hapakua na mobile phones, kwa wale tulio soma bording usangi tulikua tunaenda posta kufanya booking kwa kutumia simu ya kusokota
 
Natamani usiku isifike niendelee kukaa na wewe
lakini ndo hivyo tena mama karibu anarudi toka kazini

wangu alinihamasisha cku moja kwenye zile barua zetu, eti ungekuwa huku au mi huko uliko tungekuwa tayari tumetusuana, NB nilikua sijaonja tunda bado
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom