Usaliti wa waandishi: Mmoja Atimuliwa kwa kuandika habari za polisi

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Angalieni namna waandishi wa habari wanavyoanza kusalitiana kuhusu misimamo yao ya kususia habari za kipolisi baada ya kifo cha mwangosi. Nimeikuta hii Tanzania Daima..............................

MWANDISHI wa habari wa Radio Free Afrika mkoani Mara, Maxmilian Ngesi, amefukuzwa uanachama na Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara ( MRPC ) baada ya kukiuka makubalino ya chama hicho yaliyoafikiwa juzi ya kutoandika kabisa habari za Jeshi la Polisi.

Akizungumza na Tanzania Daima, Mwenyekiti wa (MRPC ) Emmanuel Bwimbo, alisema kuwa Ngesi amekiuka makubaliano ya waandishi wenzake na chama kwa ujumla baada ya kusikika akitangaza habari za Jeshi la Polisi kwa kumkariri kamanda wa polisi wa mkoa wa Mara.

Bwimbo alisema kuwa kitendo hicho kinaonyesha jinsi gani mwandishi huyo alivyokiuka makubaliano ya pamoja na kuwasaliti wenzake ambao wamekubaliana kwa pamoja kuwa hawataandika habari za jeshi hilo kutokana na kuzuiwa waandishi kutoandamana katika maandamano ambayo yaliitishwa nchini kote kulaani kitendo cha mauaji ya mwandishi wa kituo cha Chanel Ten, mkoani Iringa, Daud Mwangosi.

Alisema Ngesi kama mwanachama alitakiwa kutii maamuzi ya chama na tamko la chama chake kwa vile tamko hilo limewataka wanachama wote na siyo kwa mkoa wa Mara tu lakini pia baadhi ya mikoa imetoa matamko na misimamo hiyo lakini cha kushangaza yeye amekaidi na kwenda kinyume.

Alisema kamwe chama hicho hakiwezi kuvumilia mwandishi atakayekiuka agizo hilo na hatua ambayo imechukuliwa kwa Ngesi ni mfano kwa waandishi wengine hadi hapo tamko hilo litakapotenguliwa.

MY Take: Je watafanikiwa??
 
Nimeongea na mwanahabari mmoja sasa hivi wa Musoma, amenithibitishia kuwa kumbe mwandishi Ngessi ni katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Mara. Kweli wanahabari kazi wanayo
 
Hamna haja ya kumfukuza kwani jana Dr.kitila alikiuka na kushiriki kwenye TBC1.

MSIMUONEE MWANDISHI.
 
Watafanikiwa endapo watakuwa na msimamo huo ..huyo atakuwa amehongwa syo bure
 
Nilieleza awali kuwa hizi bahasha za kaki na uswahiba wa waandishi wengine na serikai/CCM lazima utawasambaratisha. Kwani hamkuona the very first days alichofanya Meena kuwatukana waandishi kwa kuwaletea Waziri wa mambo ya ndani anayewaongoza Polisi waliomuuwa mwenzao. Ninavyoona baada ya miezi miwili umoja wa wanahabari watasambaratika na kuwepo ka kundi kubwa la wasaliti ambao watawahenyesha sana waandishi wenye msimamo wa haki zao. Uvumilivu wa waandishi watakaobakia na msimamo, utawezekana kama watavumilia kutokuitwa kwenye habari za vibahasha. Njaa mbaya sana wakati mwingine.
 
Nimeongea na mwanahabari mmoja
sasa hivi wa Musoma, amenithibitishia kuwa kumbe mwandishi Ngessi ni
katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Mara. Kweli wanahabari kazi
wanayo

tatizo ndo liko hapo ..kwa mkoa wa Geita mwandishi David Azaria ni mjumbe sekretariet ya CCM mkoa
 
tatizo ndo liko hapo ..kwa mkoa wa Geita mwandishi David Azaria ni mjumbe sekretariet ya CCM mkoa
Jane Mihanji Mhariri wa gazeti sijui Radio Uhuru!!! Wanapoweka maazimio wawe wanaangalia pia maslahi ya wenzao
 
Nimeongea na mwanahabari mmoja sasa hivi wa Musoma, amenithibitishia kuwa kumbe mwandishi Ngessi ni katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Mara. Kweli wanahabari kazi wanayo

CCM is great vempire tutalikatakata pole pole mpaka likwishe kabisa!!!
 
Kuelekea 2015 tutakuwa tumeshawajua kila mwandishi kwa rangi na sura yake,wamezoea bahasha za khaki sasa zinawaumbua mchana kweupee
 
Ni upumbavu waandishi kugomea kuandika habari za polisi, ni kama mkulima kugoma kulima eneo fulani la shamba lake kwa kufikiri analikomoa shamba. Sanasana ataua watoto tu.

Halafu muandishi ndiye anayepitisha habari ichapwe kwenye gazeti?

Mbona hatusikii chochote kuhusu Mhariri, printer etc walioihariri na kuichapa habari hii? Wamefanywa nini?

Huwezi kupinga udhalimu mmoja, wa polisi kuua waandishi, kwa kutumia udhalimu mwingine wa kulazimisha waandishi kutoandika habari za polisi.

Tatizo waandishi wa habari wanaosusia wamekosa muelekeo, wanaona kwamba wanatoa favors kwa wanaowaandika , sijui kwa sababu washaharibiwa na rushwa au vipi.

Habari ni biashara. Mtumia habari ni mwananchi. Mkisusia habari za polisi mnapunguza wigo wa uandishi na kumnyima mwananchi habafi. Wengine tunapata kuona ugumu wa matatizo hata kwa kusoma nukuu za wadhalimu. Gazeti moja likitunyima, tutasoma lingine lenye habari.

Na nguvu za soko zitaamua.

Acheni kususia mapambano kitoto. Ningekuwa mimi muandidhi ndo ningewaandika polisi zaidi. After all, is not the pen supposed to be mightier than the sword, and by induction, the keyboard than the gun?
 
Ni upumbavu waandishi kugomea kuandika habari za polisi, ni kama mkulima kugoma kulima eneo fulani la shamba lake kwa kufikiri analikomoa shamba. Sanasana ataua watoto tu.

Halafu muandishi ndiye anayepitisha habari ichapwe kwenye gazeti?

Mbona hatusikii chochote kuhusu Mhariri, printer etc walioihariri na kuichapa habari hii? Wamefanywa nini?

Huwezi kupinga udhalimu mmoja, wa polisi kuua waandishi, kwa kutumia udhalimu mwingine wa kulazimisha waandishi kutoandika habari za polisi.

?

Inahitaji mjadala mrefu hii kitu
 
Nimeongea na mwanahabari mmoja sasa hivi wa Musoma, amenithibitishia kuwa kumbe mwandishi Ngessi ni katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Mara. Kweli wanahabari kazi wanayo

issue hapa ni kukiuaka makubaliano kwenye press club yao lakini mimi nafikri ni muhimu kupata maoni ya max mwenyewe ili tujue chanzo cha kukiuka makubaliano. na unajua suala lilompata mwangosi linabidi lilaniwe na waandishi wote si wanazi wa ccm,cdm,cuf nk
 
mi nilishasema tangu mwanzo, huu mgomo ni kosa kubwa ambalo waandishi wanafanya kwani hauna tija na utawaathiri raia wa kawaida na sio serekali.
Wanapoteza muda wao.
 
nitanunua gazeti litakolokuwa na habari za kipolisi na michezo hasa timu ya simba na barcelona!
 
Maxmillian Ngessi ni katibu mwenezi wa magamba mkoa wa Mara kwahiyo lisingekuwa jambo rahisi nayeye kususia shughuli za polisi kwakuwa ccm hawajasikitishwa na kifo cha Mwangosi.
 
Back
Top Bottom