Elections 2010 Usalama wa Taifa wakanusha tuhuma za Dr. Slaa

Status
Not open for further replies.
nimeliona tangazo linapita ITV nikashaanga na haramia kinana linasema siku hiyo lilikuwa nachingwea
 
Website yenyewe haiko hewani. Usiwe mjinga kama wenzako humu JF

Tafadhali bwana mdogo, najua umejiunga jana, sasa embu pitia kanuni za JF kabla haujafukuzwa kwenye hili jukwaa, unapata wapi ujasiri wa kuita watu wajinga? period! Next time kuwa makini na lugha unayotumia.
 
Hayo ht mimi nimeyasikia bt Usalama watapotea ghafla kwani Dr Slaa anapata info nyingi tu from them.So muda si mrefu damu itamwagika
 
leo nec watatangaza matokeo ya majimbo yote lakini hawatatangaza mshindi mpaka

watakapomaliza kusikiliza malalamiko ya chadema
 
May be huo ndo wajibu wake huyo Afisa,lakini akumbuke Dr Slaa huwa habahatishi..
 
Tanzania Security Services Deny Rigging of Election


November 04, 2010


By Wilfred Mwakalosi and Sarah McGregor


Nov. 4 (Bloomberg) -- Tanzania's Intelligence and Security Service rejected allegations by an opposition leader that results from the Oct. 31 election were rigged.

Chadema, the party led by presidential candidate Wilbrod Slaa, said yesterday that results announced by the National Electoral Commission were different from those released at polling stations. Slaa said security agents had tampered with both the results and the number of votes cast, Agence France- Presse reported yesterday.

"The department is not involved in whatsoever has been stated by the Chadema presidential aspirant, nor will it be used by anyone for personal gain," Jacky Zoka, deputy director- general of the service, told reporters today in Dar es Salaam, the commercial capital.

President Jakaya Kikwete won the most votes in 159 of 183 constituencies counted so far, the electoral commission said today.

Ibrahim Lipumba of the Civic United Front has the largest share of votes in 21 constituencies, while Slaa has the most votes in the three other constituencies, the commission said in an e-mailed statement. Tanzania has 239 constituencies.
 
Aaaaghhh!

Mungu epusha mbali, this' too low for TISS. Kwanini wanajibu? Nani amewashauri wafanye jambo hili? Kwanini wasiwaachie wanasiasa?

Dah...

:A S angry:

Kilichowazi ni kwamba hakuna muafaka ndani ya TISS kuhusiana na mpango wa kuchakachua kura za uraia, hata za ubunge.
Na, NAIBU MKURUGENZI WA TISS anachoJARIBU KUFANYA NI KUONYESHA KUWA KUNDI ANALOLIWAKILISHA/LIONGOZA linaji-exonerate na mipango ya kuchakachua kura. Kwamba................sisi (kundi letu)/mimi 'sivimo'
 
Wameitisha Press Conference imehutubiwa na Naibu Mkurugenzi bwana Jacky Mugenzi kuwa hawahusiki kwa namna yoyote na uchakacghuaji wa kura za urais.

Source: Mimi mwenyewe

Usalama wa Taifa kuitisha Press Conference?
Siku zote wao wapo kama hawapo na kamwe hawaongei na vyombo vya habari.
Haya basi atuambie kila kitu kabisa mpaka bajeti yao.

Wanajenga ukuta kwa sababu wameona ufa.
 
Siku hizi wanaongea mkuu. mambo ya siri yamepitwa na wakati. Ukitaka mfano soma hapa chini:

BBC News - MI6 chief Sir John Sawers says torture illegal

Mkuu nimesema kwa Tz haijawahi na nimefurahi kuona ila ameanza vibaya, angeanza kwa tamko zito katika mazingira ambayo wangejenga heshima kubwa na kuonekana kama chomba cha kweli cha umma na si kutokea kujibu tuhuma tena juu juu kama alivyofanya huyo mwakilishi wao. Naamini kwa dhati kwamba ukiondoa mgawanyiko uliopo ndani ya TIS (na ndani ya kila eneo) bado TIS wana nafasi nzuri ya kutumikia umma na si watawala na kundi dogo la wahalifu. Kwa kuwa ni mara ya kwanza waangekuja na tamko la kuwa katikati na si tamko lenye maneno ya vijembe kama vile, "Slaa ameingizwa mjini" na kwamba "anaona matokeo yanamuendea vibaya" kauli ambayo haitofautiani sana na ya Riz1.
 
Je palikuwa na haja TISS kukubali au kanusha allegations za Slaa. Binafasi nina shaka na results za NEC. One needs to look at the numbers of Kuga Mziray. Amemshinda Lipumba (kwa small margin) sehemu nyingi.All of a sudden amekuwa famous. Who financed his campaign? Vilevile kura zilizoharibika , ni average kati ya 1.5% to 3%.
 
Jamani ni kheri mseme TISS unajua mkisema UWT always najua umoja wa wanawake Tz.
 
"Lu-ma-ga;Ili kupata muafaka ni bora malinganisho ya madai ya Dr.SLAA dhidi ya uchakachuaji yakafanyiwa kazi kuliko kukanusha tu.Hapa inabidi wawe objective zaidi ya kuwa subjective. SLAA amesema nazo takwimu basi zifanyiwe kazi kuliko kuendelea kurumbana.Time is running out you know!!!!!"

Well said Lu-ma-ga
 
Kama kuna idara ya serikali inatakiwa kuwajibika kwa uhalifu dhidi ya wananchi ni hii ya usalaama wa Taifa ambayo kutokana na utendaji kizembe nchi imepata hasara kubwa kabisa. Hapa kuna moja kati ya facts hizi mbili:

Ya kwanza ni labda hawaelewi kwamba wajibu wao si kumlinda Rais na viongozi wa serikali tu bali kulinda hujuma dhidi ya taifa kama zile za kufuru ya wizi uliofanyika Benki Kuu wa EPA, Benki Kuu ndiyo kidundio (Apex) cha moyo wa taifa lolote ambapo hujuma yoyote dhidi yake ni sawa na angamizo la uchumi. Zipo pia hujuma za Mikataba ya rushwa, Richmond, Meremeta, Kiwira n.k. zimetendeka wakiwa busy "kuwalinda " wahujumu hawa wa uchumi wetu ambao kwa kweli ndiyo maadui wa kweli wa nchi yetu. Na sasa ndiyo tunapata kichefuchefu kabisa kusikia wamehusika na vote rigging zinazolenga kuharibu utashi wa wananchi!

Pili ni kwamba huenda wanadhani wanapaswa kuwajibika kwa viongozi wanaowateua, lakini sijui kama wanajishughulisha kuelewa mishahara wanayolipwa inagharimiwa na nani.

Usalama wa taifa wa kwetu wanafanya kazi ki-primitive kwelikweli, hebu angalia; wenzetu kule Marekani walikuwa usalama wa Taifa wao waliogundua hila alizotumia Rais Nixon kushinda uchaguzi walimpeleleza, wakawakabidhi Polisi ambao waliwasilisha tuhuma Bungeni ambapo baada ya kuzithibitisha wengi walichukuliwa hatua na Rais kulazimishwa kuachia ngazi. Mambo ni hivyohivyo kule Uingereza ambako kina Chenge waligunduliwa kugawana rushwa ya ununuzi wa Rada na Ndege. Hapa hakuna cha Usalama wa Taifa wala kitengo cha upelelezi chenye ubavu wa kufanya hivyo, labda ni kwa sababu ya kulipwa fadhila ya kupewa ulaji na Rais ambaye anayo pia madaraka ya kuwaondoa hata kwa kuwaonyeshea kidole tu.

Kwa mtaji huu Usalama wa taifa wataendelea kuwa mzigo wa taifa na aibu kubwa kwa nchi yetu.

-------

Crystal Clear....Need we say more!!?

Self Unconsciousness is a serious weakness....?


Unco
 
Kukanusha tu hakutoshi maana shutuma za kuihusisha idara ya usalama na ukakachuaji wa kura haukuanza leo, hata rais Kikwete mwenyewe aliwahi kuitupia shutuma nzito idara hiyo kwa kusema kuwa, wakati wa chaguzi zote za ccm, idara hiyo ilikuwa inahakikisha ya kuwa idadi ya kura wanazopewa wagombea, siyo ile waliopigiwa na wajumbe, bali ni ile waliyopangiwa na idara yenyewa kulingana na wadhifa wa mhusika. utaratibu huu wa kuhamisha kura kutoka kwa mdongo na kumpa mkubwa aliodai ulikuwa unafanywa na idara hiyo ndiyo aliouita "kura za hitifaki." Sikumbuki kama idara ya usalama iliwahi kukanusha kuwepo kwa utaratibu huo. Inawezekana shutuma za sasa uenda zinatokana na hiyo historia ya idara hiyo ya huko nyuma. Na hivyo itakuwa vigumu, kujisafisha na hizi tuhuma za sasa bila ya kuzitolea maelezo shutuma alizoelekeza kwa idara hiyo rais aliyoko madarakani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom