Elections 2010 Usalama wa Taifa wakanusha tuhuma za Dr. Slaa

Status
Not open for further replies.
Naona wootee waliotajwa wanakimbilia kukanusha....wanaogopa vivuli vyao??? hawajui kuwa kila jambo lililotendeka sirini litadhihirika machoni kwa wote, na baadao, gachuma naye kaja juu kama moto wa kifuu
 
Source: Mimi mwenyewe
Nimeipenda hii nadhani itakuwa valid and reliable. Binafsi sishangai hao jamaa kupinga we unadhani wangeweza kusimama na kusema ni kweli? Watu wenyewe have scrupulous and dead consciences unategemea nini!
 
kwanza kabisa sina chama chochote cha siasa. pili nimekuwa nikihudhuria mahakami mara kwa mara sijawahi kusikia mtuhumiwa anakubali kuwa ametenda kosa. hivyo TISS hawana jipya. ukweli huwa unauma. wasingetokea hadharani kusema.
 
TISS wangekaa kimya tungesema wameiba ndio maana hawana la kutueleza na sasa wamejitokeza kutuhabarisha tunasema wanajichanganya. Ni lipi jema? Binafisi naona dunia ya sasa ni ya uwazi zaidi si vibaya kwa TISS kujitokeza kuwaeleza wananchi jambo linaloweza kuhatarisha usalama wa Taifa hasa kama itaaminika miongoni mwetu na wale wasipenda kutafiti kabla ya kusema kwamba TISS wamechachua kura za SLAA. Good show

Malaria sugu in action
 
Mwizi akifanya uhalifu ni ngumu sana kukubali kosa hivyo si ajabu kuona hili.Watanzani tuamke sasa wakati wa mabadiliko ni huu.Serikali naidara zake zote zipo chini ya ccm toka tupate uhuru kilichobaki ni sisi kuamua kuleta mabadiliko ya kweli through peoples power.
 
nchi hii, Usalama wa Taifa wanasahau wajibu wao, wanasahau kazi iliyowaweka pale.
ni hawa usalama wa Taifa waliowaandama kina Slaa walipoamua kutaja mafisadi hadharani, mimi nawashangaa, Hivi ajira zao utolewaje, unaweza ukakuta ni genge la watoto wa kina Lowassa, Mkapa, Rostam na kina Karamagi
 
Sasa hapo wachunguze nini, kwani kuna maombi yeyote yalipelekwa usalama wa taifa kuomba kuchunguza.

Kuchunguza tuhuma ni mpaka wapelekewe maombi, are you serious? Wenzetu wako mbali hata wakisoma gazeti limetoa tuhuma wanafanya uchunguzi.
 
Kwa mara ya kwanza tangu uhuru, Usalama wa Taifa wameongea na vyombo vya habari. Acha watulie. Sauti ya Umma haiwezi kuzimwa na Usalama wa Taifa.
 
Kwa mara ya kwanza tangu uhuru, Usalama wa Taifa wameongea na vyombo vya habari. Acha watulie. Sauti ya Umma haiwezi kuzimwa na Usalama wa Taifa.

Ama kweli hadi JK aondoke madarakani, Taifa litakua nyang'anyang'a
amejizungushia kundi la wasanii na waleta mizaha katika Ofisi za umma, wewe ujiulizi kwanini Taarifa za siri zinamfikia Dr Slaa, ni kwakua Waadilifu hawakubaliani na utani wa wasanii hawa, Na bado mtajionea Mengi.
 
Mkuu wa idara ya usalama wataifa amejitokeza leo na kukanusha tuhuma zilizotolewa jana na Dr.Slaa kuhusiana na tuhuma za idara hiyo kushiriki katika zowezi la wizi wa kura za urais. Akizungumza na TBC leo Mchana kwenye taarifa ya habari Mkuu wa idara hiyo amesema

"Dr.Slaa ameingizwa mjini na na watu waliyo jifanya ni usalama wataifa,hakuna kitu kama hicho, sisi hatuna chama, tupo kwajili ya taifa na siyo chama chochote. Na mtuka kama anaushaidi ajitokeze na auweke wazi.. Najua ameingizwa mjini na na watu waliyo jifanya ni usalama wa taifa ambao sisi hatuwatambui."


Style hii aliyo tumia mkuu wa idara hii ni style inayotumiwa na Russia kuwakana watu waliyo tumwa kufanya kazi na atimaye kuboronga na kukamatwa au kugundulika, Njia hii inatumika kujisafisha...

Nakumbuka mwaka 1978 Mzee wangu alitumwa kwenda kufanya upelelezi nchini Uganda akiwa na wenzie 8, waligundulika na kukamatwa Na serikali iliwakana na kusema haiwatambui na haijawatuma bali walikuwa na mambo yao binafsi...


Na muomba Dr.Slaa asikatishwe tamaa na majibu haya bali akusanye ushaidi na kuutoa hadharani ili kuwaumbua hawa wote..

Mkuu kweli hawa jamaa wamebanwa mbavu maana ingekuwa uwongo wala wasingetoka kujibu, mambo mangapi ya uwongo huwa wanayapuuza?? sasa wameona wamewekwa uchi
 
anasema dr slaa alete USHAIDI KAMA TISS walitumika ktk uchakachuaji wa matokeo ya UCHAGUZI MKUU,

ushauri kwa jack zoa, we subiri kuumbuka, dr atakupa tu ushaidi unaoutaka
 
Hata epa mwanzoni watu walijidai leten ushahidi. ngoja aumbuke huyo ndo atakapomjua Dr wa ukweli ni nani
 
Zoa alifikiria watu huwa wanazungumza ovyo kama CCM yake walivyo!? watu usawa huu wanakwenda kwa datas! Go Dr. go and fool the fools!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom