Usaliti wa Wabunge wa CCM kwa wananchi...

Wabunge wa CCM si woga tu ni wajinga hawajui kilichowapeleka bungeni, inashangaza sana hivi mtu mwenye akili timamu anaweza kufumbia macho uozo unaofanywa na mawaziri? Jamani wabunge wa CCM mwogopeni Mungu.
 
kipimo cha kujua kiongozi mzalendo na yule bendera fuata upepo ni sasa hivyo watanzania fungueni mboni za macho yenu mu-waone viongozi mnaotarajia watawawakilisha ili mpate maisha bora katika nchi yenu yanye asali na maziwa tele
 
Hawana sababu ya kusaini kwani azimio la wabunge wa CCM ni kuwataka mawaziri wajiuzulu, nao wameitikia. Hivyo hoja ya zito haina mshiko
 
Nasikia wabunge wa CCM waliosaini kutokua na imani na waziri mkuu ni watano tu hii inaonyesha kuwa maslahi ya chama chao ni bora kuliko taifa hawa ni wasaliti watanzania tuwaazibu kwa njia ya kura.

Kama wewe ndiye ungekuwa Rais wa nchi hii ungekuwa umevunja katiba kwa kulazimisha bunge lote kuwa na msimamo mmoja unaoutaka.

Kila mtu analindwa na katiba kwa msimamo wowote hata kama atatofautiana na watanzania wote milioni 40.

Kila mtanzania kwa wakati wake ataelewa msimamo wake kwa muda wake kama ni sahihi au si sahihi. Jenga hoja kubadili misimamo ya wanaopingana na msimamo wako ipo siku watakuelewa
 
kwenye orodha ni namba 55 na 64 labda ni yule mbunge wa CUF na yule wa rufaa katika mahakama
 
Nilivyowasikia siku ile Mh. Kessy, Ester Bulaya na wengine toka CCM nilijua sasa kwisha kazi, kumbe wanafiki watupu, wanastahili hukumu ya kutupiwa mawe hadi wafe. Uzuri ni kuwa siku hizi Tz tunajua nini kinaendelea, hap wanafiki tutakutana nao tu mbele ya safari
 
Wakiamua kusimama kidete wabunge wa ccm wanaitishiwa mkifanya hivyo bunge likivunjwa uchaguzi ukirudiwa hakuna ambae ana uhakika wa kurudi na wengi wanajua walichakachua ndo maana wanakua warahisi kufyata mkia haraka sana
 
kinachopatikana wote siwanafaidi blabla zakusikilizwa na wewe umesema
 
Nyakati na uelewa kwa sasa unawalazimisha kutenda wasichopenda kutenda na kutoa katika imani waliyokuwanayo awali
 
Kweli mungu ni wa ajabu sana...............angalia anavyouumbua unafiki wa ccm na wana ccm.....kweli nimeamini kazi ya mbwa sio kubweka ni kung'ata pia......wanaogoba kukolimbwa, kumwakyembewa, kumalimwa na kuchifupiwa
 
hii ni sehemu ya utetezi wa mh kigwangalla
Tatu, msisahau kitu kimoja cha muhimu kabisa. Kwamba, mimi ni Mbunge kutokea CCM na kama walivyo wengi wenzangu hatukusaini kwa sababu hatuwezi kuiangusha serikali ya CCM kwa hoja inayoletwa na Mbunge wa Kambi ya Upinzani! Mbunge wa Chama Tawala kuamua kuiangusha serikali ya chama chako ni sawa na kuamua kukata tawi la mti uliokalia, kwa vyovyote vile utaanguka nalo! Simple logic! Mfumo wa Bunge letu ni wa Westminster, na hivyo kuna kambi ya Upinzani (yenye interest ya kutaka kuiangusha serikali inayotawala) na Kambi ya Serikali (ambayo ina interest ya kutaka kuilinda serikali yake). Kwa maana hiyo sisi wabunge wa CCM tuna jukumu la kuilinda Serikali inayopatikana kutokana na sisi kuwa majority. Serikali ni lazima i-enjoy majority status ndani ya Bunge ili nchi itawalike kwa amani na utulivu, japokuwa haimaanishi kuruhusu ubadhirifu na ndiyo maana kwenye Party Caucus wabunge wana nguvu na fursa ya kusema chochote dhidi ya serikali ya Chama Chao. Kuna wengine wanataka Bunge liwe Bunge huru (ama 'An Indipendent Power House') disregarding political opinions/inclinations/affiliations na serikali iwe serikali, hii haiwezekani kwa katiba tuliyonayo leo. Tubadilishieni kwanza katiba na mfumo wa kufanya kazi ndipo mtutake tufanye hayo mnayoyatamani.

Nadhani nimejiweka wazi bila unafiki, sasa tujadili kwa hoja siyo kwa hisia na matusi kama hatukwenda shule vile.
 
Back
Top Bottom