Usaliti wa waandishi: Mmoja Atimuliwa kwa kuandika habari za polisi

Pia tukumbuke kuwa Bw.Ngessi hamiliki chombo cha habari ni mwajiriwa anayeripotia chombo fulani cha habar ambacho kina muhariri habari tujiulize kwa nini muhariri alikubali kutolewa habari hiyo kama naye sio mnafiki
 
Hawatafanikiwa kwani usalama wa CCM wamejipenyeza everywhere
Angalieni namna waandishi wa habari wanavyoanza kusalitiana kuhusu misimamo yao ya kususia habari za kipolisi baada ya kifo cha mwangosi. Nimeikuta hii Tanzania Daima..............................

MWANDISHI wa habari wa Radio Free Afrika mkoani Mara, Maxmilian Ngesi, amefukuzwa uanachama na Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara ( MRPC ) baada ya kukiuka makubalino ya chama hicho yaliyoafikiwa juzi ya kutoandika kabisa habari za Jeshi la Polisi.

Akizungumza na Tanzania Daima, Mwenyekiti wa (MRPC ) Emmanuel Bwimbo, alisema kuwa Ngesi amekiuka makubaliano ya waandishi wenzake na chama kwa ujumla baada ya kusikika akitangaza habari za Jeshi la Polisi kwa kumkariri kamanda wa polisi wa mkoa wa Mara.

Bwimbo alisema kuwa kitendo hicho kinaonyesha jinsi gani mwandishi huyo alivyokiuka makubaliano ya pamoja na kuwasaliti wenzake ambao wamekubaliana kwa pamoja kuwa hawataandika habari za jeshi hilo kutokana na kuzuiwa waandishi kutoandamana katika maandamano ambayo yaliitishwa nchini kote kulaani kitendo cha mauaji ya mwandishi wa kituo cha Chanel Ten, mkoani Iringa, Daud Mwangosi.

Alisema Ngesi kama mwanachama alitakiwa kutii maamuzi ya chama na tamko la chama chake kwa vile tamko hilo limewataka wanachama wote na siyo kwa mkoa wa Mara tu lakini pia baadhi ya mikoa imetoa matamko na misimamo hiyo lakini cha kushangaza yeye amekaidi na kwenda kinyume.

Alisema kamwe chama hicho hakiwezi kuvumilia mwandishi atakayekiuka agizo hilo na hatua ambayo imechukuliwa kwa Ngesi ni mfano kwa waandishi wengine hadi hapo tamko hilo litakapotenguliwa.

MY Take: Je watafanikiwa??
 
Udhaifu wao waandishi huu hapa:
1. Hawana regulatory body inayoshughulikia mambo yao. Vyama holela ndivyo vinavyotoa matamko yasiyo na mashiko.
2. Binafsi wanaongozwa na tamaa na shuruti za wale wanaowamiliki.
3. Umasikini wa fikira kutokana na uwezo mdogo wa kielimu
4. Ni mashabiki wa siasa hivyo kushindwa kuandika story yenye uhalisia na badala yake wanaongozwa na utashi.
5. Si watu huru kwani hawawezi kuamua mambo yao wenyewe. Je mwandishi wa uhuru atagomea kuandika habari za
polisi? Je siyo waandishi?
6. Hakuna vigezo vya kutambua mwandishi anatakiwa awe na sifa gani.

Haya yarekebishwe kwanza ndio wawe na umoja. Sasa subiri wanakuja kutoa hoja za ajabu, utaniambia.
 
Nakubaliana nawe 100%
 
Ni upumbavu waandishi kugomea kuandika habari za polisi, ni kama mkulima kugoma kulima eneo fulani la shamba lake kwa kufikiri analikomoa shamba. Sanasana ataua watoto tu.

Halafu muandishi ndiye anayepitisha habari ichapwe kwenye gazeti?

Mbona hatusikii chochote kuhusu Mhariri, printer etc walioihariri na kuichapa habari hii? Wamefanywa nini?

Huwezi kupinga udhalimu mmoja, wa polisi kuua waandishi, kwa kutumia udhalimu mwingine wa kulazimisha waandishi kutoandika habari za polisi.

Tatizo waandishi wa habari wanaosusia wamekosa muelekeo, wanaona kwamba wanatoa favors kwa wanaowaandika , sijui kwa sababu washaharibiwa na rushwa au vipi.

Habari ni biashara. Mtumia habari ni mwananchi. Mkisusia habari za polisi mnapunguza wigo wa uandishi na kumnyima mwananchi habafi. Wengine tunapata kuona ugumu wa matatizo hata kwa kusoma nukuu za wadhalimu. Gazeti moja likitunyima, tutasoma lingine lenye habari.

Na nguvu za soko zitaamua.

Acheni kususia mapambano kitoto. Ningekuwa mimi muandidhi ndo ningewaandika polisi zaidi. After all, is not the pen supposed to be mightier than the sword, and by induction, the keyboard than the gun?
Ndivyo walivyo, yaani kuandika habari za mtu au taasisi fulani ni kama "favor".
Ingetakiwa waandishi wawaexpose mapolisi extensively na waandike habari zao na kupost picha za kila tukio ambalo polisi wanahusika .... hii ingesaidia kuwaweka polisi machoni pa wananchi na kuwavuta waandishi wa habari karibu na upande wa wananchi.

Siyo kuwafuata watu kwenye kumbi za starehe na kuwaomba elfu ishirini ili picha zao zitokee.
 
Hapa tatizo si waandishi wa habari bali jamii kwa ujumla. Watanzania wanasifika kwa kusalitiana na kukosa msimamo na uoni wa mbali. Watazame madaktari na walimu na wafanyakazi wengine waliotishia kugoma. Kiko wapi na wako wapi zaidi ya kila mwenye nafasi kutafuta namna ya kujisogeza kwa serikali ili imkatie chake na wenzake wajiju? Jamii ya hovyo huzalisha watu wa hovyo kuanzia rais hadi mfagiaji. Nenda kila idara ujuayo utaambua kusalitiana na kuchuuzana. Kinachogomba zaidi ni watanzania kuabudia mali hata kama imepatikana kwa kugawa au kuuza tigo.
 
mi nilishasema tangu mwanzo, huu mgomo ni kosa kubwa ambalo waandishi wanafanya kwani hauna tija na utawaathiri raia wa kawaida na sio serekali.
Wanapoteza muda wao.

Hivi kwa nini kitu rahisi kukiona kama hiki kinakuwa kigumu sana kueleweka mkuu?

Mie ninaona kama wewe. Kwamba kama kweli polisi ni wadhalili, na waandishi wanagoma kuandika habari za polisi, udhalili wa polisi hautaonekana vizuri.

Polisi watafanya maovu, RPC ataitisha mkutano ili kujibu maswali na kuwapa wandishi wa habari nafasi kutoa taarifa kwa wananchi, waandishi wa habari watashindwa kuripoti kwa sababu wameshajifunga kwa mgomo wao wa kuandika habari za polisi.

Mwisho wa mambo maovu ya polisi yanaendelea bila kumulikwa vizuri, wananchi wanazidi kuumia kwa umajununi wa waandishi wanaofikiri kuandika habari ni kumpa mtu favor.

Tutafika hivi?

Kama polisi ni wadhalimu, suluhisho si kususia habari zao, suluhisho ni kuziandika maradufu.
 
Hapa tatizo si waandishi wa habari bali jamii kwa ujumla. Watanzania wanasifika kwa kusalitiana na kukosa msimamo na uoni wa mbali. Watazame madaktari na walimu na wafanyakazi wengine waliotishia kugoma. Kiko wapi na wako wapi zaidi ya kila mwenye nafasi kutafuta namna ya kujisogeza kwa serikali ili imkatie chake na wenzake wajiju? Jamii ya hovyo huzalisha watu wa hovyo kuanzia rais hadi mfagiaji. Nenda kila idara ujuayo utaambua kusalitiana na kuchuuzana. Kinachogomba zaidi ni watanzania kuabudia mali hata kama imepatikana kwa kugawa au kuuza tigo.

Mie bado sijaona kugoma kuandika habari za polisi kutamsaidiaje Mtanzania wa kawaida ambaye, kama kweli polisi wana matatizo, anatakiwa ayajue zaidi matatizo hayo.

Sasa kugoma kuandika habari za polisi kutasaidiaje kuyaanika zaidi matatizo ya polisi?
 
Hivi kwa nini kitu rahisi kukiona kama hiki kinakuwa kigumu sana kueleweka mkuu?

Mie ninaona kama wewe. Kwamba kama kweli polisi ni wadhalili, na waandishi wanagoma kuandika habari za polisi, udhalili wa polisi hautaonekana vizuri.

Polisi watafanya maovu, RPC ataitisha mkutano ili kujibu maswali na kuwapa wandishi wa habari nafasi kutoa taarifa kwa wananchi, waandishi wa habari watashindwa kuripoti kwa sababu wameshajifunga kwa mgomo wao wa kuandika habari za polisi.

Mwisho wa mambo maovu ya polisi yanaendelea bila kumulikwa vizuri, wananchi wanazidi kuumia kwa umajununi wa waandishi wanaofikiri kuandika habari ni kumpa mtu favor.

Tutafika hivi?

Kama polisi ni wadhalimu, suluhisho si kususia habari zao, suluhisho ni kuziandika maradufu.

Mkuu tatizo wa tz tuemzoea kukurupuka bila ya kufanya utafiti wa jambo.
Pia tuna tatizo la mapenzi yalopitiliza na kushabikia kila kitu bila kufikiri vya kutosha kwa kudhani tunamkomoa
au kumnufaisha mtu fulani, kumbe inakula kwetu wenyewe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom