Usalama wa abiria wa pikipiki uko wapi?

Mwanamosi

Member
Aug 9, 2010
73
0
Napenda kutoa tahadhari kwa wale wote wanaotumia usafiri wa pikipiki katika maeneo yenye shida ya usafiri ambako hakuna usafiri wa uhakika kuwa tujihadhari na waendesha pikipiki ambao wamebuni mradi mpya wa kuwapatia kipato.
Hivi sasa mwendesha pikipiki anakuchukua na akifika eneo fulani lisilo na watu wengi anapigia simu wenzake na kudai anataka kuporwa,kuuawa au vyovyote na wenzake hufika kwa kasi na kukushambulia huku wakikupora,na kuharibu mali ulizonazo.
Hii imethibika baada ya kesi zaidi ya kumi kuripotiwa huko segerea na nilibahtika kujua hilo baada ya jamaa yangu mmoja kukutwa na tukio la aina hiyo na hivi sasa bado yuko hospitali kutokana na kipigo alichopewa na kundi la "wahuni" hawa.
Nasikitika kusema kuwa hawa ni wahuni na imefika mahali wamekuwa kero kwa uendeshaji wa hovyo,"mishikaki",kutovaa helmet n.k ...hofu yangu ni kuwa kama segerea kuna kesi zaidi ya 10 je maeneo mengine ni wangapi washaumizwa nao? Jeshi la polisi linatazama kwa kisingizio hakuna ushahidi..natoa rai kwa wanajamii tuwe wa msaada tuwaambie ndugu na jamaa zetu wanaotegemea usafiri huu wawe wanajaribu kukariri namba za pikipiki husika ili isaidie polisi kuwatia nguvuni wenye tabia hii au la uwe na kumbukumbu ya mtu unaemkodi ili ukirudi kesho umtambue(labda ahame kijiwe ndio hutampata)
zipo kero nyingi ila kwa sasa nadhani tutazame usalama wetu (abiria) na tuwaambie wengine kuwa kuna wahuni wachache wenye tabia kama hii...natoa pole kwa waliokumbwa na mikasa ya aina hii na mingine inayohusisha ukorofi wa waendesha pikipiki.
 
Back
Top Bottom