Usanii katika mambo ya Msingi

Sungurampole

JF-Expert Member
Nov 17, 2007
984
205
Nafikiri sheria ya kuunda katiba mpya ni jambo la msingi!

Nimepigwa na butwa kujua kumbe wabunge wa CCM kuharakisha kupitisha muswada wa kuunda katiba mpya walifanya hivyo ili tu kuwakomoa Chadema ambao walitoka nje

Jana, Mwenyekiti wa CCM(JK) ansema hata wabunge wa CCM nao baada ya kupitisha muswada kwa mbwembwe wamewasilisha kwake marekebisho 8 ili yafanyike kuirekibisha sheria ya kuunda katiba mpya.

Najiuliza tunakwenda wapi kam anchi, je hii dhihaka na usanii katika mambo ya msingi itatufikisha wapi?

Nawasilisha wakuu hebu tutafakari wote kwa pamoja.
 
kwa nini pia hufikiri kwamba walitaka kupata njia/namna ya kumbana Rais kuongeza posho yao?
 
Mswada ukikwama haukwamishi chadema tu bali serikali na hata Rais. Tulijaribu kuwa wakweli.
 
Ukifanya kitu kwa mazoea! Ndio inavyokuwa.
Nakumbuka hata tulivyokuwa Class, mwalimu atawauliza mmeelewaaaaaaaa! Wanafunzi wote wataitikia ndiooooooooo!
Sasa mwalimu apite aulize mwanafunzi mmojammoja kuwa ni jinsi gani alivyoelewa!?
Kama darasa lina wanafunzi 80, basi watapatikana 10 tu! ambao watakuwa wameelewa nini kilichofundishwa.
 
Unajua tukiwabeza viongozi wa ccm na serikali yao kuwa ni vilaza wanatuona wahuni lakini ukweli ndio huo hawapo serious na mambo muhimu ya kitaifa zaidi ya kupigania posho ziongezwe, wabunge wengi hata hawajui wanajadili nini bungeni mpaka aone kwenye gazeti ndio anashtuka kumbe hili nalo limekuwa hivi au vile!

Kuichagua ccm kuanzia ngazi ya chini mpaka Taifa ni janga tena janga baya kuliko ukimwi na kansa hivyo tufike mahali tuseme basi imetosha kwa waliyo tutenda.
 
usingizi ni noma inabidi tuweke maji ya baridi pipa zima kabla ya kupitisha kitu wabunge wote wa ccm lazima wanawe uso.
 
Ndugu,

Najaribu kufikiri kwa sauti jinsi muswada utakapokuwa unajadiliwa tena bungeni, nahisi kama vile hapatakuwa na vijembe vya 'Acha waondoke......, wamezoea...., sisi tutapitisha......, hamna lolote.......' Nahisi pia hapatakuwa na vicheko vile na kugonga meza kwa mtindo wa kuzomea.

Pamoja na hayo sifikirii upande wa pili kuwa na vijembe vya 'kuondoka kwetu ni tija kwa watanzania......., Sisi ni makini...., Mbona muswada umerudi n.k, n.k
 
Mwalimu Nyerere alishasema dhambi ya kubagua haiishi lazima itaendelea kuwala tu. Walijiona wao ni wamoja kwa kuwadharau CDM bila kujali ukweli na haki, sasa ile dhambi ndo inawala na wasiporudi na kujisafisha itawamaliza kabisa. Hiki chama sijui kina ndumba gani, yaani watu na akili zao wanashindwa kufanya kile wanachoamini ni ukweli, wanabaki kupiga meza tu. Yaani muda mwingine huwa naona huruma kweli.
 
Back
Top Bottom